Ni aibu kuwa na taifa ambalo Rais wake anaingilia Mhimili wa Mahakama na anajinasibu kufutia wakosaji makosa kinyume na katiba

Kama mwizi wa gari mstaafu anasamehewa hata huyo mhalifu anastahili.

Huu ni mwezi wa kwaresma.

Rais atoe zawadi kwa kumfutia kesi sabaya atapata thawabu.

Else itakua hadaa tu kama nyingine tulizozoea kusikia na kuona.
Kwanini amfutie kesi Sabaya peke yake kama kigezo ni mwezi wa Kwaresma? Vipi kuhusu waporaji na majambazi wengine wa silaha walioko mahabusu? Basi kuwa fair wale wote wenye kesi za ujambazi wa silaha waachiwe kama Sabaya anastahili kuachiwa kwa sababu ya kuwa ni mwezi wa Kwaresma.
 
Nimeamini wapenzi
Wa CCM humu mnaandika kwa mihemko tuu na sio kwa kutumia akili.
Kumfutia mtu kesi mahakamani sio kuingilia muhimili wa mahakama kwani mahakama haina kesi na mtu yenyewe ni maamuzi ya kesi iliyoletwa na DPP au hata wewe mtu binafsi.
DPP na vyombo vyake vya uchunguzi yaani Polisi, Takukuru, uhamiaji hata TRA ndio wenye kesi na hao wanaweza hata kumbambikia kesi raia yeyote yule.
Vyombo vyote hivyo viko chini ya Executive na hiyo ni mamlaka ya Rais. Hivi akigundua kumbe maafisa wangu au mtangulizi wangu alitenda uovu kubambika kesi ni kosa kuondoa kesi? Hapana.
Kesi za Sabaya kajiridhisha kuwa sio za kubambikwa wala siasa ni za jinai na sheria haibagui mtu anaacha mahakama itende haki.
Kwa hiyo kwa Lema ameondoa kesi zao na sio kuingilia mahakama.
 
Sidhani kama kuna mahali Samia katamka "kusamehe", navyojua kasema kufuta kesi.
 
Sabaya miaka 34 tu anaozea jela bila sababu za msingi lakini tuliwaambia wakae mbali na uharifu wao wakakataa kata kata.
 
Ni Magufuli tu ndio alikuwa na uthubutu wa kusamehe wabakaji.

Mama hawezi kuitwa msamaha kwa majambazi kama Sabaya.
 
Msamaha wa raisi uwa unakiwango chake
 
Akifuta kesi ya Sabaya watasema anaingilia uhuru wa mahakama.

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].
 
Kumtetea Sabaya inabidi usiwe na akili timamu kama mleta mada. Sabaya ni shetani katika mwili wa binadamu. Hafai kutetewa na mpenda amani yeyote. Makonda, Gambo, Mnyeti, Biswalo na Ally Hapi walipaswa wawe magerezani muda huu.
Acha ujinga, subiri kwanza mahakama idhibitishe.
 
Mleta mada, kwani ni lini ulimpongeza mh raisi kwa jema lolote alolifanya. Ni hivi, Kwa katiba hii, raisi anamamlaka hiyo hata kama siyo direct itakuwa indirect. Hukuwahi kumskia marehemu Magu akisema "Kuna mihimili mitatu, lakini mhimili mmoja (yeye/serikali) umejichimbia chini zaidi ya mihimili mingine" mwisho wa kunukuu. Huyo Sabaya hakuwaumiza wapinzani tu, hata wana ccm walilizwa. Na rais kwa kuwa ni raisi anayajua maovu ya sabaya kuliko wewe. Acha raisi afanye atakalo. Na uungane na wanaodai katiba mpya.
 
Sabaya ni jambazi
 
Huu sio upendo kama Lema amesahewa kwann sio Sabaya ubaguzi ni Dhabi kubwa Sawa .Amini nakuambia Rais wetu Mama Dr.Samia atamsamehe na Sabaya Mama ni mwenye hekima sana.
Sasa kama mnajua atasamehewa haraka ya nini? Kila jambo hufanyika kwa wakati wake. Subiri yavuta kheri
 
KWANI MAKOSA YA LEMA NA SABAYA YANAFANANA?
 
Mimi nadhani Mh. Rais amezingatia gravity (uzito) wa kesi zenyewe.

Tuhuma za Sabaya ni nzito ukilinganisha na zile za Lema ambazo ni purely kesi za kisiasa.

Pamoja na kusema haya, haimaanishi nahalalisha kitendo cha Rais kufuta kesi, sijui ametumia Sheria gani inayompa mamlaka ya kuingilia mhimili mwingine wa Mahakama huku wakituaminisha kwamba mihili hiyo iko huru kutimiza majukumu yake bila kuingiliana.

Mwl Nyerere aliwahi kusema kwamba kwa Katiba tuliyonayo angeweza hata kuwa diktekta, huu ni ukweli mchungu.

Rasimu ya Warioba irudi mezani iwe Katiba mpya, period.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…