Ndoto hii ina maana gani? Je, ni walking dead?

Ndoto hii ina maana gani? Je, ni walking dead?

Habari za jumamosi wakuu! Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, mimi nimekuwa mhanga wa tatizo hili na limekuwa la muda mrefu sana toka 2015 mpaka hivi leo nimekuwa nikikutana na tatizo hili na mara ya mwisho kunitokea ni kama week mbili zilizopita hapo nyuma.

Wengi husema ukilala chali ndio hutokea hivyo lakini kwangu sasa imekuwa sivyo tena bali hata nikilala kawaida kwa style yoyote ile, jambo hilo linaweza kunitokea. Nakumbuka kuna kipindi fulani hii hali ilizidi kwa siku ilinitokea kama mara 4 yaani usiku, asubuhi mapema majira ya sa12 ikanitokea na mchana pia nilivyolala ikanitokea, na usiku wa hiyo hiyo siku kwa kuwa nyumbani walifahamu hiyo siku tatizo lililonikuta basi usiku tulisali sana na nikabadilishiwa chumba cha kulala lakini usiku hali iliendelea vilevile.

Siku iliyofuata tulienda kwa mchungaji kwaajili ya kufanyiwa maombi lakini baada ya kufika kwa mchungaji kuna maneno alikuwa akiniambia na akiongea ambayo baadaye yalinifanya nijiulize sana maswali. Na pia kabla ya nyumbani kuchukua maamuzi ya kunipeleka kwa mchungaji, mama yangu alisema aliwahi kwenda kwa mchungaji huyo huyo kufanya maombi yake ya kawaida kama siku zote na alisema kuna siku mchungaji yule aliwahi kumwambia kuwa "una mtoto wako ambaye husumbuliwa na ndoto za ajabu wakati wa usiku...."

Hayo maombi nilifanyiwa zamani ni miaka sasa imepita ila hali hii hujirudia mara chache sana sasa nashindwa kuelewa labda huwa ina maana gani? Kwa kuwa humu JF kuna watu wengi wenye uelewa wa mambo mengi tofauti tofauti basi na uhakika naweza elewa kitu.

Asanteni! Mkawe na Sabato Njema!
Anza tu kugawa Urithi Safari inakaribia!!
 
Tatizo watu mnapuuzia mnayoambiwa na watu wa Mungu, na wengine wanayadharau kabisa na kuona ni vitu vya kufikirika tu. Je, hujawahi kuambiwa na mtu wa Mungu kufanya jambo lolote? Ulifanya? Na kwa kiwango gani?

Inaonekana unasemeshwa, na ndio maana unasema unaongea vitu visivyoeleweka. Samuel wakati anapata unabii, alisemeshwa akiwa amelala, lakini jambo hili lilikuwa jema na ulikuwa ujumbe kutoka kwa Mungu. Kwako wewe, ujumbe unaopewa hauna nia njema na wala hautoki kwenye nuru, bali kwenye giza. Kwa bahati nzuri, bado kuna nguvu (yawezekana wewe mwenyewe, wazazi, au mababu; maana nguvu huwa haipotei: conservation of energy), ndio inayokusaidia.

Nini cha kufanya? Tekeleza uliyoambiwa na watu wa Mungu, wala usipuuzie. Utawajuwa watu wa kweli wa Mungu, na wale wasio wa kweli, fuata maagizo ya wale wa kweli. Kwa mfumo aliotuwekea Mungu hapa ulimwenguni, hakuna tatizo lisilo na suluhisho, na ndio maana kila mtu alipewa kipawa tofauti na mwingine, ili kila mmoja awe na msaada kwa mtu mwingine.
 
Muwe mnasali jamaniii kabla na baada ya kulala
 
Nashukuru sana kwa huu ushauri [emoji1431] ubarikiwe !
 
KUNA MAMBO UNATAKIWA KUJUA KWENYE HILI.
1. Mungu anasema watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa. (Hosea 4:6). (Yaani kuomba watu tunaomba lakini maarifa ya kuombea au kutatua tatizo kwa namna sahihi hatuyatafuti) Ninayaongea haya kwa sababu katika kuhudumia watu mbalimbali nimekutana na watu wengi ambao watakwambia kitu kilekile ambacho Mungu ameniambia mimi lakini walioneshwa tatizo halafu hawatafuti ni namna gani Mungu ameweka njia ya kutokea kwenye hilo tatizo

2. Nimekutwa na tatizo hilo kwa muda kidogo. Niliomba sana lakini halikuisha hilo tatizo kwa maombi niliyokuwa nikiomba.

3. Nikaanza kufuatilia hili jambo lipo vipi. Kwanza hiyo si ndoto bali ni tukio halisi linalokuwa linatokea muda huo. Mimi nilianza kuwa makini kufuatilia ndipo nikaona kuwa anapokuja mtu huyo huwa macho yanaanza kuwa mazito na ninaanza kuishiwa nguvu hata nikianza kuomba siwezi halafu ghafla utaona mtu anakuja na kufanya anachofanya. Kweli nikawa napata hasira sana lakini nikanza kuamuru wale watu warudi ili niwaone vizuri ni nani? Kweli walikuwa wanarudi.

