Ndoa zinakufa kila kukicha siku hizi


Mbona hujaeleweka,watakatifu wako mbinguni,ndoa ni unyonyaji.
 
Miaka nane imetosha kabisa.... Acha tu kila mtu apambane kivyake
Huyo anasema miaka kumi, kuna watu nawafahamu kama wa 3 ndoa zao zimevunjika uzeeni. Mmoja ndoa ina miaka 35, wengine wazee kabisa.
Hii taasisi ya ndoa sijui ilekuwaje. Mimi nilibwaga manyanga baada ya miaka 5, nikaone nisije kufa kwa ajili ya mtoto wa mama mkwe. Majirani zangu wa nne, wa 2 wanaishi nyumba tofauti, mmoja mume kakimbia sijui yuko wapi, mwingine wanalala vyumba tofauti. Majanga kweli. Huko kwa wazungu ndio usiseme, wao divorce wala si tatizo, tena wanaachana kwa wema tu hata kama watoto ni wadogo, wananabaki kulea pamoja . Hii inaepusha kuchomana na magunia ya mkaa.
 
Kuzaa hata mahawara wanaozaa. Ndoa ilianzishwa kwa lengo la kuepusha uzinifu yaani ngono ifanyike kwa walengwa tu.

Lkn kwa dunia ya Leo ngono ni kwa kila mmoja na kwa yeyote. Kwa mantiki hiyo basi ndoa zimepoteza mwelekeo.
Ni kweli, ndio maana kuvunja ndoa sababu ya kutozaa haiwezekani.
 
Naona umeongeza Single maza / lishangazi mwingine mjini ...acha raia wapite nae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…