Ndugu yangu alishinda betting milioni 7 na laki 4 mwezi wa kwanza, kwa sasa anatia huruma, hii michezo ina maendeleo kweli?

Ndugu yangu alishinda betting milioni 7 na laki 4 mwezi wa kwanza, kwa sasa anatia huruma, hii michezo ina maendeleo kweli?

Nilitegemea pesa hizo zitamsaidia kwamba mwaka umeanza vizuri kwake walau afanye cha maana afungue hata biashara lakini nimekuja kumfatilia naona hakuna la maana alilofanya,

Kwa machache nayoyajua:

  • alinunua simu ya laki 9 kaiuza kwa hasara kubwa mno
  • alinunua Tv kubwa nzuri kama kainunua dukani ni milioni 1 na laki 2, kaiuza kwa hasara kubwa mno
  • mwanzoni alikuwa anabeti kwa pesa ndogo, aliposhinda anabetia mpaka laki
  • alinunua kifriji cha kutunzia katoni za grand malt, ndio yalikuwa maji kwake (hanywi pombe)

Cha maana alichofanya labda kanunua pikipiki mpya, sizijui vizuri bei ila itakuwa inakaribia milioni 2, maybe aifanye iwe boda
Ndugu yako alichokosa ni kitu kidogo, nidhamu ya pesa. Na kucheza na nyakati. Na hii ndio tofauti ya maskini akipata pesa na tajari akipata pesa
 
Elimu ya fedha wengi imetupita kushoto na hatutaki kufatilia.
Wakina sisi tukishapata hela tunachachawa

Tukiwa hatuna hela (apeche alolo) tunakuwa na mipango mingi ambayo ukiiangalia unajiona mbali kabisa kupitia hizo plan ulizoweka KASHESHE inakuja pale unapopata zali ukapata MTONYO mkubwa, sijui ile mipango huwa inayeyukia wapi..Akili zinahama kwa muda unajikuta unafanya mambo ambayo hayakuwa kwenye ile mipango yako uliyopanga, na pesa ilivyo Ukishaanza kufulia ndio kichwa kinakumbuka ile mipango..

Wengine wanasema pesa inakuwaga na uchawi (japo mi nakataa) kwamba Inampa mtu kiburi, dharau, majigambo, kuvimba na kujiona yeye ndio yeye ila ikiisha tu huyo mtu anavyokuwa mdogo mpaka inasikitisha..

Nashauri watanzania tujifunze kila siku nidhamu ya pesa na tupate maarifa ya kutunza hela

Ukitunza pesa sasa hivi itakuheshimisha baadae
 
Na mimi nilitaka kusema hivo.
JF inaruhusu kutumia Kiingereza ila jamaa ana broken English mpaka msomaji unakasirika huyu mtu alikusudia kusema nini.
Jamaa chenga kabisa anatuona mazuzu humu wakati hajui hata wakenya tupo humu tunamchora tu
 
Nashauri watanzania tujifunze kila siku nidhamu ya pesa na tupate maarifa ya kutunza hela
Mkuu watu ni wa jeuri. Anakwambia ajifunze elimu ya fedha na hajui atashika lini hizo pesa wanashindwa kuelewa hata hizi ndogo ndogo tunazoshika bado zina impact kubwa kustimulate maendeleo. Ajabu ni kwamba hata siku akipata ndio hataki kabisa kushauriwa na kuambiwa kuhusu matumizi sahihi ya hizo pesa🤣🤣
 
Uharamu wa kamali ni upi,?

Hivi kwanini huongeagi lugha ya taifa mkuu, does it somehow give you a feeling of being smart just to speak what many Tanzanians can't comprehend ?
Dah ngoja na Mimi niteme ngeri kidogo naona soft ware yangu kumkichwa imelowa na Mvua,, we have no problem with his love for speaking english but since all of us here are using Swahili language, what is the point of him for using English
 
Mkuu unajua watu wangapi wanapata take home ya zaidi ya 1M hapa bongo ?
Nurses, walimu, wafamasia, polisi, Askari,

Hawa ndo wengi bongo na wote wanakula chini ya M, hapo nazungumzia wenye Bachelor, hizo diploma wanakula 500 -600,
Halafu unasema 1M ndogo ?
Kaka unatumia nguvu nyingi kumuelewesha mtu aliejiandaa kutoelewa hoja yako. 1M ni pesa kubwa,ni mtaji wa mtu huo.
 
