Ndoto hii ina maana gani? Je, ni walking dead?

Ndoto hii ina maana gani? Je, ni walking dead?

Natumai mu wazima sipendi kupoteza muda hii mada sijui ni swali au maelezo tujionee wenyewe

Mimi bwana ni mkristo ninae mjua tu vizuri yesu tena japo kabla ya kumaliza kidato cha nne ilipokua unantajia neno MUNGU ni kama ninavyochukulia majina mengine ya watu enzi hizo

ila baada ya hapo nilisikia ushuhuda mmoja nikaona wacha na mimi niwe muumini mzuri kila siku naomba vizuri tu na dhambi niliacha zote

sasa baada ya muda nilihitaji huyu MUNGU ninaye muabudu hasa YESU ajidhihirishe kwangu kwa namna yeyote ili niwe na hakika na nilichokua nafanya niliomba ila wapi nikawaza nikaona hizi imani nikama kunyimana uhuru

Nalijua neno vuzuri sana nikarudia maisha yangu ya kawaida ila ilikua kila ninavyofanya dhambi moyo kama unauma na kama sauti juu inakazia

nakumbuka jana kuna mtu kaniuzi kweli ila mara nasikia moyoni samehe nilijawa na hasira sana mpaka kupiga teke ardhi kwa hasira ya kuisikia sauti kuniambia nisamehe kisha nikaijubu Kusamehe ndo nini?

hua japo naipuza hii imani ila hua siachi kuomba hasa nikiwa nalala au nakula na nikiwa barabarani

ila kila nikikaka najisemea Mbona sasa huyu Mungu mwenyewe hajidhihirishi kwangu naweza nikawa nimepigwa hapa kuabudu vitu visivyo kuwepo

Ila mpaka naandika hapa roho inanishuhudia kuwa YESU yupo na pia kuwa niombe napuuza maana nimeomba sana

mchana niliota ndoto mbili fupi moja ni kuwa nimepita pembeni ya kanisa la kilokole Kwa hasira nilishika gari na kulilushia kanisani ila mara Nikajua kuwa haliwezi kufika kanisani kwa kua YESU yupo sijui najuaje ila najikuta nimejua na kweli lile gari halikufika

yapili et nimeisahau ila nayo inahusu YESU kwamba yupo nikikumbuka nitakuja kuiweka

Bado nipo njia panda ila nahisi kunavitu vingi hua vinatokea nyuma ya hivi tunavyoviona ila kunauwezekano MUNGU yupo na anafanya kazi.
 
Kumekucha, wagonnjwa poleni sana na wazima mshukuruni Maulana.......,

Ndugu yenu usiku wa Leo nimeota ndoto ambayo tofauti na ndoto zote ninazoota ambazo huwa sizikumbuki/nazisahau ila nakuwa najua kuwa nimetoa hii niliyoota Jana naikumbuka vema sana.wataalamu waliobobea katika ndoto na wenye uzoefu kwenye ulimwengu wa ndoto nawaomba mnisikilize kwa makini kijana wenu na mnitafisrie ndoto yangu kwa usahihi vinginevyo mtakuwa na mchango mkubwa kwa lolote litakalonipata nitasimulia katika mtindo wa point point sitaweka longolongo nyingi ili nisiwachoshe.

Basi usiku wa Jana nikalala sikumbuki muda saa ngapi, nikaanza kuota nabwekewa na mbwa wawili mmoja mkubwa mwingine mdogo,walibweka Sana wakitishia kuniuma nami nikawa napambana kuwatishatisha wakawa wananizunguka zunguka kutaka kuniuma, katika purukushani nikaokota pande la kijiti na kuanza kujihami.

Nikajihami muda mrefu kidogo huku nawakosakosa na wao wananikosakosa ila nikafanikiwa kumpiga mkubwa na nilipompiga tu akageuka siafu.alipogeuka sikujua kijiti kiligeuka kuwa Nini ila kilibadilika kuwa Kama mfano wa nyundo nikambonda huyo siafu na kumpasua kichwa, haukupita muda na mbwa mdogo akageuka siafu pia na yeye akala bonge la yok kichwani nikawa nimewamaliza.

