Ndege ya Rais yaonekana Dubai, Saudi Arabia

tumwombee maza, pengine ameenda kuwaambia wabadilishe vipengele,ama la atawapiga chini awalipe fidia. mambo mema yanakuja bila shaka. kati ya watu wanaosikiliza na kufuatilia mitandao sa100 ni mmojawapo, na hapendi kabisa achafuliwe jina. basi tu kazungukwa na genge la ajabu ila yeye anaweza kuwa na nia njema sana.
 
Hivi kweli ndege kama Air force 1 inawezekana ikaonekana mfano Botswana bila taarifa yoyote kwa nchi ya Marekani? Lakini huku kwetu ni kitu cha kawaida sana. Nakumbuka kuna ndege moja ya serikali fulani ilikwenda kubeba majani ya ng'ombe ya first lady west Kilimanjaro ikazama kwenye matope basi haikuruka tena na haikutangazwa wala mpaka leo haijulikani kama iliuzwa chuma chakavu au bado ipo pale pale lakini ni miaka mingi sana imepita.
 
sasa sisi tunategemea kila kitu kwa wazungu, hatujawahi kurusha hata unyoya tu wa kunguru kwenye satelite, simu na mawasiliano yetu yooote mzungu kayaweka kiganjani. ndio maana wana uhakika hatutakuja kuwatawala.
 
Amekwenda kuhani msiba wa yule mdogo wake rais wa Abu Dhabi aliyefariki Alhamisi
kama anahani, si lazima atakutana nao, awaambie tu kwamba kama hawataki hatuwabembelezi, yeye akiondoka madarakani tutawanyooosha, na pia Mungu wa Ibrahim Isaka na Yakobo ambaye ndiye proved kuwa na Nguvu kuliko mungu wao atatusaidia na kututoa kwenye mikono yao.
 
ila kwenye uchaguzi ujao Watanganyika tuwe makini, tusichague tena mtu mwenye ndugu uarabuni, manake hata wakifiwa tu msibani wanaenda na ndege yetu. baadaye wataanza kwenda hata kwenye kitchenparty za ndugu zao uarabuni.
 
Kinachoshangaza kwanini akae kimya kwenye jambo kubwa kama hili, badala yake wasaidizi wake kila mtu ana jibu lake, tatizo ni nini hasa.
 
ila kwenye uchaguzi ujao Watanganyika tuwe makini, tusichague tena mtu mwenye ndugu uarabuni, manake hata wakifiwa tu msibani wanaenda na ndege yetu. baadaye wataanza kwenda hata kwenye kitchenparty za ndugu zao uarabuni.
Hatukumchagua🙏🙏🙏
 
Kama wangepanda ndege na kuja tz hapo sawa lkn umewafuata kwao hiyo sahau mkuu.
 
Huyu Mama naye sasa amekuwa kiguu na njia, hatulii! Amalize miaka yake hii 2 iliyobaki apumzike!
Alizoea NGO, Nchi ni zaidi ya NGOs!
Mlipenda Rais anayejifungia ndani. Uraia ni pamoja na kusafiri kwendda kuona atafanyaje kulinyanyua taifa, wananchi na mema ya nchi ndio utimamu kwa kiongozi. Tanzania ina watu wa hovyo sana na wanafiki, na wasio na utu hata kidogo

Ndio maana yule Jamaa alikuwa anawatupa tu kwenye viroba!😁😁😁
 

Teknolojia inawaumbua.

Miaka 10, 20 ijayo mijizi na midikteta ya Afrika itakuwa imetoweka kwenye uso wa dunia.

Watu wanajanjaruka, wanaamka, wanaerevuka kila uchwao, lakini viongozi wa Afrika bado wanadhani kila mwananchi wao ni iliterate muuza ndizi kwenye sinia kichwani huku kwenye center za vijiji vyetu masikini ya Mungu.

Abdurahman Kinana, Waziri wa Ulinzi wakati mimi niko primary svhool, kajitoa ufahamu, kawaambia wananchi wa Musoma mtu aliyekula kiapo haibi, hawezi uza nchi. Kwa hiyo katika historia ya dunia mijizi ya kitaifa huwa inatawala bila kuapishwa ?

Wanadhani sisi ni majuha, mazuzu yasiyo na elimu, wwhu wanaoamini kila kitu wanachoambiwa na viongozi. We ARE NOT fools, Mzee Kinana, we ARE NOT!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…