Ndoa ina mwezi mmoja, nishaanza kukosa amani

Dini inaruhusu kuoa wapili?
Mathayo 19:4-6,10
[4]Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,

[5]akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?

[6]Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.

[7]Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha?

[8]Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi.


[10]Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa.

Ukimuacha ama ukaoa mwingine huyu uliemuoa unazini nae
Haya kama kanisa likikufungisha ndoa nyingine na suti nzur ukavaa
maandiko yanasema ww unazini nae maisha yako yote mbele za Mungu
Ndio maana maandiko yanasema hakikisha unaemuoa ni mungu amekupatia.
Sio tamaa zako.

Ww hutaweza kumuacha isipokuwa wakati unamuoa hukumkuta na bikira na yeye hakukuambia tangu mwanzo kuwa alishafanya uasherati kabla ya kuwa na ww na akakuomba msamaha kwa hilo

Mwanamke ndie anaevunja ndoa
Maandiko yanasema sio mwanaume ni mwanamke anaeivunja kwa ujinga wake.
 
Hiki kitu niliwahi kuwashauri wadau humu ndani ila wakaniona mi muhuni, mara ooh binti atakujaje kukaa kwako ikiwa ana wazazi wake 😅 ila kwa wenye jicho la tatu walielewa vyema ile concept. Inasaidia sana hasa zama hizi ambazo watoto wakike hawana malezi.
 
Utajuaje kama Mungu ndie amekupatia maana wote uomba Mungu awape wenza lakini shetani huwahi kujibu maombi
Wengi ni malaika uchumbani wakiingia kwenye ndoa ugeuka chui.
 
Shida iliyopo sasa wanawake wanatafsiri kupendwa na mwanaume ni kama ataonyesha kuvumilia tabia za kipuuzi na hapo hapo ulizivumilia anakutoa thamani tena kuwa umeshindwa kuwa mwanaume imara na kumsimamia.

Mimi ndio maana siruhusu mizaha na mwanamke hata siku moja. Utani tunataniana sana na huwa nafanya nae comedy zile za couple hadi anajua hapa yupo na best friend wake ila anajua the moment akianza leta mizaha na makusudi mimi namchenjia na sina haya nae usoni.
 
yaelekea umeoa mwanamke ambaye hukumfahamu hapo awali. Hilo ni kosa ulilofanya. Sasa pima, kama mema ya msingi yake ni mengi basi vumilia, yakubali hayo mapungufu & ishi nae.
Hawa ndio wale siku ya ndoa unashangaa mwanaume anafuraha kuliko mwanamke mara akate viuno mbele ya hadhira bila hata soni, mara atoe risala ndefu akimsifia mwanamke wake utadhani alimpata kwa jackpot, mara apige goti kumvisha pete, mara alie tena. Yaani upuuzi mtupu.
 
Mbona hayo yote ni kawaida subiri phase two ndo utajue wanawake ni nini, rafiki yangu hu ni mwezi wa pili analala kwenye gari lake ila ndoa yake in miaka 4, hapo kwako hiyo inaitwa cooling break mechi bado kabisa.......
Sasa kuna faida gani ya kuoa au kuolewa. Mtakufa kabla ya siku zenu. Ndoa sio kuvumiliana ujinga.
 
Ukiwa ndani ya Yesu utajawa Raha Sana in every aspect UTA experience rahaa
 
Tukisema msioe mnatuita mashoga, sasa pambana na hali yako.
Dunia ya sasa kwenye wanawake 20 unaweza kupata wawili au mmoja tu mwenye sifa ya kuwa mke.
Kwa sasa hata mmoja hakuna , amini usiamini huu ndiyo ukweli.
 
Hypergamy.
Hilo ni jaribio, women will always try to test men to see if they are strong enough.
Suluhisho sio kuoa mwingine, weka boundaries, zikivunjwa, you know what to do.
Ila usitafute mke wa pili, jua jinsi ya kudeal naye.
 
Utajuaje kama Mungu ndie amekupatia maana wote uomba Mungu awape wenza lakini shetani huwahi kujibu maombi
Wengi ni malaika uchumbani
Umewah kuwa kwenye shida ukamuomba Mungu ikapoteapotea.
Ama ukaomba kisha watu ata watatu wakaota ndoto moja inayofanana kila kitu kuhusu ww na hata hukuwaambia kitu kuhusu.
Ama umewahi kuomba kuwa na uhitaj na ukapata

Mungu hujihusisha sana na mamb matatu kwa mwanadamu
Kuhakikisha anapata wokovu.
Anapata mweza sahihi katika safari ya duniani.
Na kumpatia uzima wa milele.
Ayo mengine ni nyongeza.
Kuzaliwa kuoa/kuolewa na kufa.

Mungu hakupi usipomuomba.
Alimpa adam mke pasipo kuombwa akaishia kulalamikiwa kuwa ni huyu mwanamke ulienipa

Tangu siku hio Mungu hampi mtu mwenza isipokuwa uyo mtu amemhitaji na aakamuomba.

Kuhusu njia anazozijibu kasome visa mbali mbali vya watu waliotaka mke wakamshirikisha Mungu
Wakwanza akiwa ni isaka.

Ila kwakuwa umekishwa kosea.
Ww chakufanya ni kimoja

KUDUMU MWAMINIFU.
ENDELEA KUMPENDA TUU.
MUOMBEE SANA.
MUONYESHE UPENDO ZAIDI YA WA MWANZO BILA KUJALI,

Maana ibilisi alishakupata kupitia mke.
Kumbuka adam hakudanganywa na nyoka miaka yote mpaka pale mwanamke alipotumiwa na shetani.
Na ni hvyo kila wakati.

Huyo ni ibilisi kabisa amemvagaa mkeo.
Wala mkeo yeye hana shida.
 
KATAA NDOA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…