Nguvu ya Umma Senegal, funzo jingine kwetu

Nijihisi kusemwa na nani mjomba? Kazi kweli kweli.

Ukweli wa mambo ni kuwa, kwamba Dkt. Ndumbaro kasema watanzania wanataka Katiba mpya:

"ni kupoteza muda kuwaelimisha kuhusu umuhimu wa Katiba mpya walamba asali, wahuni au wale vijana wa hovyo."

Zaidi sana kutokea hapo:

1. Ni uzezeta kudhani Samia angependa katiba mpya ipatikane kabla ya 2024.
2. Ni uzwazwa mwingine kudhani kuwa atakuwa na nia ya kutupa katiba mpya kama tunavyoitaka kwa content na wakati asiokuwa na manufaa nao.
3. Ushawishi wa kutosha unahitajika kumfanya kuridhia matakwa yetu. Hili linawezekana.

Jukwaa hili ni huru for which you are entitled to your own opinion.

"Bwana Uzima Tele, denooJ, makaveli10 wajumbe wengine tusaidiane kuwajuza pedals za brake, clutch na accelerator zilipo."

Kwamba wao nao ni wapigania katiba mpya kwa namna isiyojulikana.

Kazi kweli kweli.

Si utuwekee mkuu ya kwako iliyokuwa elaborate kweli kweli? Kwani umezuiliwa kuandika uzi wako ulioshiba?

Makasiriko yote ya nini ndugu usiku usiku huu?

Hiiiiiii bagosha!
 
Enough of this.
I have stated what I needed to state. It's your choice, reflect on it or simply ignore.

I see no specific issue here that requires my direct response.
 
Acha kuwapamba pamba hawa wasenegalizi wako. ni vibaraka wa Saudi Arabia wakubwa. halafu kwa haibu mbaya nchi ya senegal ni mwanachama wa the Arab League. Yaani wanajiita black arabs. hapa africa continent nchi za senegal, mali, somalia, SudanNigea,, Chad na gambia hujiona wanachama wa the arab league!huu ni upuuzi mtupu na vibaraka wa saudis!
 
Anza basi kushika bango wewe na familia yako kuhamasisha wengine!
Hivi lizione uwa unamatatizo gani,yaani kwa vile wewe na mama yako mpo Bungeni mnakula tu mishahara mikubwa na posho kila siku haujui shida yoyote ndo utuandikie ujinga wako humu?
 
kwetu itachukua muda kidogo labda miaka 30 ijayo, pale mazombie yatakapoisha kwa kufa yenyewe, au kwa miujiza
Hapana mkuu hata huko yanakotokea sasa mazombie pia wapo. Anasema Museveni, "maendeleo ya Uganda hayawezi kusubiri wakaramojong wajue kuvaa suruali."

Jukumu hili ni letu mbona tunatosha sana? Angalia Kenya au hapo Senegali kwani palikuwa na "wakoma" wangapi waliowafurusha "washami?'

Nyomi hizi:



Hazina watu 1,000. Raila hakukamatwa kwa sababu ya nyomi hizi. Unasema CDM yenye watu 8m + ilikosa watu hapo watu 1,000 wasio mazombie kuzuia kina Mbowe kukamatwa?

Kwamba hata huko CDM wote ni mazombie? Kumbe mazombie watakuwa nani basi?

Organization.

Yawezekana matatizo yetu yako hapo. Nyani haoni kundule tunazo sababu za kujihoji internally.
 
Siyo Tabia nzuri kujifanya msemaji wa kila kitu siyo nidhamu
 
Uzima Tele nimekupata na hoja yako inayonitaka nilianzishe peke yangu wengine mfuate..

Hivi, kwanini mnisubiri nilianzishe peke yangu ili nanyi mnifuate? kwamba ndio tuseme bado mmelala mnasubiri mpaka nitakapolianzisha ndipo nanyi mtaamka?

Hebu tutazame mifano iliyoletwa na mleta mada au mingine ambayo tumekuwa tukiishuhudia mara kwa mara maeneo tofauti; anzia na Kenya, nenda hapo Senegal, tusogee kule North kwenye ile Arab Spring ya wakati ule...
hivi huko kote ni nani aliyelianzisha akawapeleka watu barabarani kuwatoa vyumbani kwao?

Hii mambo ya kusubiri fulani alianzishe kwangu naona ni usanii tu, tunategana, kwasababu naamini kabisa, deep inside, hata wakina nyie mnaosubiri wengine waamke nanyi pia mnajua vizuri mnatakiwa kulianzisha, tatizo sijui mnachosubiri ni kitu gani...

Ndio maana kule juu nikasema hili ni taifa teule la wanakondoo, wasio na tofauti na marehemu..
 
Mwanzo umeandika ukidai hujui hiyo nyomi ina malengo yapi, hivyo unadai unamuona mleta mada ana maneno mengi yasiyoeleweka...

Ajabu chini unamzungumzia Sall unayedai ana malengo yake, sasa kama umeshajua hayo, palikuwa na haja ipi kuanza kwa kudai hujaelewa "maneno mengi" ya mleta mada?

Kama kweli ulikuwa hujaelewa, ungetakiwa umuache akufafanulie kwanza ndipo uanze kujadili, lakini kujadili kwa kirefu kitu ambacho unadai hukukielewa mwanzo naona hilo ni tatizo lako na sio vinginevyo..
 
Nyie kila siku mnajifunza tu!
Ni kwa sababu wanaojifunza si katika wale wanaotarajiwa kufanya kwa vitendo hayo mafunzo ndio maana inabaki hivyo hivyo kuwa wao kila siku wanajifunza tu, humu JF tu sidhani kama kuna member hata mmoja katika hao wanaojifunza ambaye anaweza kuwa na dhamira ya kuingia road yani ni watu ambao wanatamani kuona ikitokea kama Kenya au huko kwengineko ila wao wakiwa hapa hapa JF wakifuatilia matukio huku wakiendelea na mijadala kwamba huo ndio uhusika wao au mchango wao kwenye mabadiliko.
 
Ungekuwa unajua vizuri historia ya siasa za Senegal ungelijua ya Kwamba Mark Sall aliyevurumishwa alikuwa ndiye Mpinzani Namba Moja Senegal (tuseme kama Mbowe na Chadema yake hapa Tanzania). Baada ya kuupata Urais kwa kumuondoa Abdoulaye Wade akanogewa na asali (Ahahahahaha, asali) hadi kutaka kuchonga mzinga!

Tafsiri ya Senegal ni Kwamba tusiwaamini wapinzani hata kidogo. Bora kubaki na CCM yetu na wapinzani kuambulia viti viwili vitatu vya ubunge na udiwani! Ahahahahaha!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…