Ngazi za mishahara Serikalini - Tanzania (TGS, PHTS, PSS, SAIS etc)

Ngazi za mishahara Serikalini - Tanzania (TGS, PHTS, PSS, SAIS etc)

Naomba kuuliza kwa architects wakiajiliwa na serikali wanaanza na ngazi ipi ya mshahara na ni sawa na kiasi gani?
naomba mnijuze
 
Habari wana jf. naomba kujuzwa kwa anaejua ngazi za mishahara kwa maaskari magereza kuanzia mwenye elimu ya darasa la saba mpaka chuo kikuu. kama huna coments tulia kimya, sihitaji matusi.
 
Chuo kikuu, degree ya uchumi.
kweli siku hizi elimu haina mpango kabisa, yaani na digirii yako unataka kuwa polish, enzi zetu polisi ni darasa la saba tena waliofeli. Wanataka pilosi wenye digirii ya uchumi ili waende kulinda benki, we jaribu bahati yako
 
Viwango vya mshahara nimeviona lakini sijajua wale wa magereza wako upande gani. uwezekano wa kupata upo wakuu mie nilitaka kujua mshiko wao kwanza.
 
mhmhm sasa ukilinganisha na wengine kuna utofauti kweli au? mfano wale wahasibu, administatrators n.k ambao nao ni graduate/bachelor ? na wao si wanaanza na TGSD1 instead of TGTSD1, kifupi mie naona ngoma droo coz hata nao rate ni hiyo hiyo sema tu watu tuna kasumba ya kuwaponda walimu au kazi ya ualimu but salary level is almost the same, and sometimes walimu wana opportunity ya kutumia brain zao kuongeza kipato tofauti na wafanyakazi wa kawaida ambao toka saa 2 asubuhi hadi saa 9 na nusu yupo tu ofisini na dili hazisomi at the end of the month hana source nyingine zaidi ya kusubiri semina au workshop

Kwel uwezekano huo upo mkuu lkn kumbuka wahasibu wao wana semina nyingi sana,wanasaini vocha hewa kibao,inshort tofaut yao iko hiv mkuu mwl yy daily anashinda na wanafunzi na whole issues zinazohusu academic wkt muhasibu mostly yy ana deal na financial issues daily
 
TPGS 4 (mamlaka ya bandari-TPA) ni shlingi ngapi? kwa anayejua tafadhali.
 
hiviii wanavyosema tgs d1, 2, 3, 4,5n.k wanamaanisha nini hizo series 1.... Na kuendelea zina maana gani..ndugu yangu amepata kazi serekalini kaanbiwa mshahara ni tgs d nataka kumshauri aende huko atoke private..sasa hiyo c nayo naona ina mishahara tofauttofaut nashindwa kumuelekeza msaada tafadhali

hizo series kiserikali ni level of seniority with respect to salary scale,maana yake ni kwamba, anaeanza kazi leo kwa level husika ya mshahara mfano tgs d ikifika mwakani mwaka wa fedha wa serikali atapanda na kuwa tgsd2 na vivyo hivyo kila mwaka wa fedha anazidi kupanda hadi atakapopandishwa cheo kidaraja atakuwa tgse au zaidi kulingana na sifa iliyompelekea kupandishwa cheo.
Sasa basi kwa anaeanza kazi leo na bachelor kwa mfano,akamkuta mwenzie alieanza miaka ishirini iliyopita na astashahada yake kuna uwezekano mkubwa mfumo huu wa seniority level of experience ukambeba yule mwenye astashahada akawa ana mshahara mkubwa kuliko mwenye shahada.
 
WADAU HESHIMA KWENU KUNA KAZI ZINATOKA SERIKALINI AU KATIKA TAASISI MBALIMBALI, SASA UNAKUTA SEHEMU YA MSHAHARA WANAKWAMBIA UTAKUWA.,MFANO As per Treasury Registrar's Salaries Circular No.3 of 2014. ... TANZANIA etc, au
As per Treasury Registrar's Salaries Circular No.5 of 2014. ... sasa nauliza hiyo Circular ni ipi mwenye nayo tafadhali aiweke hapa itusaidie wote: Hiyo Circular No 5 ya mwaka 2014 ni TSH NGAPI BASIC/GROSS SALARY NDUGU WANA JF??
 
Wadau hakuna anaejua haya masuala jamani?? Naona mnapita kimya kimya au ni ishu ngeni sana wanajukwaaa??
 
Kwenye huu uzi msidanganyane... narudia, msidanganyane... hususani wale wa sekta binafsi msiwadanganye waliopo serikalini kwa kujionesha nyie mambo yenu huko ndo safi ile mbaya! Nina uzoefu wa sehemu zote mbili. Majority, narudia MAJORITY wa wale waliopo sekta binafsi ni afadhali hao waliopo serikalini!

Huko sekta binafsi ndo hatari tupu hususani kwenye hizi kampuni maarufu... unless uwe kwenye managerial position or at least supervisory level... but in most cases, huwezi kutoka na ki-degree chako huko ulikotoka na hapo hapo ukapata supervisory position! Kama ulisoma biashara, sana sana utaishia kuwa marketing or sales officer ambao wengi wao wala hainusi hiyo TGSD! Sana sana utaishia kuwa Customer Service Executive... kampuni nyingi utalipwa chini ya laki 6 with limited opportunity to adavance! Ukienda kwenye mabenki, kama hutakuwa Teller basi Loan Officer au Bank Officer... wote hao mshara wao wala haina tofauti na hiyo hapo juu with very few banks ndizo zipo above industrial level!

Ukienda Vodacom, Airtel, Tigo na Zantel, utaishia kurigishia t-shirt za kampuni ya simu tu... huku uswahilini watakuogopa kwamba jamaa anafanyia Voda lakini wanaofahamu watakuwa tu wanakusikitikia kijana mdogo unavyojishebedua wakati huna hela! Kwa mtu asiyefahamu anaweza kushangaa nikisema kwa mfano, kwenye kampuni za simu, Freelancers.... narudia FREELANCERS huwa wanakula mpunga mkubwa kwa mwez kuliko wafanyakazi wenyewe! Kama kuna aisyefahamu kuhusu Freelancers ni wale jamaa ambao ukienda kwenye kampuni za simu utawakuta pale nje wakisajili laini na mambo mengine kama hayo... trust me, wale jamaa wanachukua mpunga mkubwa kuliko walioko kwenye viyoyozi kule ndani!!

It's crazy lakini ukweli ndivyo ulivyo...
 
Ni mshahara wa Tshs 282,595.50

Hiyo ni take home au bado makato mengine?

Maana nikifikiria makato ya bodi,bima ya afya,nauli za daladala na gharama nyingine za maisha si nitabakiwa na 50,000
Kwa hali hii mwanangu atasoma English medium kweli?,na gari je nitanunua kweli?, mh na hela za kwenda vacation Dah,NIMESHINDWa!
 
Wanandugu naombeni kujua majukumu ya mkaguzi wa mji msaidizi kazi zake pia TGPSW1 ni sh ngap?
 
Back
Top Bottom