Ngazi za mishahara Serikalini - Tanzania (TGS, PHTS, PSS, SAIS etc)

Ngazi za mishahara Serikalini - Tanzania (TGS, PHTS, PSS, SAIS etc)

Thanks wakuu,nimeona zile kazi ambazo zimetangazwa na serikali, nyingi kwenye mshahara zinaeleza habari TGS,ikawa inanitatiza.
 
Serikalini mshahara si mkubwa. Mishahara mikubwa kidogo ni kuanzia TGS H-M. Ila nakumbuka kama L na M ni fixed i.e no more annua increments ila ni kama kila 2 na zaidi. Ila kwa H-K sina hakika kama imefika kilo 2.
 
kuna mfanyakzi wa serekali alinimbia juzi ukiona grade a,b,c na wengineo wamwanzo mwanzo mshara ni mdogo ila ziki panda e ,f,g,h ndio zina anza kuuwa mkubwa
 
hata mimi huwa inanitatiza sana.hivi tgs c ni kiasi gani na yenyewe,mimim nimesomea diploma ya uhasibu kwa hivyo viwango nitaangukiwa grade ipi.
 
tgsd laki 4 na nusu, ila utakatwa katwa utakachopewa ni aibu,tgse laki 8 na arobain elfu
 
Naombeni msaada kwa anaejua viwango vya mishahara hapa tz
yaan unakuta umeandikiwa TGS.D
au Tgs E,
hz mm zinanichanganya sana naomba kujulishwa kila Tgs na mshahara wake msaada plz
 
NImesoma post zote mwanzo mwisho, Ukweli ni kwamba mshahara wa mawilimu mwenye degree ni mdogo sana, na roho inauma sana, hata kama una GPA kubwa. kuna madaktari wana GPA ndogo sana lakini utakuta wanachukua mshahara mnono.

Ushauri wangu ndugu, Usiukatae ualimu kama huna altenative- nenda kadake hizo hizo, huku ukifikilia otherwise. Vijana wengi wana tabia ya kuponda ualimu huku wakikaa kwa kaka zao, shemeji zao au dada zao. Hiyo nimmbyaya sana.

Tafiti zinaonyesha kuwa, hapa bongo Walimu wanaongoza kwa kuhama field ya ualimu. Kwa hiyo isikupe shida kuanza na hiyo 350,000/= we kaichukue hiyo kazi jipange uangalie utakavyotoka. Walimu wanachomoka sana. Ila tahadhali ukienda kuanza kazi ukapewa ka cheo ukalala itakula kwako.
Ualimu isiache kama huna pa kuanzia.

ushauri mzuri sana mkuu
 
320,000.00 ukigawa kwa 30 ni sawa na 10,700/= tshs kwa siku!
Hivi pesa hii mtu akijipanga kufanya kilimo cha umwagiliaji wa pampu tu ya kawaida akitumia maji ya mto wa kudumu hawezi kupata hata 500,000 kwa mwezi?

Nauliza tu, i stand to be corrected!

kila kitu kinachangamoto zake, lakini cha muhimu mhusika kuzikubali. Tatizo kubwa ni kipindi kisichopungua miezi 3 ndipo uanze kupata hicho kipato je unajipangaje
 
kila kitu kinachangamoto zake, lakini cha muhimu mhusika kuzikubali. Tatizo kubwa ni kipindi kisichopungua miezi 3 ndipo uanze kupata hicho kipato je unajipangaje

nalo neno
 
320,000.00 ukigawa kwa 30 ni sawa na 10,700/= Tshs kwa siku!
Hivi pesa hii mtu akijipanga kufanya kilimo cha umwagiliaji wa pampu tu ya kawaida akitumia maji ya mto wa kudumu hawezi kupata hata 500,000 kwa mwezi?

Nauliza tu, I stand to be corrected!

Sasa Kodi ya chumba kimoja kwa wamjini katika miji mikubwa tz ni 30,000/ bei ya chini umeme 10,000/= maji 5000/= usafiri sh 1200/= kwa siku plus mahitaji binafsi mf chakula, mavazi na ukiweka na kukaa bar unaishia patupu
 
HEBU TIZAMA TOFAUTISHA YA KUTISHA YA VIWANGO VYA MISHAHARA MIPYA
KWA WATUMISHI WA UMMA TANZANIA:

Ngazi ya Cheti:
Mwalimu 244, 400/
Afya 472,000/
Kilimo/Mifugo 959,400/
Sheria 630,000/
Ngazi ya Diplomma
Mwalimu 325,700/
Afya 682,000/
Kilimo/Mifugo 1,133,600/
Sheria 871,500/
Ngazi ya degree
Mwalimu 469,200/
Afya 802,200/
Kilimo/Mifugo 1,534,000/
Sheria 1,166,000/

angakia hapo penye italics na bold
 
Mkuu hii calculation ukiyoiweka ni sahihi kweli? maana hizo percentage ulizoweka makato yake yanafika sh 122591
Gross Salary 422,730.00
14% Tax 59,182.20
8% NHIF 33,818.40
5% pension 21,136.50
2% CWT 8,454.60


Take home salary= 300,138.30

Mkuu nadhani utakuwa umekosea kidogo ktk hisabati zako. Usitafute asilimia ya Tax kabla ya kutoa % ya Pension.
nadhani itakuwa kama ifuatavyo:-

Gross salary 422,730.00
5% pension 21,136.50
8% NHIF 32,127.48
14% Tax 51,725.2428
2% CWT 6,354.82

Take home salary= 311,385.96
 
Serikalini hii grade ya mshahara inaanzia kiasi gani? Just Salary Scale 6.1

My Regard!!
 
Back
Top Bottom