Nitashukuru kama atakuwa ameenda kupiga magoti wabadilishe vipengele vya mkataba. ila inatia huruma sana kwamba Rais wa nchi ahangaike hivyo kwa mwekezaji, badala ya mwekezaji yeye aje hapa baada ya kuona malalamiko, rais wa nchi ndio anaenda.
Si mnaona tulichokuwa tunasema utumwa ndio huu sana, tumeanza kuhangaika kwenye mali zetu sisi wenyewe. mwarabu kakaa kimyaa anasubiri sisi twende tukapige goti na akiwekez ahapa tutamlinda na kumwabudu. natamani iwe kweli, aende kwa waarabu akaongee nao upya, wabadilishe vipengele vya mkataba, wawekeze mambo yaendelee.