Uwepo wa majeshi ya Kenya na Uganda huko Somalia ni tofauti kabisa na hili na Ukraine na Urusi. Haya yapo kule Somalia kwa umbrella ya AU; urusi amekwenda Ukraine kwa kutaka kuitawala Ukraine na kuinyang'anya sovereignty yake.
Mgogoro wa Kenya na Somali kwenye bahari ya hindi haufanani na huu kabisa. Kenya na Somalia wanabishania mpaka wa majini na kuna tume ya usuluhishi inashughulikia mgogoro huo. Urusi haina mgogoro wowote wa mpaka na ukraine, bali tu haipendi serikali ya ukraine iliyochaguliwa na watu na inataka kuiondoa kabisa serikali ili kusudi iweke ya kwake.
Mkuu "Nyumba ya Nguchiro na mchwa", tofauti hizo ulizo orodhesha hapo nazifahamu barabara, lakini nikukumbushe, kabla ya jeshi la Kenya kuwa chini ya mwamvuli wa AU, walifanya uvamizi nchini Somalia, hata kama nia yao ilikuwa ni kuwashughulikia Shaabab. Mfanano wa uvamizi huo na wa Urusi upo, ila najua hutopenda kuangalia huko.
Mgogoro wa Kenya na Somalia kwenye bahari ya Hindi, hakuna tume yoyote inayoushughulikia kwa sasa. Swala hili limeamriwa mahakamani, lakini Kenya hakubaliani na uamzi huo, kwa hiyo anatishia vita endapo Somalia itafuata uamzi wa mahakama na kutafuta uwekezaji katika maeneo hayo.
Unasema Urusi haina mgogoro wowote wa mpaka, lakini anatumia visingizio, ikiwa ni pamoja na kulinda waasi wa nchi hiyo ili atimize lengo lake kuu la kuzuia NATO kufika mpakani kwake. Kama unalielewa vyema hili, pengine utaona sababu hasa ya uvamizi huo.
Ulaya na Magharibi kwa ujumla hawawezi kujiondoa lamani kutokana na uvamizi huu.
Nguchiro na Mchwa wakiwa ndani ya Kichuguu kama majirani ni lazima waheshimiane. Nguchiro akileta ukorofi na kutaka misaada ya kuhatarisha maisha ya Mchwa ndani ya nyumba yao, hakika ni lazima mchwa nao watafute njia zozote za kujihami wasidhurike, ikiwa ni pamoja na kuwashambulia akina Nguchiro kama wanajitia ujuaji kwa kiburi cha wafadhiri toka nje.