Ndoto ya wengi ni Kazi, nyumba, Familia, mwisho Gari

Ndoto ya wengi ni Kazi, nyumba, Familia, mwisho Gari

Siyo kuwa na demu mwenye makalio makubwa?
Nakazia
IMG_20240202_124542.jpg

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Basic Needs Zimekuwa Ndoto Za Watu?

Ndoto Inatakiwa Iwe Tofauti Na Mahitaji Ya Muhimu (Basic Needs) Maana Basic Needs Ni Lazima Uwe Navyo Kwanini Iwe Ndoto Tena Kuvipata.

Inabidi Tujitazame Vyema Tuone Tunakwama Wapi.

Kwa lugha nyepesi ni kuwa ni ndoto ya watanzania wengi kufukuza umaskini
 
Kwema!

Kibongobongo wengi ndoto yao ni kupata kazi, kisha nyumba( inaweza kuwa uwezo wa kulipia apartment), Familia(mke au mume na watoto) alafu mwisho usafiri kama kagari Fulani hivi kakishkaji.

Imeisha hiyo
Unakula kwa shida.

Umepanga au huna pa kulala.

Huna familia kwasababu maisha yako mwenyewe bado unayamudu kwa shida.

Unabanana kwenye daladala Kama mjusi.

Kuna tatizo kuwa na ndoto za kujitoa kwenye hali hiyo, kwanza????
 
Yeah àiming high is the best choice
Huwezi ku-aim high wakati hata kula kwako ni shida, utaokota makopo.

Utajiri ni uwekezaji unaotokana na compounding. Na Huwezi kuwekeza pesa ya KULA.

Siku zote utawekeza SURPLUS, na surplus itapatikana kwa Kwanza unapomudu KULA, KULALA VIZURI na KUSAFIRI VIZURI itakavyowezekana
 
Ni basics ndio ila sio wote wako blessed nazo, na wanatamani siku wazitimize ili waonekane nao wanaishi. Kuna watu wanajenga nyumba inaisha upande mmoja anahamia na bado watu wanamtamani...😊
Unamjua huyu mwanariadha wa Kenya anaitwa Kiptum alovunja rekodi ya mbio za km 42 na alipanga awe mtu wa kwanza kukimbia chini ya masaa mawili kwenye marathon ya April? Kafariki kwenye ajali ya gari juzi na kocha wake..ndoto yake ilikua kujengea familia yake nyumba na amefariki kabla hata hajajenga na sasa familia inahaha serikali iwasaidie. Kaacha legacy kubwa kwenye mbio na dunia inamtambua maana vyombo vyote vikubwa vya habari duniani vimetangaza habari ya kifo chake,lakini pamoja na hiyo achievement kaiacha familia kwenye hali mbaya. Tusidharau ndoto za basic needs.
Huwezi kuwaza dreams wakati una struggle kwenye eneo basic la maisha yako.
 
Huwezi ku-aim high wakati hata kula kwako ni shida, utaokota makopo.

Utajiri ni uwekezaji unaotokana na compounding. Na Huwezi kuwekeza pesa ya KULA.

Siku zote utawekeza SURPLUS, na surplus itapatikana kwa Kwanza unapomudu KULA, KULALA VIZURI na KUSAFIRI VIZURI itakavyowezekana
Huo ndio uhalisia mkuu, hata wenye vikubwa walianza from somewhere. Lazma uwe na pakushika kwanza ndio usogee
 
Huo ndio uhalisia mkuu, hata wenye vikubwa walianza from somewhere. Lazma uwe na pakushika kwanza ndio usogee
Halafu watu hawajielewi kwasababu ya tamaa zao.

Matajiri wengi walianzia kwenye msingi mzuri.

Unakuta baba au babu yako alianzia sehemu akafikia stage fulani ya maisha na wewe unaanzia hapo.

Sisi kila anayezaliwa anaanza upya.

Tena unazaliwa unakuta baba yako bado amepanga chumba kimoja Kwa Aziz Ally.

Maana yake, ndogo zako lazime ziwe kuboresha Maisha yako yasiwe Kama ya wazazi wako pamoja na kuboresha Maisha ya kwenu ukiweza.

Unless uwe na talent ikuoe booster.

Lakini wengi wetu tunaotegemea Ualimu au ujasiriamali wa duka la mangi au kuchoma chipsi, ndogo kubwa utabebeshwa sembe, utafirwa au utatembea sana kwa waganga na kila siku utawaza stori za paka mweupe na rupiah za wahindi.
 
Ni basics ndio ila sio wote wako blessed nazo, na wanatamani siku wazitimize ili waonekane nao wanaishi. Kuna watu wanajenga nyumba inaisha upande mmoja anahamia na bado watu wanamtamani...[emoji4]
Unamjua huyu mwanariadha wa Kenya anaitwa Kiptum alovunja rekodi ya mbio za km 42 na alipanga awe mtu wa kwanza kukimbia chini ya masaa mawili kwenye marathon ya April? Kafariki kwenye ajali ya gari juzi na kocha wake..ndoto yake ilikua kujengea familia yake nyumba na amefariki kabla hata hajajenga na sasa familia inahaha serikali iwasaidie. Kaacha legacy kubwa kwenye mbio na dunia inamtambua maana vyombo vyote vikubwa vya habari duniani vimetangaza habari ya kifo chake,lakini pamoja na hiyo achievement kaiacha familia kwenye hali mbaya. Tusidharau ndoto za basic needs.
Habari ya huyu mwanariadha Kiptum Cheruiyot imenisikitisha sana.
 
Back
Top Bottom