Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Hili swali ni kwenu nyie mamlaka ya usalama wa Ndege zetu, usalama wetu abiria, usalama wa anga letu.
Nisiwachoshe, ukiisikiliza hii video hapa chini, ndege tuliyo nunua bado ni mtihani wa usalama wetu abiria. Wanasema sio salama, ina matatizo mengi sana na inafaa iwe grounded.
Huyu mfanyakazi wa zamani wa Boeing na mpiga filimbi mkubwa anasema kwamba ndege hii ya aina ya max sio salama, ina matatizo makubwa. Serikali njooni huku mtuambie ukweli ni upi kabla hatujachinjwa kama ndugu zetu wa Kule Ethiopia na Indonesia.
Sikilizeni video hii na mutoe majibu ya uhakika kabla hayajatokea ya kutokea maana hawa ngozi nyeupe sisi kwao ni litmus test yao wakati mwingine: Video hii hapa:
View: https://youtu.be/pT4B7oyGBw8?si=3kLm309dbgig8xRO
Usiwe na wasiwasi; kwa sasa hivi ndege hizi ni salama kabisa. Mwezi jana tu, American Airlines imenununa ndege 85 kwa mpigo.
Uongozi wa Boeing ulijifanya kujiendesha kibishara zaidi na kudhoofisha gharama za Engineering ndio uliosababisha ndege hizo zipate jina baya. Baada ya zile ajali za Malaysia na Ethiopia, kulifanyika marekebisho na kuhakikisha engineering na safety standards vinapewa kipaumbele kama zamani. Nadhani viongozi wa Boeing waliokuwa wanakimbilia kufanya mambo kwa pupa wakiangalia faida tu wameshaachia ngazi.
