Hapa Naona kizunguzungu tu.
Rais akiwa Arusha anasema alizungumza na Lema na kumwambia kwamba asihofu arudi nyumbani atamfutia kesi zake.
Jambo hili linashangaza mno.
Mosi, Rais anapata wapi mamlaka ya kuingilia mhimili mwingine?
Haoni kwamba anavunja katiba hadharani?
Tunaposoma katiba tunaona kwamba Mahakama ni mamlaka inayojitegemea.
Yeye nguvu za kuingilia Mamlaka nyingine anazitoa wapi?
Ukiachana na hilo.
Lema ni mpinzani. Yeye ni Chama tawala.
Chukulia mfano wa mtoto na mtoto wa jirani.
Yaani inakuwaje mama anaacha wanawe wanalia njaa halafu anapeleka chakula kwa watoto wa jirani.
Huyu atakua mzazi wa aina gani?
Rais yupo tayari kufuta kesi ya Lema hata kwa kuvunja katiba lakini hayupo tayari kuvunja katiba kwa kufuta kesi ya Sabaya ambaye ni mwanachama wake.
Upendo wa mashaka huu. Au tuuiteje.
Maana Logically it doesn't make sense at all.