Uchaguzi 2020 NEC yamuita Tundu Lissu kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya Taifa

Parasatic Mind

CCM inasubiri mbeleko ya NEC na Wakurugenzi

Tatizo watu wana maisha magumu

Fujo na vurugu na Maandamano husababishwa na ugumu wa maisha

Venezuela huko tatizo watu maisha magumu

NEC inajichimbia shimo zaidi
Yaani tumewalea sana karibu uvumilivu utakoma!
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemuandikia barua mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu ya kumuita katika kikao cha kamati ya maadili ya Taifa.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dkt. Charles Mahera amesema hilo leo jijini Arusha wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa mgombea huyo atafika mbele ya kamati Septemba 29 mwaka huu.

Akizungumzia uratibu na usimamizi wa kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu amesema tume imekumbana na changamoto kwa baadhi ya wagombea wa kiti cha Rais kutoheshimu sheria, taratibu na maadili ya uchaguzi.

Ameongeza kuwa baadhi ya wagombea wamekuwa wakitumia maneno ya kukashifu wagombea wenzao, tume, pamoja na kutoa taarifa zisizo za kweli zenye lengo la kuleta taharuki na uzushi miongoni mwa Watanzania.

Chanzo: TBC Online
kama ni kweli najua kila tukio huwa ni fursa kwa Lisu hivyo kwenye kikao hao NEC watakamatana uchawi wenyewe jamaa atakavyo wanyooshea,na uzuri wakimaliza kikao Lisu anatuletea tena hadharani walichozungumza kwenye kikao
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemuandikia barua mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu ya kumuita katika kikao cha kamati ya maadili ya Taifa.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dkt. Charles Mahera amesema hilo leo jijini Arusha wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa mgombea huyo atafika mbele ya kamati Septemba 29 mwaka huu.

Akizungumzia uratibu na usimamizi wa kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu amesema tume imekumbana na changamoto kwa baadhi ya wagombea wa kiti cha Rais kutoheshimu sheria, taratibu na maadili ya uchaguzi.

Ameongeza kuwa baadhi ya wagombea wamekuwa wakitumia maneno ya kukashifu wagombea wenzao, tume, pamoja na kutoa taarifa zisizo za kweli zenye lengo la kuleta taharuki na uzushi miongoni mwa Watanzania.

Chanzo: TBC Online
Hatumwogopi huyo mkurugenzi
 
Huyu Mkurugenzi Charles Mahera tunajuwa namna alivyopata hii nafasi ya Ukurugenzi wa NEC kwa upendeleo ili aje atumike kumptisha Magufuli akishindwa au atengeneze mazingira ya Magufuli kushinda.

Haiingii akilini kwa kutomuandikia Mahufuli kwa vitendo vya wazi wazi anavyovifanya kwenye mikutano ya Kampeni hasa anapotoa maagizo kwa TANROADS kujenga mababara.

Nitoe onyo tu, Mahera akumbuke ana familia inayomtegemea, akimfumbia macho Magufuli na kukubali maagizo anayompa itamgharimu yeye na kizazi chake. Mwaka huu CHADEMA hatuibiwi!!!

Sasa watoa vitisho ukitumia jina la bandia ndo waona umetishia kwelikweli.
 
Huyu Mkurugenzi Charles Mahera tunajuwa namna alivyopata hii nafasi ya Ukurugenzi wa NEC kwa upendeleo ili aje atumike kumptisha Magufuli akishindwa au atengeneze mazingira ya Magufuli kushinda.

Haiingii akilini kwa kutomuandikia Mahufuli kwa vitendo vya wazi wazi anavyovifanya kwenye mikutano ya Kampeni hasa anapotoa maagizo kwa TANROADS kujenga mababara.

Nitoe onyo tu, Mahera akumbuke ana familia inayomtegemea, akimfumbia macho Magufuli na kukubali maagizo anayompa itamgharimu yeye na kizazi chake. Mwaka huu CHADEMA hatuibiwi!!!
Usitishe watu bhana tunajua mmepanga nini ila hamtafanikiwa. Kama vipi mwambie asiende basi uone-ebo
 
Back
Top Bottom