Ngazi za mishahara Serikalini - Tanzania (TGS, PHTS, PSS, SAIS etc)

Ngazi za mishahara Serikalini - Tanzania (TGS, PHTS, PSS, SAIS etc)

Kama ni freshy lakini.. ila kama ulikuwa na diploma hapohapo serikalini ukaenda kujiendeleza ukarudi na degree unakuwa E ila kama ni freshy unapewa D. Wanaconsider experience rather than your degree.

Na ukiomba ukapewa D alafu ukajiendeleza ukapata Masters unapewa ngapi?
 
Mishahara ya serikali inakatisha tamaa labda upate mashirika ya umma,Govt agency na taasisi nyinginezo. Vinginevyo ni pasua kichwa tu utaishia kuwa mdokozi tu wa pesa za umma.
 
Tgs d1 ni 567,000 tu

Wa juu ni tgs d12 ambao ni 693,500
 
Hivi wafanyakazi wa serikali wanaringa nini ? kumbe wengi m hawaijui ? sasa mbona wanatuletea giza ya foleni kwa vigari vyao vya mikopo ?
 
Mada yahusika-kumekuwa na swala la ngazi za mishahara ambalo watu wengi wamekuwa wakiulizia' hii ni kwa sababu waajiri wengi wanapotangazi ajira huwa hawaelezi ni kiasi gani kwa tarakimu mfano ngazi ya mshahara ni TGS D, A B C E n.k ombi langu wakuu kwa yeyote anayejua ngazi za mshahara serikalini atufahamishe hapa kuanzia na TGS A na kuendelea.

Naomba kuwasilisha hoja
 
Mada yahusika-kumekuwa na swala la ngazi za mishahara ambalo watu wengi wamekuwa wakiulizia' hii ni kwa sababu waajiri wengi wanapotangazi ajira huwa hawaelezi ni kiasi gani kwa tarakimu mfano ngazi ya mshahara ni TGS D...A B C E n.k ombi langu wakuu kwa yeyote anayejua ngazi za mshahara serikalini atufahamishe hapa kuanzia na TGS A na kuendelea....naomba kuwasilisha hoja

TGS A ni ndogo kuliko B na kuendelea! TGS J ni kubwa mno katika utumishi wa Umma Serikali kuu!
 
Tatizo umeweka kwenye Pdf...ungetuandikia moja kwa moja ingekuwa safi tunatumia Tecno mkuu...otherwise thanka for your contribution
Mkuu nikikuwekea the way unavyotaka hautaielewa...!! Ina majedwali na columns kibao...!!
 
Back
Top Bottom