Habarii, naomba mwenye uelewa wa kutafsiri ndoto anisaidie tafadhali,
nimewahi kuskia kwamba ndoto zinazohusu nywele inatakiwa uwe makini nazo, maana nywele kiroho zinamaana kubwa.
Hivyo naomba mwenye uelewa na ndoto hii anieleweshe:
Nimeota naelekea kanisani lakini ,kabla sijaingia church nikapita maliwato , nilikuwa na wenzangu, lakini nikakuta watu wengi huko , wa kanisani, badala ya kufanya shughuli iliyowapeleka wao wakawa wananishangaa namna nywele zangu zilivyo nzuri na zilivyo ndefu. Yaan Kila mtu akawa anazisifia.
Katika ndoto pia nikarudi nyumbani but kabla ya kuingia ndani, wakatokea jirani zangu wawili wakawa wananishangaa pia nywele zangu zilivyorefuka, mmoja anazisifia na mmoja akawa anaziangalia kwa jicho la husda bila kuzisifia.
But Mimi katika ndoto sikuwa nawasiwasi nikawa naona ufahari ,namwambia hiyo jirani yangu alozisifia kwamba unaona mchicha unazidi kurefuka.
Nimeamka nimekosa amani moyoni mwangu, please naomba msaada wa uelewa katika Hilo tafadhali.