Mkuu
igwee frm anambra nataka nikuulize!
Unadhani kwanini watu huamua kuingia kwenye ndoa?maana kama ni starehe za kwenye ndoa wanaweza kuzipata nje ya ndoa lakini kwanini waishie kwenye viapo?huoni kama kuna la ziada hapo?
Personally,simu yangu na ya mke wangu password tumeweka zinazofanana muda wowote nikitaka kushika simu yake au akitaka kushika simu yangu hakuna simile nashika/anashika nimempa hadi uhuru kama simu ikapigwa nipo mbali pokea elekeza anitafute kwa namba nyengine au ajibu atakavyoona inafaa.ukishaamua kuowa amua kweli kuowa unapotaka mkeo awe muwazi kwako na wewe vaa uhusika kuwa muwazi kwake hii theory imenisaidia sana kwenye maisha yangu ya ndoa.
Na huu ndo umekuwa mtego mbaya kwa ndoa za kisasa,mume kuanzia dialing,msg,w'app kajaza passwords tofauti tofauti mke nae hayupo nyuma naye kafanya hivyo hivyo simu ikiita mnatizamana kwanza unadhani kutakuwa na ndoa hapo!hayo ni maigizo.