Lakini baada ya kuwamaliza nikasikia kelele za watu wawili wanakuja kwa kusema nimeua mbwa wao nikaanza kukimbia na wao wakaanza kunifukuza walikuwa na mbwa wengine wawili wakubwa Zaid..nikakimbiiia na kuwaacha kwa mbali kidogo nikachoka nikapata wazo la kupanda mti nikachagua mti mmoja mkubwa Sana ulio vichakani nikaupanda ila matawi yakawa yanayumba kiasi Cha kutaka kuniangusha.

Haukupita muda waliokuwa wananifukuza wakapita kwa mbali kidogo na nilipojificha wakawa wanaulizana nimeenda wapi halafu wakaamua kuendelea mbele kunitafuta huku Mimi nawaona lakini mbwa wao mmoja akanusa sijui harufu yangu akaja mpaka nilipojificha chini ya mti akanitazama tu Kisha akakimbilia walipokimbilia wale watu, alipoondoka wakajitokeza watoto watatu wawili wa kike mmoja wa kiume wakaniona nikawaashiria ishara ya kunyamaza kwa kidole na mtoto mmoja wa kiume akaniambia kwa ishala ya lugha ya alama wanazotumia wasiosikia neno (DUMU)....baada ya hapo nikashuka nakumbuka nilimpa jibu (HOME) halafu tukaanza kutimua mbio kushuka kimlima hivi chenye vichakani na mawe kwa speed Kali Sana tukielekea nyumbani ambapo katika ndoto yangu palionekana ni kijijini kwetu nilipozaliwa.wakati tunakimbia kumbe na wale watu na mbwa wao waligundua tukasikia kwa mbali na wao wanakuja kwa kukimbia.

Tukakimbia na wao wakatukaribia Sana nikamwambia dogo wewe kimbilia kwetu (maana tulikuwa tunaishi familia mbili yetu na ya baba mdogo nyumba zimepakana) Mimi nitakimbilia kwa baba mdogo. ukifika tu chukua mwaga sikumbuki vema ni Nini chini chora mchoro wa jua weka macho mawili Kisha funika na dishi dogo la plastik Kisha jifiche uvunguni na Mimi nikafyatukia home kwa bamdogo nilipofika nikafanya vile na nikafunika, punde wale watu waliokuwa wanatufukuza wakafika wakaingia chumbani ila wakawa hawanioni wakaanza kushangaa dishi chini mmoja akafulifunua wakakuta mshumaa mdogo unawaka akamua kuukanyaga akaungua mguu na Cha ajabu mshumaa wenyewe ukawa hata hauzimiki halafu nikaja kuzinduka na ndoto ikawa imeishia hapo.

Nimebaki na maswali mengi Sana kuhusu hii ndoto maana NI kawaida Mimi kuota vitu Leo halafu baada ya muda nakuja kuvishuhudia kwa macho na Kukumbuka kuwa nimewahi kuota, mfano naweza kuoka Niko sehemu Fulani halafu baadae nikaja kufika kweli hiyo sehemu.

nakumbuka nimewahi kuota madharani iwe ofisi Fulani, mkoa Fulani, eneo Fulani watu funalan na nikafika kweli n.k.

funga kazi ni siku nimeota nakutana na mkuu wa nchi katika mazingira Fulani ikapita miaka Kama 7 hivi nikaja kukutana na shujaa wetu akiyeondoka na yeye akauchangamkia mkono wangu.

Wataalamu wa ndoto nawaomba hapa kwa msaada tafadhari.

Samahani kwa uandishi Kama wa darasa la pili.
 
‘Ninamsifu Yehova, Mfalme wa mbinguni. Sasa ninajua kwamba Yehova ndiye Mtawala. Anawanyenyekeza wenye kiburi, na humpa yeyote yule amtakaye ufalme huo.’
 
