Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemuandikia barua mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu ya kumuita katika kikao cha kamati ya maadili ya Taifa.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dkt. Charles Mahera amesema hilo leo jijini Arusha wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa mgombea huyo atafika mbele ya kamati Septemba 29 mwaka huu.
Akizungumzia uratibu na usimamizi wa kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu amesema tume imekumbana na changamoto kwa baadhi ya wagombea wa kiti cha Rais kutoheshimu sheria, taratibu na maadili ya uchaguzi.
Ameongeza kuwa baadhi ya wagombea wamekuwa wakitumia maneno ya kukashifu wagombea wenzao, tume, pamoja na kutoa taarifa zisizo za kweli zenye lengo la kuleta taharuki na uzushi miongoni mwa Watanzania.
Huyu Mkurugenzi Charles Mahera tunajuwa namna alivyopata hii nafasi ya Ukurugenzi wa NEC kwa upendeleo ili aje atumike kumptisha Magufuli akishindwa au atengeneze mazingira ya Magufuli kushinda.
Haiingii akilini kwa kutomuandikia Magufuli kwa vitendo vya wazi wazi anavyovifanya kwenye mikutano ya Kampeni hasa anapotoa maagizo kwa TANROADS kujenga mababara.
Nitoe onyo tu, Mahera akumbuke ana familia inayomtegemea, akimfumbia macho Magufuli na kukubali maagizo anayompa itamgharimu yeye na kizazi chake. Mwaka huu CHADEMA hatuibiwi!!!
TL asiende tukianzishe hapa hapa. Haina haja ya uchaguzi tena.
Wamuite Magufuli kwanza - anadhalilisha akina mama, anafokea wapigakura eti hawapati maendeleo wakichagua wapinzani, sasa wanasema eti TL ana uraia wa nchi nchi nyingine! Waache ushenzi Watanzania tuamue kiongozi tunayetaka atuongoze.
Majibu ni marahisi tu, kuwa tume ya uchaguzi sio huru. Wagombea kibao wa upinzani wameenguliwa na tume ya uchaguzi kwa hila, na wagombea wa ccm wanavunja sheria wazi wazi bila kuchukuliwa hatua. Ni hivi, safari hii kuchezea kokote matokeo hakutakuwa na kumuachia Mungu fullstop.
Baada ya wagombea urais kuapishwa DEDs wanawajibika kwa NEC. Kitendo cha Magufuli kuwaita DEDs Dodoma yeye akiwa mgombea alivunja sheria za uchaguzi kwa kiwango cha kutishia amani.