Nguvu nilizowekeza kwenye ujana wangu nakula Matunda yake sasa

Shukran mjukuu, [emoji114]
Kubaliana na upinzani humu JF maana wengine tayari wameshachelewa kwa kutokuwa na uwekezaji mzuri kama wewe, pia wengine ni Waathirika wa afya kwa magonjwa ya kisasa na madawa ya kulevya.

Hongera sana Mzee Baba [emoji1666][emoji122]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Hongera Sana kwa ushauri mzuri baba.
Kwa kuongezea ujana ndio unapredict future yako iweje kiuchumi, kiafya n.k.
Afya ni muhimu mno kwenye ustawi wa mengineyo. Vijana wengi hawajali afya zao sijui ni kujisahau au kutokujua na wengi wanajitetea wakisema kufa kupo pape pale (yes sipingi) ila ni muhimu kuzijali afya zetu
 
Shukran mkuu, nafahamu hili ni jukwaa huru, hivyo kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo yao,

Mimi sina shida na hilo maana maneno hayani punguzii chochote kile,

Atakayeona ni uongo sawa atakayeona ni kweli sawa pia
 
Kabisa, na mimi nilizingatia pia nisi nenepe

Maana hamnaga unene wenye afya na namshukuru Mungu afya yangu ipo vizuri kabisa ila kuumwa kwa hapa na pale kumo pia

Shukran mkuu 👐
 
..Ulizaliwa 1953, ilitakiwa Ustaafu Kwa LAZIMA Kwa Mujibu wa Sheria, Mwaka 2013 !!
Vipi Ukastaafu 2016, Miaka 3 baadaye! Vipi, ulifoji ? Tuanzie Hapo kwanza....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…