Ni halali Wazanzibari kufanya kazi za Watanganyika?

Lini maisha yaliwah kuwa rahisi???
 
Nasikia ukienda Zanzibar na kama wewe ni wa Bara/Tanganyika basi huruhusiwi kununua ardhi huko na kuimiliki kwa kisingizio cha kwamba wao wazanzibari wako wachache na ardhi yao ni Ndogo. Ila wakija huku wao wanamiliki tu ardhi, na hapo hapo asilimia kubwa ya Wazanzibar hawautaki Muungano. Sasa nawaza kama Muungano ungevunjika basi Wazanzibari wote wenye ardhi bara wangerudi makwao Zanzibar na wangepoteza umiliki wa ardhi zao huku Bara. Mi naona hawa Wazanzibar Wangeung'ang'ania huu Muungano kwa kuwa kuna baadhi ya maeneo unawafavour japo maeneo mengine mengi ni changamoto kama wanaumia wao na ndio maana kuna muda wanaona Muungano sio msli kwao. All in All wacha tuendelee kuuthamini muungano, Sisi sote ni Watanzania.
 
Mhuu kuna shida hapa, inajulikana, ila viongozi wana woga kulitatua. Wanaogopa kuvunjika kwa muungano (Kikwete hutuba yake bungeni akiipiga Rasimu ya katiba iliyopendekeza serikali tatu). Dawa sii kulitupilia chiniya kapet dawa ni kulitatua na tuna fursa hiyo katika kutengeneza katiba mpya. Ila silioni hili likitekelezwa kwani kila aneingia madarakani na kuona alivyo juu ya sheria hupendelea kupaki juu ya sheria (na shinikizo la chama tawala ili kubaki madarakani) hufanya yake na kuondoka zake.
 
Syo walimu tu hata ma DED wako kibao mfano wa kinondoni Hanifa Hamza
 
Juzi shirika la POSTA limetangaza kutenga Asilimia 25 ya AJIRA zake Kwa wazanzibar labda ndio wakati watu wenyewe hawazidi Asilimia moja ya watanzania wote
Huyu demu nampendaga sana yani ubaguzi wa wazi, hakuna mtanganyika anaeajiriwa znz ila wa znz kibao bara
 
Ni halali kwa sababu hatuna utabganyika wala tanganyika, tuna tanzania!
nop kuna tanzania na zanzibar,
nilisafiri nje nchi flani nikakuta kuna chama cha diasporas cha watanzania na pia kuna chama cha wanzanzibar.
Hawa wanzanzibar hawapo kabisa kwenye. chama cha watanzania ilhali pasport wanazotumia ni sawa zote za jamhuri ya muungano wa Tanzania. Na pia wamejiandikisha kwenye ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Nikajaribu kuwadodosa watanzania wezangu mbona mmejitenga?
Wakanijibu Wazanzibari ni wabaguzi sana hata kule hawajitambulishi kama watanzania wanajitambulisha ni Wazanzibari.
Kwa kifupi kuna tatizo kubwa sana watawala wamelifumbia macho.
Ila ujinga huu aliutaka Mzee wetu RIP JK Nyerere.
The same kwenye ishu ya ardhi wao wao huku wanamilikishwa ardhi sawasawa kama watanzania wa bara ila mtanzania wa bara kwa zanzibar haiwezekani sanasana atakodishiwa kama mwekezaji mgeni rejeeni clip Askofu Mkuu Jimbo la Zanzibar alivyomchana live Rais wa Zanzibar kuhusu suala la umilikishwaji ardhi wa bara huko Zanzibar.
Ndio maana kuna hitajiko la Katiba Mpya hususani ile rasimu ya Jaji Warioba bila mabadiliko yeyote ifanywe ndio Katiba ya Nchi


 
Lile jambo litatimiaje nkt ulishanyea kambi mkuu pia umempiga biti bi mkubwa...tuje kwenye point sasa hayo maswala yao ya ukaazi ndo yanayokubagua wewe mtanganyika kupata kazi,ardhi huko zanzibar...bila hivyo hupati kazi wala huwezi kununua ardhi..
 
