Hivi unafahamu kwamba hao wafalme na manabii wa Mungu mfano Suleman na baba yake Daudi waliua watu wengi sana katika utawala wao, Mungu aliwaruhusu hilo na ndio kwanza akazidi kuwapenda na kuwabariki, kwahiyo mnataka kusema kwamba kuua siyo dhambi tena sababu hao walifanya na Mungu akazidi kuwabariki
Hivi unajua kuwa Suleman alipooa wake wengi akafikia hatua akamchukiza Mungu hadi Mungu akaamua kumpa adhabu ya kuugawanya ufalme wake na kumpa kijakazi wake
Na mwisho wa siku baada ya kufanya hayo yote akaandika kitabu cha Mithali, ambacho baadhi ya maandiko humo ni majuto kutoka kwake akielezea kwamba alikuja kugundua kuwa yale yote yalikuwa ni ubatili mtupu na kujilisha upepo, na Mungu alimruhusu na kumpa kila kitu kwa makusudi ili aje ajionee kwamba unaweza kuwa na kila kitu unachokitaka hapa duniani na bado ukakosa hiyo raha na amani unayodhani utaipata