Kwenye huu uzi msidanganyane... narudia, msidanganyane... hususani wale wa sekta binafsi msiwadanganye waliopo serikalini kwa kujionesha nyie mambo yenu huko ndo safi ile mbaya! Nina uzoefu wa sehemu zote mbili. Majority, narudia MAJORITY wa wale waliopo sekta binafsi ni afadhali hao waliopo serikalini!
Huko sekta binafsi ndo hatari tupu hususani kwenye hizi kampuni maarufu... unless uwe kwenye managerial position or at least supervisory level... but in most cases, huwezi kutoka na ki-degree chako huko ulikotoka na hapo hapo ukapata supervisory position! Kama ulisoma biashara, sana sana utaishia kuwa marketing or sales officer ambao wengi wao wala hainusi hiyo TGSD! Sana sana utaishia kuwa Customer Service Executive... kampuni nyingi utalipwa chini ya laki 6 with limited opportunity to adavance! Ukienda kwenye mabenki, kama hutakuwa Teller basi Loan Officer au Bank Officer... wote hao mshara wao wala haina tofauti na hiyo hapo juu with very few banks ndizo zipo above industrial level!
Ukienda Vodacom, Airtel, Tigo na Zantel, utaishia kurigishia t-shirt za kampuni ya simu tu... huku uswahilini watakuogopa kwamba jamaa anafanyia Voda lakini wanaofahamu watakuwa tu wanakusikitikia kijana mdogo unavyojishebedua wakati huna hela! Kwa mtu asiyefahamu anaweza kushangaa nikisema kwa mfano, kwenye kampuni za simu, Freelancers.... narudia FREELANCERS huwa wanakula mpunga mkubwa kwa mwez kuliko wafanyakazi wenyewe! Kama kuna aisyefahamu kuhusu Freelancers ni wale jamaa ambao ukienda kwenye kampuni za simu utawakuta pale nje wakisajili laini na mambo mengine kama hayo... trust me, wale jamaa wanachukua mpunga mkubwa kuliko walioko kwenye viyoyozi kule ndani!!
It's crazy lakini ukweli ndivyo ulivyo...