Ndoto ya wengi ni Kazi, nyumba, Familia, mwisho Gari

mkuuu umepangilia hadi nimeogopa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Kuna mambo ukiyatazama kwa utulivu unabaki kuguna tu moyoni maana ukifungua kinywa unaweza ukakufuru. Kuna watu wanazaliwa mpaka wanakuwa kitu kinachoitwa shida au umaskini wanausoma kwenye Nyambari Nyangwine tu.

Ni watu ambao uthubutu wao uko close to perfect na chochote atachofanya atafanikiwa tu maana resources zote ako nazo from the start. Hata akianzisha usindikaji wa asali leo hii ataipromote na atauza tu na kuwa tajiri mkubwa ndani ya miaka michache.
 
uzuri hakuna sheria inayosema lazima kila mtu atoke nyumbani akaishi mwenyewe πŸ˜ƒ
 
Sure .Connection zote izi hapa.
 
Sure mzee.maana back up anayo pia ana stress na vitu vidgo vidgo.
 
Mfano mtu ni graduate ni jobless miaka zaid ya 5 unafkr atakuwa na ndoto kubwa.
 
uzuri hakuna sheria inayosema lazima kila mtu atoke nyumbani akaishi mwenyewe πŸ˜ƒ
mkuu ukiona mtu mazingira yanamlazimu kutoka home basi asilimia kubwa home hakuna cha kufanya inaumiza sana moyo... imagine mtu anakua anakuta home miradi ipo ya hela ndefu huyo hata wazazi wake watamkazia abaki home asimamie miradi mbali na hapo labda kama kijana hajielewi na hakuna raha kama kukaa home unaona mambo yanavyokwenda ukitaka kuanzisha kitu una full support kuanguka ni ngumu sana
 
ngozi nyeusi tulilaaniwa na mizimu πŸ˜‚πŸ˜‚ unakuta mtu anaweza kuendeleza vya home ila kwulimbukeni na ubinafsi anakwenda kusota ili aseme alikomaa akapata kitu fulani wakati hicho hicho angelata akiwa home na mambo yakanyooka....
 
hapo kwenye mapenzi hahahaha mkuu nimecheka sana
 
Mfano halisi ni vibiashara vya Azam Pesa na Sarafu, vimejiegesha kwenye BRAND kubwa ya Azam.

Lakini ukifuatilia waanzilishi wa hizo kampuni siyo hata Bakhresa, Wala watoto wake.
 
Nazani elimu inayotolewa haifiti kwa maisha ya sasa wenzetu huko ulaya vijana wao wakihimu makampuni kibao yanawataka sisi huku kwetu ni changamoto sana
 
Kujilinganisha na Wahindi ni UZUZU mwingine.

Mhindi Kwanza hahitaji mtaji kuanzisha biashara hata kubwa kunwa.

Mhindi akiweza kulipa Kodi ya frame, mzigo anaweza kuchukua Sayona, Metl, Murzal au Jambo.

Anachofanya ni kuuza na kuchukua faida tu baada ya mauzo.

Wewe takataka hakuna anayekwamini kwanza
 
Kuna lengo la maisha, halafu kuna mambo ambayo yanakusaidia kulifikia lengo.

Hapo kwenye lengo ndio kuna maana ya maisha yenyewe,ambapo watu wanatofautina mitazamo na malengo ya maisha.
Lakini msingi mkuu wa hii mitazamo ni kile anachokiitakidi mtu baada ya yeye kuondoka hapa duniani.

Kuishi maisha bora ni jambo lenye kuhitajika kwa kila mwanaadamu, haijalishi wewe uanayatafsiri vipi maisha bora.

Ila waliokosa maarifa wameyafanya yale mambo ya kuwasaidia kufikia lengo la maisha, kuwa ndio lengo la maisha yenyewe.
 
Ni kweli ila sio kila mtu ana guts za kupata hivyo vitu maishani. Njia halali kufikia ndoto zetu imekuwa ni ngumu sana kwenye corrupt country kama yetu hii na ikiwa huna mtaji wala connection.
Mtaji sio tatizo sababu mtaji wa kwanza ni wewe mwenyewe kuwa mzima wa afya

Hii nchi kwa sasa shida ipo kwenye elimu inayotolewa mashuleni haiendani na kasi ya ukuaji wa technologia dunia kwa sasa inahitaji watu wanaotumia zaidi maarifa kuliko nguvu

Wenzetu wanaandaa mpango kupunguza masaa ya kufanya kazi sababu wameshagundua kufanya kazi masaa mengi hakuleti matokeo makubwa
 
Kimsingi kuna watu wameamua kuchagua kupata matokeo kabla ya kufikiria kufikia malengo sio kosa lao kufikia malengo kunahitaji watu wenye maarifa na elimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…