NIKAMUULIZA MUNGU HII KWA NINI INAKUWA HIVI. AKANIJIBU MAJIBU YAFUATAYO.
1. Sina nguvu za kiroho. Nguvu za kiroho zinakuwa zinajiactivate automatical inapotokea shida yoyote na unaweza kushinda katika ulimwengu wa roho na kushinda. Soma Waamuzi 16:20, Halafu soma mistari ya nyuma yake ujue chanzo cha kuishiwa nguvu(Yaani kumuasi Mungu na agano lake) Nikaomba maombi ya Samsoni kwenye Wafalme 16:28.

2. Akaniuliza swali hili je unayo damu ya Yesu Kristo? Unaifanyia nini?

3. Akanifundisha kuhusu malaika walinzi alionipa na namna ya kuwatumia. Kweli watu tunaangamizwa kwa kukosa maarifa. Aliniambia malaika hawajui lugha yako ya kusema malaika fulani naomba bali wanaijua lugha ya amri ambayo ndiyo wanatakiwa kutii. Mfano Unasema kwa jina la Yesu Kristo enyi malaika walinzi ninawaamuru kukaa katika nafasi yenu na kunilinda. (Hapa nakwambia nilichokiona mwenyewe nilikuwa najificha maana kulikuwa na risasi zikitembezwa mpaka niliogopa) Nikashangaa sana na kumtukuza Mungu. Mungu ametupa vitu vikubwa sana lakini hatujui kuvitumia.

Tatizo limeisha na wala sioni tena hizo habari. Wale watu wananiogopa sasa maana siku ya pili niliona kwa jinsi ya mwili nilipokutana na mmoja wa wale watu.

NB: Tafuta maarifa sahihi kutoka kwa Mungu ya jambo linaliokukuta. Yohana 16:13
 
Tatizo watu mnapuuzia mnayoambiwa na watu wa Mungu, na wengine wanayadharau kabisa na kuona ni vitu vya kufikirika tu. Je, hujawahi kuambiwa na mtu wa Mungu kufanya jambo lolote? Ulifanya? Na kwa kiwango gani?

Inaonekana unasemeshwa, na ndio maana unasema unaongea vitu visivyoeleweka. Samuel wakati anapata unabii, alisemeshwa akiwa amelala, lakini jambo hili lilikuwa jema na ulikuwa ujumbe kutoka kwa Mungu. Kwako wewe, ujumbe unaopewa hauna nia njema na wala hautoki kwenye nuru, bali kwenye giza. Kwa bahati nzuri, bado kuna nguvu (yawezekana wewe mwenyewe, wazazi, au mababu; maana nguvu huwa haipotei: conservation of energy), ndio inayokusaidia.

Nini cha kufanya? Tekeleza uliyoambiwa na watu wa Mungu, wala usipuuzie. Utawajuwa watu wa kweli wa Mungu, na wale wasio wa kweli, fuata maagizo ya wale wa kweli. Kwa mfumo aliotuwekea Mungu hapa ulimwenguni, hakuna tatizo lisilo na suluhisho, na ndio maana kila mtu alipewa kipawa tofauti na mwingine, ili kila mmoja awe na msaada kwa mtu mwingine.
Kuna watu wa shetani kumbe.
Asante mkuu kwa kunifundisya jambo jipya siku ya leo.
 
Hakuna kukabwa,ni ulimi unaziba tundu la hewa,na wanaodai kukabwa wote hulala chali
Ulimi huwa unaziba ndundu la hewa wakati gani? Je ni mcha au usiku au ukilala tu? Mfano mimi ilikuwa ikinitokea hili nikiwa sijalala chali mida ni sa nane usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi. Unawezaje kunielezea kuhusu upande wangu pia?
 
Unajuaje kwamba hukulala chali!?...unapolala mwili hulegea,hata vishuzi hukutoka bila kuamua,ulimi nao hulegea,hurudi nyuma na kuziba tundu la hewa
 
Unajuaje kwamba hukulala chali!?...unapolala mwili hulegea,hata vishuzi hukutoka bila kuamua,ulimi nao hulegea,hurudi nyuma na kuziba tundu la hewa
Ninaelewa kwa sababu nilivyolala ndivyo ninavyoamka huwa najiona sijabadili ulalaji. Lakini hujanijibu maswali yangu mengine.
 
Kuna watu wa shetani kumbe.
Asante mkuu kwa kunifundisya jambo jipya siku ya leo.
Wote tuliumbwa kuwa watu wa Mungu, ila ni sisi wenyewe tunaamua kuacha kufuata njia za Mungu na kugeukia njia za shetani.
 
Ukiona unaota hiyo ni neema yani Mungu anakusemesha juu ya hatari ijayo au mabaya yalio kupata yanatokana na nn! Sasa Kwa kutoa sadaka uku umeisemesha e.g Kwa sadaka hii Mungu ingilia kati)Au To a yamkini kuna makosa ulitenda kwa kujua na kwakutokujua.
 
Wote tuliumbwa kuwa watu wa Mungu, ila ni sisi wenyewe tunaamua kuacha kufuata njia za Mungu na kugeukia njia za shetani.
Nafikiri ungemjibu hivi wote ni watu wa Mungu ila watu wote si watoto wa Mungu.

Mathayo 12:34 NEN​

Enyi uzao wa nyoka! Mnawezaje kunena mambo mema, wakati ninyi ni waovu? Kwa maana kinywa cha mtu huyanena yale yaliyoujaza moyo wake.

Nyoka ni nani? Ni shetani

Ufunuo 20:2​

Akalikamata lile joka – nyoka wa kale, yaani Ibilisi au Shetani – akalifunga kwa muda wa miaka 1,000.
 
Back
Top Bottom