Sean Paul
JF-Expert Member
- Jun 16, 2013
- 1,330
- 3,289
Mkuu jibidiishe kusoma.Umeleta ushahidi wa hiki ulichoandika?
Katika Uislam kuna vitu vya lazima, hivi huitwa FARADHI, kuacha na kutenda. Vile vya kuacha ukivifanya unapata dhambi na vya kutenda usipotenda unapata dhambi. Mfano sala, usiposali unapata dhambi na usizini, ukizini dhambi. HIYO NDIO MAANA YA LAZIMA katika uislam. Vitu vyote vilivyopigwa marufuku vimeelezwa katika kitabu chao Quran. Hakuna maelezo katika Quran yanayoelekeza mtu azikwe siku gani au azikweje.
Sambamba na hilo, kuna mafundisho na matendo ya Mtume wao (SAW), aliyoyaelekeza kufanya. Haya, sio lazima kwamba yafanyike. Mfano Muhammad ndio kaelekeza wazikane namna gani. Lakini hakuna ulazima mtu azikwe hivyo, lililo muhimu mtu azikwe na uchache wa kumzika mtu ni kumuweka kaburini na kufukia. Hayo mengine ni ziada tu.
Katika maelezo yake Muhammad kapendekeza mambo yafuatayo yafanyike haraka ikiwa yatatokea
1. Mtu akifa azikwe haraka kama hakuna sababu ya kuchelewesha.
2. Mtu akitaka kusilimu asilimishwe fasta.
3. Watu wakitaka kufunga ndoa waozeshwe haraka.
Kwahiyo kwa sababu walizo nazo wenyewe Wairan, wanachelewesha maziko na wala hawapati dhambi.
Kama una hoja lete.