Ni changamoto zipi umewahi kupitia ukiwa katika hali ya umasikini?

Kwa waliozoea hiki ni chakula kitamu sana hiki ila ukiwa hujazoea ni shiida.
 
Hawa wageni na ukiacha hayo hawa jamaa wanatabia za kinyonga
 
Nilikuwa nakaa Mabibo- home hali ilikuwa mbaya sanaa

Nikitoka shule
Nilikuwa naenda hapo mahakama ya ndizi naokota ndizi mchanganyiko mbichi na mbivu narudi nazo nyumbani na lundo la ndizi mama anapika ndio tunakula familia nzima yaani familia ilikuwa inaniona kama vilee ndio mkombozi wao Kwa ndizi za kuokota kila siku lazima niende zangu kindo kuokota ndizi

Umenifanya nilie Kwa kukumbuka hii inshu- nilikuwa mdogo sanaa lakini situation ya home niliijua yote so nililazimika kufanya vitu juu ya uwezo wangu

Nashukuru Kwa hali zote- alhamdullillah
 
Samahani mkuu hakikisha unamkumbusha kauli yake ili aombe radhi usilee ujinga
 
Niliwahi kwenda kwa kaka Dar es Salam kumsalimia nkakaa miezi miwili nkaona hana moyo wa kunisapoti mimi mdogo wake ntoke kimaisha ikabidi nitoroke kwake nikatafute maisha yangu....."nilipitia mengi mno sitaki tena niyapitie tena yale niliyopitia, sitaki mwenyezi Mungu anisaidie mimi na wewe unayesoma ujumbe huuu"

NOW, najitegemea nisingetoka kwa kaka nisingekuwa hapa nilipo.!
 
Heeee nyie mmetokea wapi mbona wanajf hatupo hivo
Wew achana na nyie wakishua ambao mmekulia maisha mazuri hamuzijui shida wala umasikini.

Jf wengi wanaFake maisha lkn kwa Ground ukweli mnaujua[emoji23].

Mim nakumbuka niliwai pigwa na maisha mpaka nikafanya kama alichokifanya mtoa mada yaan kusachi nguo nikaambulia vumbi tupu[emoji23][emoji23], kiufupi niliambulia patupu kwa hasira nilizikusanya nguo zote nikawabeep washikaji waje wajichagulie kwa bei nafuu, maajabu na washikaji nao walipokuja wakaishia kunikopa nikaambulia buku3 ya kula siku moja.

Nishawai shindia pipi ivory na maji mengii siku nzima mpaka ukitembea tumbo linanguruma ule mlio wa maji kujaa tumbonii[emoji23][emoji23].

Shaenda mpaka kwa sangoma aloge nipate pesa kibahati nilipe madeni ya watu lakin mjinga yule nae akaanza masharti ya kijinga huyo nikatimka[emoji23][emoji23]

Kiufupi ukiwa ktk kipind kigumu kuna njia unazoamini zitasaidia kujikwamua lkn maajabu hizo njia ndio zinakuzamisha ktk mateso zaidi[emoji23].

JF watu wakiacha kuigiza maisha na kueleza uhalisia wao watasaidika humu kuna wengi tu wana Roho nzuri za kusaidia hata mimi kwa niliyoyapitia sipendi kuona mwingine anayapitia, lkn kwa hii Trend ya wanaJF kufake maisha basi acha wote tuonekane tuna magari na manyumba.
 
Huyo mwamba na shem kamwe usiwasahau maishani

wakumbuke tuu hata kwa maombi 🤔
 
Niliwahi shinda na kulala na njaa mimi wife na mtoto wangu wa kiume.

Nilimwaga machozi usiku ule kimyakimya huku wife hajui, asubuhi nikaamka 12 kamili kucheki vibarua vya kubeba zege (Mind you nina degree ya Geology na nilishawahi fanya kazi kwenye kampuni kadhaa ila wakati huo nikawa sina ajira na vyanzo vya mapato vyote vilifilisika).

Na sikuambulia kibarua mpaka inafika saa 5 asubuhi hapo mwili unatetemeka balaaa, wife akanitumia sms kuwa kakopa chapati 6 kwenye mgahawa nije nile nishushie na maji nisije nikazimia mbele za watu.

SITOSAHAU

Nitakuja na kisa changu namna nilijifanya mganga wa kienyeji ili nimpige dada mmoja wa kichaga 600,000 ili nipate kodi, kula na kadhalika. MUNGU ANISAMEHE SANA.
 
Mkuu watu kama hao ni wachache sana dunia hii....
 
Niliwahi kuamka na 150tsh na unga 1/8 na madeni maduka yote mtaani, nina mke na mtoto. Wife anauliza tutafanyaje, namwambia usiwe na wasiwasi tutakula tu.

Hatukuwahi kulala njaa, licha ya kutembelea kwenye chaki karibu mwaka mzima. Mungu yupo. Tumtegemeeni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…