Muungano hautovunjika bali unaweza ukaboreshwa !! Let say kama Rasimu ya katiba ya Mzee Warioba ilivyopendekeza !! Serikali tatu ! Au vipi ??!Sio muda naweka hathari hasi na chanya zitakazotokea pindi Muungano ukivunjika.
Mkuu Kilewella are you serious? Hivi hujui kweli kwamba Rais wa JMT ana madaraka gani? Au ndo choyo? Kule Zanzibar kuna ofisi za BOT, Uhamiaji, Posta, simu na nyingine. Hizi zinatambulika ni ardhi gani? Hemu tuwe serious wakati wa kutoa michango hapa JF. Wenyewe wanasema JF home of great thinkers. Tuchangie tukitilia maanani hili.Kwa nini inatamaniwa Rais wa JMT ajengewe Ikulu mahali ambapo hana uwezo hata wa kuteua Mkuu wa wilaya. Huoni Ikulu ya JMT inakwenda kujengwa kwenye eneo ambalo Rais wa JMT hana mamlaka nako?
Hiyo Ardhi itakuwa ni ya JMT ama itakuwa ya SMZ na itatambulikaje kisheria, ni ardhi ya nchi ya kigeni kama zilivyo Ardhi wanazopewa mabalozi wa nchi za nje Tanzania kujenga ofisi zao ama itatambulikaje?
Kwanza nitangulie kwa hoja yako ya mwisho kwamba ni wazanzibari ndiyo wanatakiwa waulizwe kama wanautaka Muungao ama la. Kwa mujibu wa Mwalimu (na ndiyo mtizamo wangu pia) kwenye kitabu chake cha "Uongozi wetu na hatima ya Tanzania" alishangaa ni kwa nini viongozi wa CCM wanashindwaje kuwauliza Wazanzibari swali rahisi kama hilo.. Ninachouliza ni athari gani mnaziziona?
Wazanzibar waulizwe kama wanataka muungano au la!
Mtanganyika asiulizwe haimhusu wala haathiriki na chochote au lolote lile ukivunjika.
Kama kweli zinajengwa ofisi za Ikulu , VP na PM huo ni upotevu wa pesa za umma mkubwa, na unaongeza gharama za kuhudumia ofisi kwa Mtanganyika anayeumia na tozo sasa hivi.Mkuu Kilewella are you serious? Hivi hujui kweli kwamba Rais wa JMT ana madaraka gani? Au ndo choyo? Kule Zanzibar kuna ofisi za BOT, Uhamiaji, Posta, simu na nyingine. Hizi zinatambulika ni ardhi gani? Hemu tuwe serious wakati wa kutoa michango hapa JF. Wenyewe wanasema JF home of great thinkers. Tuchangie tukitilia maanani hili.
CC: brazaj
Bado huelewi! Ofisi ya VP ilianzwa wakati wa JK na kumalizwa wakati wa JPM.Kumbuka Nyerere, Mwinyi, Mkapa, JK , JPM hakuna aliyefikiria wazo la hovyo kama hilo. Walijua Waziri mkuu wa Tanzania hahitaji ofisi mahali asipokuwa na kazi napo.
Bado huelewi! Ofisi hizi ni za JMT ambayo Zanzibar ina haki sawa na Tanganyika kwani nchi hizi ndizo ziliungana kuunda JMT. Ikiwa ni sawa kuwa na Ofisi Dar na Dodoma kwanini isiwe sawa kuwa na Ofisi ndogo Zanzibar? Gharama hizi zote zinatoka JMT ambapo Zanzibar ni mshirika wa Tanganyika ISIYOKUWEPO.Huu ni uharibifu mkubwa sana wa pesa, hatuhitaji ofisi hizo Zbar kwa hoja yoyote isipokuwa uharibifu na matumizi mabaya ya resources bila kujali anayebeba gharama hizi ni Mtanganyika peke yake si Mzanzibar.
nop kuna tanzania na zanzibar,
nilisafiri nje nchi flani nikakuta kuna chama cha diasporas cha watanzania na pia kuna chama cha wanzanzibar.
Hawa wanzanzibar hawapo kabisa kwenye. chama cha watanzania ilhali pasport wanazotumia ni sawa zote za jamhuri ya muungano wa Tanzania. Na pia wamejiandikisha kwenye ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Nikajaribu kuwadodosa watanzania wezangu mbona mmejitenga?
Wakanijibu Wazanzibari ni wabaguzi sana hata kule hawajitambulishi kama watanzania wanajitambulisha ni Wazanzibari.
Kwa kifupi kuna tatizo kubwa sana watawala wamelifumbia macho.
Ila ujinga huu aliutaka Mzee wetu RIP JK Nyerere.
The same kwenye ishu ya ardhi wao wao huku wanamilikishwa ardhi sawasawa kama watanzania wa bara ila mtanzania wa bara kwa zanzibar haiwezekani sanasana atakodishiwa kama mwekezaji mgeni rejeeni clip Askofu Mkuu Jimbo la Zanzibar alivyomchana live Rais wa Zanzibar kuhusu suala la umilikishwaji ardhi wa bara huko Zanzibar.
