NECTA yathibitisha tuhuma alizotoa mwanafunzi wa Chalinze Modern Islamic ni za kweli, Yaifungia shule

Kawaida wazazi wana shirikiana na walimu ktk hizi tuhuma

Pia walimu utumia kusaidia vijana wao wasio jiweza waweze kutusua ili waweze kupata marks za kwenda shule nzuri private au government
.... mbaya sana! Ni zaidi ya ushetani kumnyima mwenye haki haki yake!
 
Hii ni habari kubwa sana kwa watu wanaotaka mfumo wa kuendesha elimu yetu ubadilishwe. Hiyo ilikuwa ni English Medium.

Jinsi vyombo vyetu vya habari vilivyo dhaifu unakuta kumuita huyo mtoto kufanya naye stori, inakuwa ngumu.
 
Kwaiyo hichi ulichokiandika ndio kimepangilia vizuri?
 
Huyo binti Serikali impeleke shule za vipaji maalumu anaonyesha ana akili nyingi mno kuanzia darasani hadi uelewa mkubwa wa kisheria wa kudai haki zake

Mbeleni aweza ifaa nchi huyo Nadhani naeleweka kwa wenye uelewa
... yuko vizuri sana upstairs! Kitendo cha kuwa bold kudai haki yake tena kwa level yake ya STD7 yuko vizuri sana. Wengine hata F4, F6, hata vyuo huko wangeogopa kudai haki zao kama kawaida ya watanzania walio wengi.

Mfano, mtu mzima anaenda kununua bidhaa iwe dukani, sokoni, buchani, n.k anaona kabisa mizani "imechezewa" lakini kumwambia live muuzaji anaogopa! Huyo binti achongewe sanamu kama mdai haki mdogo zaidi kuwahi kutokea nchini.
 
Hao walimu waliohusika kwenye ujinga huo wamelaaniwa na watapata laana kubwa hapa duniani na akhera. Hawawezi kucheza na maisha ya watoto kwa sababu za kipuuzi wanazozijua wao wenyewe.
 
ccm mna vituko 😄
Tuhuma si za kweli. Shule imefungiwa.Hau?
🤣
 
Hii ni habari kubwa sana kwa watu wanaotaka mfumo wa kuendesha elimu yetu ubadilishwe. Hiyo ilikuwa ni English Medium.

Jinsi vyombo vyetu vya habari vilivyo dhaifu unakuta kumuita huyo mtoto kufanya naye stori, inakuwa ngumu.
... ha ha ha! Inaonekana unachukia sana mfumo wa elimu kwa Kiingereza Mkuu. Kwenye hii issue English inaingiaje?
 
Yaani ni shida qumeermake,sijui wanafundisha nini huko shuleni siku hizi!!
 
Huwa kuna tuzo ya Mwanamke jasiri nimesahau watoaji huyu msichana watetezi wa haki za binadamu ,vyama vya wanasheria nk wampe tuzo ya jasiri

Msichana kusimama single handedly kutafuta haki yake

Hakuna mijitu mibwege nchi hii kama hao wanaojitia watetezi wa haki za binadamu Tanzania. njaa tu unawasumbua.Mtoto kwa kuwa hakuwa na hela hakuna hata taasisi moja ya kutetea haki za jamii iliyojitokeza kumsaidia.Waliufyata sababu wanaona hamna maslahi ya hela.

Hata Chadema wanaojifanya watetezi wa wananchi hawakujitokeza walijifungia kwenye vyoo vya ofisi ya makao makuu ya Chadema Ufipa.Utafikiri hata hawakusikia malalamiko ya huyo mtoto

Huyo msichana apewe nisha ya ujasiri ita motivate wasichana wengine kuwa bold kwenye kudai haki zao ns kuwa na misimamo wanapoonewa au kutaka kuonewa

Niwapongeze waandishi wa habari wamefanya kazi kubwa sana
 
... hapo Chadema inaingiaje? Sio lazima kila kitu uingize siasa.
 
... ha ha ha! Inaonekana unachukia sana mfumo wa elimu kwa Kiingereza Mkuu. Kwenye hii issue English inaingiaje?
Kwanza sichukii mfumo wa kutoa elimu kwa Kiingereza. Lakini kama Kiingereza ni kuelewa mbona kuna watoto ilibidi wafanyiwe mitihani yao na wengine??

Kufundisha kwa Kiingereza kuanzia darasa la Kwanza mpaka chuo Kikuu siyo suluhisho kwa matatizo ya mfumo wetu wa elimu uliojaa mataka taka ya kutosha.

.. yuko vizuri sana upstairs! Kitendo cha kuwa bold kudai haki yake tena kwa level yake ya STD7 yuko vizuri sana. Wengine hata F4, F6, hata vyuo huko wangeogopa kudai haki zao kama kawaida ya watanzania walio wengi.
Umeona ulichokuwa umeandika hapa. Kumbe watu wapo F4,F6 au chuo kikuu hawajafikia daraja ya Iptsum.

Elimu na Lugha ni kama Kapu na kinachobebwa. Kama kinachobebwa ni kinyesi hata kapu liwe zuri kiasi gani bado harufu itatoka na karaha itapatikana. Lakini kama kinachobebwa ni dhahabu, basi hata kama kapu ni bovu kiasi gani, haliwezi kupunguza thamani ya dhahabu.
 
... kwenye ule uzi mwingine nili-comment "... English inajenga confidence sana ..."; na ndicho kinachoshuhudiwa kwa huyo binti kwa sababu msingi wake wa Kiingereza ni mzuri hali iliyompa confidence of course along with her other personal traits. Angekuwa shule za Kiswahili, I believe, haki yake ingekuwa imepotea.
 
Ndio maana inafanya tuwe na baadhi ya Viongozi mbumbumbu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…