Lile jambo litatimiaje nkt ulishanyea kambi mkuu pia umempiga biti bi mkubwa...tuje kwenye point sasa hayo maswala yao ya ukaazi ndo yanayokubagua wewe mtanganyika kupata kazi,ardhi huko zanzibar...bila hivyo hupati kazi wala huwezi kununua ardhi..
Mtanganyika unapata kazi Zanzibar as an expert, na ardhi unalikikishwa as an investor!. Mimi Mzee Mayalla amefanya kazi Zanzibar for 4 years as a head of security. Usikute kule kuna wadogo zangu!.
P
 
ni kweli
 
Wazanzibari ambao hawaishi huko hawatambuliki kama Wazanzibari. Hawana haki ya kumiliki ardhi. Hata leseni ya udereva wanadai kitambulisho cha Mzanzibari mkaazi.
Kitambulisho hiki kimewekwa mahsusi kwa kubaguwa. Na wananyimwa hata wanaoishi huko kwa tafauti za kisiasa ili wakose haki za msingi ikiwemo ajira.
 
Dodoma ni eneo tu, lakini Wazanzibari wenyewe wanashiriki kikamilifu ndani ya CCM. Kwani hujui kuwa CCM ni TANU na ASP?.
Hapana. Dodoma si eneo tu.
Utayasahau vipi ya akina Jumbe mara hii; unataka hata hili tukumbushane tena?

Ndiyo, inawezekana kukawa na mwonekano wa kimazingaombwe wa "wazanzibar wenyewe wanashiriki kikamilifu ndani ya CCM...", lakini nitakushangaa kama hujui unafiki uliomo ndani ya CCM, bila kujali washiriki wanatokea sehemu gani ya Muungano.
 
Si ni Wazanzibar waliomkataa Mzanzibar mwenzao Salim. Ahmed Salim asiwe rais baada ya Nyerere mwaka 1985, Wakaona ni heri achukue "Mtanganyika" mzee Ruksa?

Si ni Wazanzibar ndani ya CCM waliomwambia Seif Sharif Hamad kuwa hawatoi nchi kwa vipande vya karatasi?
 
Uzi wa kibaguzi na uliokosa mashiko. Kama mzanzibar kaoa au kaolewa huku bara huyo mtoto anayezaliwa abaguliwe kwa sababu ya wazazi wake?.

Mada nyepesi inayokwenda kinyume na tamaduni za kitanzania inaweza kuvunja mshikamano wetu badala ya kuufanya ukawa imara.
 
Huu ndio ukweli.
Kwa visingizio mbali mbali Wazanzibari wanabaguwa wenzao.
Kuna kulinda mapinduzi.
Kuna kulinda muungano
Kuna kudumisha amani na utulivu.
Mwisho wa yote ni kuendelea kuhodhi madaraka ili kunufaisha kikundi chao.
 
Duh!

Hata Jumbe mwenyewe niliyemtaja hapo juu; si ni akina Maalim waliomchomea utambi?

Kwa hiyo mambo yanaanzia huko huko kwa waZanzibari wenyewe?

Hata hivyo, sina mfano, na sijui kama unao mfano wewe, mahsusi wa waZanzibari walioko CCM, waliokomalia jambo ambalo CCM ya waTanganyika hawakulitaka na wakafanikiwa kulipitisha walivyotaka wenyewe bila ya baraka za CCM Tanganyika.
Bendera na Katiba ya Zanzibar?
 
inaelekea unafahamu mengi sana naomba kufahamishwa maana simfahamu kile ni kisiwa cha Zanzibar Zanzibar yenyewe ni ipi
 
Aiseeee!

Naona umevamia mada bila kuelewa kinachojadiliwa.

Ni nani anayembagua mwenzake kati ya pande mbili za Muungano. Hili nalo hulijui wala hulioni?

Haya yanayofanyika sasa hivi ndiyo unayodhani yataufanya Muungano kuwa "imara". Unaelewa maana ya hilo neno "imara" kweli, au unajiandikia tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…