Ndoto hii ina maana gani? Je, ni walking dead?

Ndoto hii ina maana gani? Je, ni walking dead?

N:B Sina mazoea kabisa ya kwenda kwa waganga,

Ndoto inaanza tupo mimi na mganga juu ya bonde, chini kuna mto ambao maji yake.

Hata sijui ni kipi nlifata kwa huyo mganga ila akawa kamazliza shughuli yake, aliniambia nivue begi langu ambalo lilikuwa na laptop ndani yake akalitupa mtoni, Laptop nliifungasha ndani ya kitu kama rambo ikiwa ndani ya begi kwa hio maji yasingeingia sana.

Laptop yangu ilikuwa na mambo mengi sana muhimu ya kunihusi mimi ambayo siwezi kuyapata kwengine, mfano picha nlizotunza, nyaraka binafsi, password zangu za sehemu mbali mbali, mauzo, n.k

Mganga aliniambia kafanya hivyo ili kukamilisha shughuli.

Ilibidi nianza kutafuta watu wa maeneo hayo mitaani wanisaidie kutafuta hilo begi lakini watu hao wakaniambia hio ndio tabia ya waganga na huwezi kutoa kilichotupwa na waganga mtoni unaweza kupata pigo kubwa.

Sasa sijajua ina maana gani ila kwa mbali nachojua tu ni kwamba wiki hii zipu ya begi langu la laptop kuna muda inaachia japo ni mara 2 tu hili tukio limetokea.
 
Wadau yaani hii imenitokea mara tatu naota hii ndoto nacheza draft na moo na bakresa sasa sijui ata ina maana gani wataalam wa ndoto please naomba msaada au nataka kupata mihela ya uzeeni hahahaha
 
Wadau yaani hii imenitokea mara tatu naota hii ndoto nacheza draft na moo na bakresa sasa sijui ata ina maana gani wataalam wa ndoto please naomba msaada au nataka kupata mihela ya uzeeni hahahaha
Utakuwa tajiri mkubwa
 
Wadau yaani hii imenitokea mara tatu naota hii ndoto nacheza draft na moo na bakresa sasa sijui ata ina maana gani wataalam wa ndoto please naomba msaada au nataka kupata mihela ya uzeeni hahahaha
Moo na bakresa ndio wakina nani hao?
 
Kama unakula ugali uliosongwa kwa kutumia unga wa Azam na kunywa Mo cola kabla ya kulala...basi acha mara moja, ndoto zikizidi unaweza kumuona daktari
 
Wadau yaani hii imenitokea mara tatu naota hii ndoto nacheza draft na moo na bakresa sasa sijui ata ina maana gani wataalam wa ndoto please naomba msaada au nataka kupata mihela ya uzeeni hahahaha
Mods peleka hii Jukwaa la Jokes!
 
Mtanisamehe wakuu endapo baadhi yenu nitawakwaza ila sina namna itabidi tu niongee kinacho nitatiza pengine wenye ujuzi wataniambia huwa kuna maana gani.

Ni hivi kipindi cha utawala wa hayati Magufuli. Nianze mwanzoni kabisa kabla hajagombea kuna ndoto nilikuwa nikiota nikiwa nae pamoja yeye na Lowasa tukiwa tumepanda gari aina ya ndoki kwa msiozijua ndoki ni gari fulani hivi wanazipenda sana wamisionali kwa jina jingine difenda.

Basi tukawa tumekaa nyuma mimi na Mheshimiwa Lowassa pamoja na hayati Magufuli tukawa tunapiga story kuhusu uchaguzi ule wa 2015.

Nikawa namwambia Lowassa bwana mkubwa huwezi toboa japo kuwa una ushawishi basi tukawa tunachekavwote kwa pamoja kumbukeni ni ndoto hiyi ningeileta mapema sema sikuwa mzoefu wa hii JF.

Tukiliacha hili tuje kwenye lengo kuu katika utawala wa hayati Magufuli ilikuwa kitu kama2017 nikaja nikaota ndoto tena ambapo siku ielewa maana yake ila nikapoteza ikaja 2019 nikaota tena vile vile kama ya 2017 tumekaa sehem na hayati Magufuli alafu ghafla kanipotea nikalia sana ndoton maelezo ni mengi ila nimefupiasha.

Halafu ikapita kama wiki katika huo mwaka nikio ota nikakuta watu wanatoroka na kuzusha Mheshimiwa rip ila haikuwa hivyo mpaka 2021.

Sasa kinachokuja kunishangaza wiki iliyopita zile ndoto zimeanza kujiRudia tena nimeota nimekaa na Mheshimiwa Samia halafu kwenye hiyo ndoto tunagombana sana kiasi kwamba mpaka nashindwa kuelewa lakini mwisho wa siku najikuta humo humo ndani ya ndoto nakuwa na huzuni sana halafu jana nikiwa kitaa jamaa karopoka vilevile Mheshimiwa R.I.P sasa na shinda kuelewa tafsiri ya haya mambo.

Wakuu samahani nimeshindwa kujizuia kusema.
 
Shukuru mzee wa galilaya hayupo lazima ungeitwa kuhojiwa, na hata jela🏃.
 
Back
Top Bottom