Ngorongoro - Loliondo: Askari Polisi amekufa baada ya kupigwa Mshale mmoja tu, RC Mongella amlilia

Ngoja tuwasubiri wabunge wanaowatetea hao wananchi nao wanasemaje
 
Waziri mkuu anahabarishwa tu kinachoendelea. Hawezi danganya tu wakati anajua tuko kwenye dunia ya kidigitali, ukweli haufichiki sasa, sio mirahisi kihivyo. .
Aliyemwambia kwenda kudanganya msikitini wakati mwendazake alikuwa ameshakufa kitambo leo anaenda kudanganya Bungeni wakati uhalisia unaendelea.
 
Your browser is not able to display this video.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella akizungumzia kwa uchungu tukio la kuuawa kwa Askari Polisi siku ya jana Juni 10, 2022 na kikundi cha Watu wanaopinga zoezi la usimikaji wa bikoni katika eneo la Pori Tengefu la Loliondo.
 
Ni nini kinawafanya masai wakaidi kutoka ngorongoro? hawajaliowa fidia au ni kiburi?
 
Si tumeambiwa huko ni salama tupu na Mhe Waziri mkuu? imekuwaje tena
 
Ni nini kinawafanya masai wakaidi kutoka ngorongoro? hawajaliowa fidia au ni kiburi?
Kwani kati ya Wamasai (wenyeji wa hilo eneo), wanyama na Waarab! Nani wenye haki ya kuishi hilo eneo?
 
Mmasai Putin kasawazisha katika dimba la Loliondo mpaka sasa ni 1-1 ingawa refa (mpaka piko) anapendelea upande mmoja
 
Tulitoka kwenye adha ya muda mrwfu ya COVID-19 ba utalii ukadorora ile mbaya
Vikafuata vita vya Ukraine, mafuta na vitu vikapanda bei. Sasa serikali kwa ubabe wanaturudisha tena kwenye vita na kuwafukuzia watalii Lenya
God help us
 
Kwa tunavyowajua polisi, kwa hili lililotokea hao raia watachapika sana.
 
Masai hatibiwi hospital[emoji23][emoji23]
 
Kama ni mshale hao sio wamasai, lazima watakuwa ni Wasonjo. Na hii inaonyesha kwamba Wasonjo na Wamasai wanakula sahani moja, meza moja, kiko kimoja kwenue hili sakata
 
Tukubali tu kumtoa mmasai Ngorongoro ni sawa na kumtoa nyati Ngorongoro au tembo.
Mmasai ni moja ya kivutio cha utalii miaka na miaka toka enzi .
Kwa hili serikali kwa mimi inakosea
 
Hawa jamaa wanaleta siasa kwenye mambo yenye madhara makubwa kwa Taifa! Mara hao Wamasai wanatoka nchi jirani! Mara hakuna aliyejeruhuwa! Mara picha ni za miaka 3 iliyopita!

Yaani siasa na propaganda kila sehemu!
Hawaeleweki yani kila kiongozi anapanua mdomo. Unaweza Dhani haya mambo yanafanywa na chokola aliyevuta ngada kumbe ni kiongozi mkubwa ila akili yake haitaki unafiki inajionyesha waziwazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…