Ndoto tunazoota na tafsiri zake

Mara nyingi kuna ndoto hizi zinajirudia sana
Kwanza huwa naota either nimewachokoza watu au nimeiba kitu wanavyonikimbiza napaa juu naenda umbali mrefu sana natua sehemu baadae naendelea kupaa naenda mbali sana
Ya pili huwa naota nipo na mtu nnaemfahamu lakini baadae anakuja kugeuka sura anakuwa mtu wa kutisha na huwa nasali mpaka hanidhuru au nakutana na kundi la watu nywele zinasisimka kabisa naanza kusali pia watu hao wanageuka kuwa wa kutisha wanashindwa kunidhuru msaada
 
Msaada wakuu mi nnaota naokota hela na hii ndoto inajirudia sana tu msaada tafadhali
 
Okoka kwanza. Mpe Yesu maisha yako. Nenda kanisani ukaombewe halafu mwambie Mungu akutoe kwenye hilo jeneza cz wamekuua ktk ulimwengu wa kiroho ingawa unajiona mzima. Mwisho utakuta mambo hayaendi kabisa. Damu ya Yesu ikutoe ktk hilo jeneza uwe huru sasa. Tulitolewa ktk ufalme wa giza tukahamishwa na tukaingizwa ktk ufalme wa mwana wa pendo lake( Yesu kristo) Yesu akutoe huko ulipo uwe huru sasa. Ulalapo mwambie Mungu nifunike kwa Damu Ya Yesu. Kuwa na imani utatoka huko bt usiache kuomba na uwe mwaminifu kwa Mungu siku zote.
 
Mmh mercky ngoja tu niseme neno kwamba hiyo ndoto ilikuwa na maana mbili
1. Alikuwa anawangiwa ndio maana kaamka kichwa kinamuuma
2. Ni ndoto tu ya kawaida inayomtabiria mema kwakuwa kuna baadhi ya ndoto tafsiri huwa kinyume
Hiyo ndoto haimtabirii mema hata kidogo na akiipuuza atakuja kusema hapa. Ndoto ni mlango ambao shetani anautumia sana na ni mlango ambao Mungu anautumia kusema na sisi. Hapo kaamka kichwa kinamuuma ni kwel kabisa ktk ulimwengu wa kiroho wamemuua na pindi alipo amka kaamka kafadhaika na amekosa raha. Hakuna chema hapo kaka yangu shetan kapata nafasi ya kuingia na ana uhalali bila shaka hadi kuingia huko. Yampsa amwambie Mungu aingilie kati ili shetani akose uhalali katk maisha yake. Cz ndoto inagusa nafsi na nafsi ikifungwa ni hatari.
 
Mkuu sina jipu,sidaiwi wala sitembei na mke wa mtu. Labda Kama kuna mtu ananichezea tu.
mbona avatar yako ni mke au wewe jike dume?
ndio mahana unaota ndoto mbaya.

swissme
 
mbona avatar yako ni mke au wewe jike dume?
ndio mahana unaota ndoto mbaya.

swissme

Avatar yangu haihusiani na Mimi na si lazima kila avatar inayoonekana kwa ID ya mtu imuhusu kwani ni dhambi kumuweka mtu mwingine vipi Kama ni mke wangu? Vipi huyo wa kwenye avatar yako ni wewe? Vipi kwa wale wanaoweka picha za simba ,chui au vitu Kama hivyo nao ni chui au simba?
 
mbona ndoto zetu hazipati majibu?au mwenye uzi amesinzia???
 

Hii nimeiota leo hii hii,
Nimeota kuna mtu anagonga mlango huku akiita jina langu kwa sauti, tena sauti ya kike akitaka nimfungulie.ghafla nikashituka na sikusikia ile sauti,nikafungua mlango sikuona mtu lakini tangu muda ule sauti yangu imekauka haitoki vizuri,hii ina maana gani?
 
Huyo ni mchawi....ndugu...kila kitu kinachotokea kwenye Mwili ujue chanzo chake ni Ulimwengu wa Roho....watu wanarogwa sana kupitia ndotoni....utakuta unapigiwa Simu ukiwa usingizini....Lazima ujue namna yakuikemea hiyo hali iishie huko huko...
 
kuna watu(wachawi) walichukua sauti yako kimiujiza.
 
yote yanayotukia ktk maisha hutanguliwa na ulimwengu wa roho, uotacho ndicho hutokea au dalili ya kinachofanyika ktk ulimwengu wa roho
 
kuna kundi la wachawi huwa wanakuja kukudhuru ila huwa wanashindwa.
 
Mie niliota ndoto nang'oka meno kuna mama flan alininunia sasa nilipotazamana nae katika ndoto ndo baada ya mda mfupi nikawa nashindwa kuongea baada ya mda kidogo ndo nikawa naskia meno yanang'oka matatu ya juu.
Mkuu ina maana gani hiyo?
 
Ktk maisha tunakutana na changamoto nyingi sana,ktk mchakato huo basi nikajikuta tumefarakana na jamaa mmoja hivi na hatimaye tukaingia kwny bifu zito.
Hali iliyopelekea mpaka kukatika kwa mawasiliano baina yetu...Sasa juzi nimeota nimekutana na jamaa kanipokea Kwa bashasha tukaenda mpk kwake Kwa ajili ya chakula, nilipofika kwake mke wake alikasirika ....hebu nitafsirie Mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…