Nchi za Afrika zagawanyika katika upigaji kura kuhusiana na Vita vya Russia na Ukraine, Tanzania yachagua kutofungamana na upande wowote

Nchi za Afrika zagawanyika katika upigaji kura kuhusiana na Vita vya Russia na Ukraine, Tanzania yachagua kutofungamana na upande wowote

Huu Ndio msimamo wa siku nyingi watoto wa siku hizi watakuwa hawajui .
Wakati Fulani Mwl Jk Nyerere alikuwa mwenyekiti wa jumuiya ya na mataifa yasiyofungamana na upande wowote.
Na Hii inasaidia kuepuka kugombana na yoyote.
 
Huelewi hata falsafa ya kutofungamana upande wowote ilikuwa inahusu nini!!
Wwe unaelewa ebu tueleze hata kwa ufupi Basi!? Maana nyinyi ndiyo mkisha gombana hata na wapenzi wenu mnatulazimisha na sisi tuchaguwe side! Watu Wazima Ovyoo!!
 
Uwepo wa majeshi ya Kenya na Uganda huko Somalia ni tofauti kabisa na hili na Ukraine na Urusi. Haya yapo kule Somalia kwa umbrella ya AU; urusi amekwenda Ukraine kwa kutaka kuitawala Ukraine na kuinyang'anya sovereignty yake.

Mgogoro wa Kenya na Somali kwenye bahari ya hindi haufanani na huu kabisa. Kenya na Somalia wanabishania mpaka wa majini na kuna tume ya usuluhishi inashughulikia mgogoro huo. Urusi haina mgogoro wowote wa mpaka na ukraine, bali tu haipendi serikali ya ukraine iliyochaguliwa na watu na inataka kuiondoa kabisa serikali ili kusudi iweke ya kwake.
Mkuu "Nyumba ya Nguchiro na mchwa", tofauti hizo ulizo orodhesha hapo nazifahamu barabara, lakini nikukumbushe, kabla ya jeshi la Kenya kuwa chini ya mwamvuli wa AU, walifanya uvamizi nchini Somalia, hata kama nia yao ilikuwa ni kuwashughulikia Shaabab. Mfanano wa uvamizi huo na wa Urusi upo, ila najua hutopenda kuangalia huko.

Mgogoro wa Kenya na Somalia kwenye bahari ya Hindi, hakuna tume yoyote inayoushughulikia kwa sasa. Swala hili limeamriwa mahakamani, lakini Kenya hakubaliani na uamzi huo, kwa hiyo anatishia vita endapo Somalia itafuata uamzi wa mahakama na kutafuta uwekezaji katika maeneo hayo.

Unasema Urusi haina mgogoro wowote wa mpaka, lakini anatumia visingizio, ikiwa ni pamoja na kulinda waasi wa nchi hiyo ili atimize lengo lake kuu la kuzuia NATO kufika mpakani kwake. Kama unalielewa vyema hili, pengine utaona sababu hasa ya uvamizi huo.

Ulaya na Magharibi kwa ujumla hawawezi kujiondoa lamani kutokana na uvamizi huu.

Nguchiro na Mchwa wakiwa ndani ya Kichuguu kama majirani ni lazima waheshimiane. Nguchiro akileta ukorofi na kutaka misaada ya kuhatarisha maisha ya Mchwa ndani ya nyumba yao, hakika ni lazima mchwa nao watafute njia zozote za kujihami wasidhurike, ikiwa ni pamoja na kuwashambulia akina Nguchiro kama wanajitia ujuaji kwa kiburi cha wafadhiri toka nje.
 
Ni muafrika mjinga pekee atakae jihusisha na mambo ya migogoro ya mabeberu.

Kukaa kimya napo ni jibu.
Undumila kuwili na wala hakuna maana yoyote zaidi ya kutaka misaada kutoka kote kote.
 
Zanzibar kama nchi tunaburuzwa na serikali ya JMT inayotuwakilisha UN. Wazanzibari tunapinga vamizi la Ukraine maana linafanana na vamizi alofanya Nyerere Zanzibar. Tungekuwa na kiti chetu UN, tungepiga kura ya kukemea vamizi la Putin kama ndugu zetu wa Oman walivyopiga. Kuwakilishwa UN na machogo ni kero.
 
Mie nikajua tigray ni huko ethiopia!
Tigray ni huko Ethiopia ila jimbo ni semi-autonomous. Eritrea imekuwa ikishirikiana na Ethiopia kuwaadhibu Tigray ambao wanapakana na Eritrea.

Eritrea ilijitenga na Ethiopia 1993, na wakati huo Watigray ndiyo walikuwa watawala wa Serikali Kuu ya Ethiopia
 
Kama kuna jilani amevamiwa pale kijijini harafu ukunga unapigwa ili mtoke kuonyesha kupinga uvamizi,wenzio wanatoka wewe unajifungia ndani hapa kimsingi upo pamoja na mvamizi, kwakuwa wewe nimwana jumuia na jumuia inapinga uvamizi, hupaswi kujifungia''
 
Tanzania inawapinga wote kwa kuanzia Ukrain kutumika na USA kuichokoza Russia na Russia kiipiga Ukrain ingawa pia ilikuwa haiepukiki huwezi kupiga kura ya upande wowote ikiwa hukubaliani na wote.
 
Back
Top Bottom