Ndani ya siku 18 za Mama Samia, Taifa limejawa na FURAHA ingawa hajagawa pesa barabarani wala kuongeza mshahara ila maneno tu ya faraja!

Hayo maneno ya Kigogo mkosaji umeya paste huku ndugu yangu.
Sio kila kitu kupinga miaka 6 ilikuwa ya machungu ,hao wapinzani unaoasema wana wanachama ,waliingizwa barabara wakaogopa kufa.
Kinachofurahisha watu ni kuona hata wana CCM hawakuwa na furaha pia.
 
Bora ya mama kuliko Jiwe Mara elfu, Mimi mwenyewe Nina furaha, tumpe mda
 
Mungu amlaze sehemu anayostahili kuwepo huko alipo mavumbini.
 
Ndugu yangu hakuna kinachouma Kama kodi za dhuluma. Wafanya biashara wamepitia maumivu mengi sana
 
I think hivo vitarudishwa Tena bungeni ka hyo Sheria ya mitandao, kanuni za mawasiliano ya kielectronic ni ya kufutwa kabisa hata hyo ya msajil ni ya kufutwa kabisa
 
Kwahiyo mkuu tumshauri mama kesho asubuhi akija aite vyombo vya habari na aseme ataleta katiba mpya???
 
Hawa watu sijui wanataka wafanyiwe nini kwa kweli.

Hili taifa ni la maajabu sana.

Mama yetu kipenzi ameanza kushughulikia matatizo yetu tena katika namna inayoridhisha haswa ila bado tu.

Dah! Poleni viongozi wa Tanzania
 
Yaani baadhi ya wenzetu sijui wana akili gani.

Wao wakiambiwa sheria ndogo tu kwamba wacha kunywa pombe basi hawatoweza kuamka asubuhi na kuacha, itabidi iwe ni mchakato kuacha hiyo pombe.

Ajabu wanataka mama akurupuke na kutafuta kila sheria hawajui kama ni mchakato
 
Je ulitaka azibadikishe kwa usiku mmoja? Utaratibu ni kwamba hizi sheria lazima zipelekwe bungeni na kuzifutulia mbali. Nakubaliana na wewe sheria kandamizi zipo na haziitaji kuwepo kwenye jamii na dunia ya leo?
 
Sasa ana wiki moja unaanza kumlaumu hivi
 
ndio maana umeambiwa mnafiki
 
Ni kweli usemayo ila tusemacho ni kwamba tuna imani na tumepata imani na Mama, alivyomsikivu haya atayafanyia kazi. Mama anatakiwa apewe muda na tusikatishane tamaa kwamba eti ni wale wale tu.

Ndani ya siku 18 mama amefanya tuliyokuwa tunayalilia for ages.

Sisi watanzania tunampenda na tuna imani na Mheshimiwa rais wetu kipenzi chetu, mama yetu Samia Suluhu Hassan
 
Mkuu tunakupa ruhusa wewe usimuamini.

Tuachie Sisi watanzania tumuamini.
 
Yaani saa nyengine ndio maana rais Magufuli alikuwa akiwaambia hawa wabaki na mavi yao nyumbani.

Yaani mnafarijiwa na kupewa tumaini jipya huku mambo yakifanyika mdogo mdogo ila bado tu hawa walimwengu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…