‘Ninamsifu Yehova, Mfalme wa mbinguni. Sasa ninajua kwamba Yehova ndiye Mtawala. Anawanyenyekeza wenye kiburi, na humpa yeyote yule amtakaye ufalme huo.’
Huu ndio uhalisia wa ndoto yangu?
 
Ndoto yako ni ngumu
Ila uwepo vitu kama rungu, nyundo na mti mkubwa ni ishara ya utawala au mamlaka
.Ndoto Inategemea nani anaota ndoto moja inaweza kuwa na maana tafauti kutegemea na mtu aliota.
Km wewe ni mtu una mamlaka ya kufanya maamuzi jiandae na mabadiliko utakapo hisi umewashinda adui zako watakuja tena na nguvu kubwa kwa ghafla
 
Ndoto yeyeto yenye ujumbe, ishara ni lazima utaikumbuka tu ukiamka. Hata ndani ya siku tatu.
Ukiona uuhikumbuki ndoto uliyoiota achana nayo hio ni ndoto ya kawaida tu. Maana ndoto zipo za aina tatu tu.
 
Tafsiri ya ndoto hio ni kwamba ulikuwa unafatiliwa na wachawi Ili wadhuru maisha yako lakini ukapambana nao na ukawashinda ndo maana ya kuwauwa mbwa baada ya kuwashinda wakaenda kuongeza nguvu hao mbwa wengine still ukawashinda so Ina maana una nguvu kubwa kuliko hao wapumbavu ndo maana ukawashinda.
 
Habari za jumamosi wakuu! Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, mimi nimekuwa mhanga wa tatizo hili na limekuwa la muda mrefu sana toka 2015 mpaka hivi leo nimekuwa nikikutana na tatizo hili na mara ya mwisho kunitokea ni kama week mbili zilizopita hapo nyuma.

Wengi husema ukilala chali ndio hutokea hivyo lakini kwangu sasa imekuwa sivyo tena bali hata nikilala kawaida kwa style yoyote ile, jambo hilo linaweza kunitokea. Nakumbuka kuna kipindi fulani hii hali ilizidi kwa siku ilinitokea kama mara 4 yaani usiku, asubuhi mapema majira ya sa12 ikanitokea na mchana pia nilivyolala ikanitokea, na usiku wa hiyo hiyo siku kwa kuwa nyumbani walifahamu hiyo siku tatizo lililonikuta basi usiku tulisali sana na nikabadilishiwa chumba cha kulala lakini usiku hali iliendelea vilevile.

Siku iliyofuata tulienda kwa mchungaji kwaajili ya kufanyiwa maombi lakini baada ya kufika kwa mchungaji kuna maneno alikuwa akiniambia na akiongea ambayo baadaye yalinifanya nijiulize sana maswali. Na pia kabla ya nyumbani kuchukua maamuzi ya kunipeleka kwa mchungaji, mama yangu alisema aliwahi kwenda kwa mchungaji huyo huyo kufanya maombi yake ya kawaida kama siku zote na alisema kuna siku mchungaji yule aliwahi kumwambia kuwa "una mtoto wako ambaye husumbuliwa na ndoto za ajabu wakati wa usiku...."

Hayo maombi nilifanyiwa zamani ni miaka sasa imepita ila hali hii hujirudia mara chache sana sasa nashindwa kuelewa labda huwa ina maana gani? Kwa kuwa humu JF kuna watu wengi wenye uelewa wa mambo mengi tofauti tofauti basi na uhakika naweza elewa kitu.

Asanteni! Mkawe na Sabato Njema!
 
Ni ndoto tuu kwa Kiingerza inaitwa Nightmare induced by REM's

Ni ndoto kwa Kiingerza inaitwa Nightmare induced by acute REM's muone bingwa wa magonjwa ya usingizi Muhimbili kwa msaada
Haina uhusiano na dhana ya kufikiri a ya mashetani na majini
 
Kama upo Dsm nenda kwa Mwamposa utakuwa sawa na kama Rc nenda kaaabudu pale St Joseph mlango upo wazi
 
punguza mawazo mkuu mawazo hayatakufikisha hata hapo morogoro nje ya hapo utaota sana
 
Back
Top Bottom