Nilitegemea pesa hizo zitamsaidia kwamba mwaka umeanza vizuri kwake walau afanye cha maana afungue hata biashara lakini nimekuja kumfatilia naona hakuna la maana alilofanya,

Kwa machache nayoyajua:

  • alinunua simu ya laki 9 kaiuza kwa hasara kubwa mno
  • alinunua Tv kubwa nzuri kama kainunua dukani ni milioni 1 na laki 2, kaiuza kwa hasara kubwa mno
  • mwanzoni alikuwa anabeti kwa pesa ndogo, aliposhinda anabetia mpaka laki
  • alinunua kifriji cha kutunzia katoni za grand malt, ndio yalikuwa maji kwake (hanywi pombe)

Cha maana alichofanya labda kanunua pikipiki mpya, sizijui vizuri bei ila itakuwa inakaribia milioni 2, maybe aifanye iwe boda
Kailamba Lolo mzee ndio chaguo
 
Mkuu unajua watu wangapi wanapata take home ya zaidi ya 1M hapa bongo ?
Nurses, walimu, wafamasia, polisi, Askari,

Hawa ndo wengi bongo na wote wanakula chini ya M, hapo nazungumzia wenye Bachelor, hizo diploma wanakula 500 -600,
Halafu unasema 1M ndogo ?
Mimi ukinikamatisha 1M siku 2 nyingi imekata ndio maana nakwambia ni ndogo sana,
 
Kaka unatumia nguvu nyingi kumuelewesha mtu aliejiandaa kutoelewa hoja yako. 1M ni pesa kubwa,ni mtaji wa mtu huo.
1M ni ndogo sana au niseme ilikua kubwa labda kwa Mwaka 2000 sio 2024, 2024 buku haina thamani buku10 ndani ya dakika 15 imeyeyuka tena hizo dakika 15 nyingi sana ni dakika 1 ukigusa tu imeyeyuka nini 1M?

Ukipewa 200M leo haimalizi Miezi 6 imekata nini 1M, nazungumzia matumizi sio uwekezaji, yaan tukupe 200M utumie tu usifanye uwekezaji wowote Miezi 6 hutoboi imeyeyuka nini 1M?
 
kaka mcheza kamar na maendeleo ni kama mwiz na polis cz kufanya maendeleo kwa hela ya kama labd uliend ku test zal tu ukabutua uachane na kamar ufocus na mamb yako ila mchez kamar knachmfnya asiendlee akila lak kwa buk anaona ngoj nbet kwa ef10 nile milion akila km ivo milion 7 azngatii alichopt anaamn ipo siku atapga hela nying zaid na hapo ndo shida atlist umkut ana net na anafanya mishe zngine za kipato il km anatgmea kamar ni kufel tu mwisho wke
 
Bora yake yeye anaweza kuipata hio hela tena hata kwa njia nyingine za kihalali
kuna mwamba apa wakuitwa Michael Carroll alishinda lotto £ 9.7milion zaid ya 31.5B ya kibongo mwamba akaanza bata za hatari advtaiz kiongoz alikua anahudumiwa na wahudumu wakiwa uchi, group sex na madem 9 karibia milion tano za kibongo kwenye cocain daily baada ya muda mfupi mwamba akawa pumbu kabisa kushinda hata huyo ndugu yako bora yake yeye kabak na boda na kafriji kakuwekea visungura mwamba wa island alibaki tee kabisa saiv anafanya kaz ya kukusanya magogo kwenye kiwanda cha makaa ya mawe analamba dola kumi kwa saa ilikwamba aweze kuikamata ile hela alioskwanda ndani muda mfupi itabid apige mzigo kwa masaa milion moja na laki mbili na ishilini na tano elfu miatisa kumi na tano 1,225,915.1 ATTACH=full]2954021[/ATTACH]View attachment 2954021
Nimefuatilia huyu mwamba ana vituko
 
Back
Top Bottom