Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Kubaki neutral ni kutokupiga kura kabisa; ukishapiga kura halafu kura yako ikawa ya kukubali pande zote, hiyo ni kukosa wa decisiveness, yaani kufuata upepo kokote utakapoenda na lengo lake kubwa huwa ni kukwamisha uamuzi kimya kimya.to abstain maana yake imebaki neutral, haipo upande wowote, yaani haikupiga kura.
Angalia: kwenye mkutano wenye wajumbe 19 unaotambua quoruma ya wajumbe 15, iwapo jambo linatakiwa liamuliwa kwa simple majority (51%) , ikatokea wajumbe 8 wakasema ndiyo, wajumbe 7 wakasema hapana, na wengine 4 wakasema kotekote (kama tanzania), mkutano huo hautapitisha uamuzi wowote kwa vile simple majority ya quorum haitapatikana, kwani wale wa ndiyo watakuwa ni 42%, wa hapana ni 36% na hao wa kotekote ni 26% kwa hiyo simple majority haitapatikana. Iwapo wale waliopiga kotekote wasingepiga kura kabisa, basi wale wa ndiyo wangekuwa 53% na wale wa hapana wangekuwa 47% na uamuzi ungepitishwa.
Kwa nini tupelekea mtu atuwakilishe kwenye mkutano halafu asiwe na msimamo?