Ndio maana kuna hitajiko la Katiba Mpya hususani ile rasimu ya Jaji Warioba bila mabadiliko yeyote ifanywe ndio Katiba ya Nchi
Suala la ardhi Zanzibar: Askofu Augustino Shayo apiga msumari wa moto mbele ya Rais Mwinyi
Mhashamu Askofu Augustino Shao wa Zanzibar ametimiza Jubilei ya miaka 25 katika utumishi wa kanisa la Roman Catholic huko Zanzibar. Kwenye sherehe zilizohudhuliwa na wananchi mbalimbali wakiwemo viongozi wa kidini, askofu Shao kwenye salamu zake kwa Rais wa Zanzibar, amezungumzia mambo...www.jamiiforums.com
Zanzibar inachangia asilimia ngapi kwenye fuko la Tanzania?Bado huelewi! Ofisi ya VP ilianzwa wakati wa JK na kumalizwa wakati wa JPM.
Bado huelewi! Ofisi hizi ni za JMT ambayo Zanzibar ina haki sawa na Tanganyika kwani nchi hizi ndizo ziliungana kuunda JMT. Ikiwa ni sawa kuwa na Ofisi Dar na Dodoma kwanini isiwe sawa kuwa na Ofisi ndogo Zanzibar? Gharama hizi zote zinatoka JMT ambapo Zanzibar ni mshirika wa Tanganyika ISIYOKUWEPO.
Naomba radhi kwa kutoelewa swali nilipojibu mara ya kwanza, kuhusu "athari zinazotokana na muungano kuvunjika."Lakini hii siyo athari ya kuvunjika muungano. Ninachouliza ni athari gani mnaziziona?
Wazanzibar waulizwe kama wanataka muungano au la!
Mtanganyika asiulizwe haimhusu wala haathiriki na chochote au lolote lile ukivunjika.
Leo hii tuna rais Mzanzibari anawaamulia Watanganyika mambo mengine ambayo wala siyo ya Muungano. Sasa hii inakuwaje?
Hakuna Mtanganyika mwenye power ya kuwaamulia Wazanzibari mambo yao ya ndani yasiyo ya muungano!
Kwa Mujibu wa Jenerali Ulimwengu anadai wakati wa mijadala yao G55 na Mwalimu pale Msasani, Mwalimu aliwahi kumuuliza Mateo Qares kuwa "Wewe una ukaribu zaidi na Wazaramo na wandengereko kuliko wao walivyo karibu na Wazanzibari?"Kuna makundi mangapi hilo ni tatizo lao, kwa Mtanganyika wa Kigoma au Tukuyu au Tarime haathiriki
Hili lisiwe swali gumu kulijibu.Zanzibar inachangia asilimia ngapi kwenye fuko la Tanzania?
Kapimwe akili, hauko sawa hata kidogo!! Labda nikuhoji swali dogo: hivi Watanganyika wakihamua kuwatimua Waunguja wote na Wapemba wanao ishi bara na kumiliki mashamba,aridhi ,majengo na viwanda nk, niambie mtakuwa wageni wa nani??
FYI, you people needs us more than we do - don't you forget that, mnatutegemea kwa mambo mengi tu, msione mambo mengi tunamezea mkafikiri sisi ni KUBWA JINGA far from it, I trust this serves you right next time utafikiria mara mbili mbili kabla huja-comment chochote kuhusu masuala ya Muungano. CHEERS.
Mbona alimtetemesha Jumbe alipomuona yuko serious?Ni athari gani?
Mwaka 1967 Nyerere alisema '' Wazanzibar wakiukataa muungano sitwapiga mabomu''
Nauliza athari gani?
Ninaposema Kigoma, Tukuyu au Tarime nina maana moja kwamba ile impact ya muungano kwa watu hao ipo wapi? Kiuhalisia nini unadhani watakosa nje ya muungano? Hawategemei chochote kutoka ZanzibarKwa Mujibu wa Jenerali Ulimwengu anadai wakati wa mijadala yao G55 na Mwalimu pale Msasani, Mwalimu aliwahi kumuuliza Mateo Qares kuwa "Wewe una ukaribu zaidi na Wazaramo na wandengereko kuliko wao walivyo karibu na Wazanzibari?"
Ukiiangalia Tanganyika ya Tukuyu, Tarime au Kigoma na kusahau kuwa Tanga, Dar es salaam au Mtwara nako ni Tanganyika. Utakosea.
Idi Amini aliwaza hivyo alipoamua kuwafukuza wahindi, matokeo yake.....Kapimwe akili, hauko sawa hata kidogo!! Labda nikuhoji swali dogo: hivi Watanganyika wakihamua kuwatimua Waunguja wote na Wapemba wanao ishi bara na kumiliki mashamba,aridhi ,majengo na viwanda nk, niambie mtakuwa wageni wa nani??
Hapana swali ni hili, SMZ inachangia nini? Hatuzungumzii mtu binafsi.Hili lisiwe swali gumu kulijibu.
Mzanzibari anapoamua kuishi na kufanya shughuli zake sehemu yoyote ya Tanganyika, huyu tayari anachangia kwenye pato.
Kwa hiyo, kama tukiondoa haya ya wanasiasa kubagua watu kwa misingi ya wanakotokea (i.e., mTanganyika asiweze kujishughulisha Zanzibar, kwa mfano), hili swala siyo swala la muhimu sana.
Ila pengine umuhimu wake utaongezeka, wakati Zanzibar akigundua na kuchimba gesi/mafuta, halafu pato hilo lihodhiwe huko huko Zanzibar, lakini gesi ya Mtwara ikiuzwa ilete faida kote Zanzibar na Tanganyika, hapo swali litakuwa na uzito wake.
Kama huna hoja, kusoma hoja kunasaidia. Ahsante