Ndoa zimekuwaje? Kuna Video inatrend leo Mume akimkaba mkewe na kutaka kumuua live barabarani

Ndoa zimekuwaje? Kuna Video inatrend leo Mume akimkaba mkewe na kutaka kumuua live barabarani

Sasa kuachana hivi hivi ikiwa Mwanaume amekugaramia vitu vingi vya thamani hawezi kukubali umcheke ujinga,

Somo hapa ni wanawake waache tamaa na kujiona wajanja kupenda kuhongwa na kutaka mali za wanaume Halafu hamtaki kuwa watumwa wa hao wanaume.

Hutaki kutawaliwa na Mwanaume usile Hela żake wala mało zake ,

Tafuta kazi jipatie kipato chako uwe huru.

Mwanamke uingie kwenye uhusiano wa penzi sio sababu ya njaa bali usukumwe na penzi kisiło na masharti kama kutaka fedha.
Ok.
 
Wanaume kama hawa ni huwa ni fisi kukabiliana na mwanaume mwenzake
Yaani jitu zima linamkalia mke wake, aibu nimeona mimi
 
dada yangu akitendewa uo uhayawani lazima nishikiliwe na watu wa maximum security nafungwa pingu miguuni, mikononi na mdomoni nawekewa lile kufuli la kuzuia nisiwang'ate yan yaan familia ya marehemu shemeji yangu haitonisahau kamwe
Ndoa Ina utaratibu wake siyo Dada yako amfanyie upumbavu mmewe Alfu ww uingilie kwa kutetea upumbavu wa Dada yako. Huo unakua siyo Ustarabu na Wala siyo kusolve tatzo Bali ni kuchochea ugomvi na kusababisha matatzo zaid.
 
Kibongo bongo mtu anaweza kupiga hata zikafika miss call milioni moja🤣. Trust me, sisi wabongo, ni wachache ambao akipiga simu moja usipopokea ataacha. Back kwa hao wanandoa: inaonyesha ndoa yao ina kutoaminiana, yaani mume anahisi mkewe anachepuka. Na ndoa ikishafika kwenye stage hii vi-ugomvi vidogo vidogo haviishi.
Dah! Missed call 2, inafuata sms… incase mtu yuko sehemu ambayo hawezi pokea simu asome ujumbe kama anaweza kurespond.

Yaani nipige simu zote hizo kuthibitisha mtu kama anakula mtu mahali au nimzuie asile mtu? Kwani mtu si anaweza pokea simu na akaendelea kukatika??

🙄
 
Missed calls zikishazidi 2 ni kujitafutia presha, napiga mara 2 then natulia.
 
Back
Top Bottom