Ngorongoro - Loliondo: Askari Polisi amekufa baada ya kupigwa Mshale mmoja tu, RC Mongella amlilia

Amekufaje wakati Kassim alisema bungeni hakuna mapigano?
Hii taarifa ni ya kichonganishi na ya kichochezi. Jana mzee baba mr.Prime Minister majaliwa alisema hali ni shwari na mama tulia akasema mijeledi iende kwa wazushi sasa huyu askari amekufaje au alikamatwa na simba wkt analinda simba wasiingie kwenye makazi ya watu
 
Aridhi yote Tanzania ni mali ya serikali inauwezo wa kuipangia matumizi yoyote kwa mda wowote, labda mbadili katiba iondowe hicho kipengere
WAPI pameandikwa ardhi ni mali ya serikali we mjomba ?
 
PM na Tulia hawa wote ni Masalia ya JPM waongo na waficha ukweli
 
Kuna watu wanamchafua majaaliwa mchana kweupe akose sifa za kugombea uraisi 2025, nishastuka. .
 
Huyu Mongela hajui kuwa issue ya Ngorongoro ndo inaondoka na Ukuu wa Mkoa wake Serikali itakapojikosha!!!
 
Wamaasai walijaribu kumzuia wakati askari wanafanya kazi yao
 
TUNDU LISSU ATOA HISTORIA YA MAENEO TENGEFU NA HIFADHI ZA TAIFA LOLIONDO, BUNGE LATIKISIKA DODOMA

Tundu Lissu anaelezea historia ndefu na kunukuu andiko la Prof. Issa Shivji na Dr. W.B Kapinga juu ya Haki za wa Masai pamoja na wenyeji wa Maswa, Bunda n.k ambapo hidhafi za wanyama / maeneo tengefu yapo kupitia utafiti wao wa kina na andiko hilo kuchapishwa na kunukuliwa katika vyuo vikuu mbalimbali vya dunia kuhusu haki za wenyeji



Serikali juzi ilisema kule Kagera kuwa waTanzania wanazaana sana na ardhi inaendelea kuwa chache,
Mh. Rais akizungumza kuhusu idadi ya watu akuwa ziarani Kagera, Tanzania 10 Juni 2022

je ni kweli unaweza kuhamisha mamia ya watu toka sehemu moja ya Tanzania na mifugo yao ya kienyeji kwenda sehemu nyingine ya Tanzania bila madhara ya mapigano ya kugombania rasilimali ardhi ?

Nini kifanyike kwa muda mrefu ili kuweza kufanikisha serikali ifikie malengo yake bila kuleta athari za wananchi pamoja na watekelezaji kama askari kuumizwa au hata kupoteza maisha ?

Hiki kinachoendelea Ngorongoro, Loliondo, Geita, Kagera, Morogoro, Handeni, Mtwara, Lindi, Kigoma n.k kwa wananchi kuona hakuna ardhi ya kutosha serikali ichukue hatua gani ?

Kampeni za social re-engineering: yaani uzazi wa mpango, kilimo cha kisasa, ufugaji wa kisasa, uvuvi wa kisasa, mfumo wa maisha za jamii zote za Tanzania zinabidi kuanza sasa kwa serikali kuanzisha mpango mkakati na fedha ili kukabiliana na hali hii ya kugombania ardhi.

Kwa serikali kuwa na mpango wa muda mrefu wa social re- engineering yaani kiibadilisha jamii yote ya kiTanzania kupitia mambo hayo hapo juu itafanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza ukuaji mkubwa wa idadi ya watu, wananchi watabadilisha mifumo yao ya maisha, watazalisha kwa wingi mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na kushiriki katika ajira nyingi zaidi za viwandani pia katika sekta za huduma n.k

Hatua hizi zitaondoa makundi makubwa ya wamachinga, wafugaji wa kienyeji, wakulima wa kijima (jembe la mkono), wavuvi wanaovua samaki kizamani ktk kina kidogo cha maji , wazurulaji waliozagaa mijini (panya road) n.k ambao katika ujumla wao ni "bomu la kijamii" linalotaka kulipuka muda siyo mrefu na dalili zake tayari tunaziona.

 
Ni Africa tu ndipo ambapo unaweza kukuta migogoro ya ardhi,hili bara lina laana
 
Mara nyingi nikissikia idadi ya Askari wa marekani walio uliwa huko arabuni hata mmoja tuu waga napata hofu sana kuhusu idadi ya waarabu waliouliwa
 
Wamasai wanafikiri wanaweza shindana na serikali!???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…