Ni halali Wazanzibari kufanya kazi za Watanganyika?

Uzi una mantiki sana nashangaa hujibu hoja umeingiza mambo yasiyokuwepo

1. Mtoto anayezaliwa na wazazi wa pande mbili ni Mtanzania. Tatizo linakuja kwamba Mtanzania ni Mtu wa bara halafu kuna Mzanzibar. Mtoto huyo anabaguliwa na Wazanzibar kwasababu ya huo Uzanzibar.

2. Hoja ya Allen Kilewella : yapo mambo Wazanzibar wanalamika si ya muungano.

21% ajira zilizotengwa kwa Wazanzibar ni pamoja na mambo yasiyo ya muungano, je hiyo ni kuwatendea haki Watanganyika ambao hawana fursa hiyo Zanzibar?

Hivyo unatakiwa kujibu hoja za mleta mada si kugundua hoja nje ya mada.

Kwa lugha rahisi Wazanzibar wanalaani kuongezwa kwa mambo ya muungano kama elimu ya juu, lakini wapo bodi ya mkiopo ya elimu ya juu na wanapewa kutoka HESLB. Je Mtanganyika anapewa ZHESLB?

Hapa ni kwamba Wazanzibar wanasema '' Nguruwe ni haramu lakini mchuzi wake ni halali''

Tunakuuliza wewe, je hiyo ni sawa?
 
Nawaza sana mantiki ya kwenda kujenga Ikulu ndogo Zanzibar, ofisi ya Makamu wa Rais, na cha kustaajabisha sana ofisi ya waziri Mkuu. Hivi Waziri Mkuu ni mambo ya Muungano?? Hivi hawajui ni kwa nini tuna Waziri Mkuu kwenye serikali ya Muungano Tanzania?

iko siku tutakuwa na Waziri Mkuu toka Zanzibar na watanganyika watakaa kimya.
 
Hata masheikh wa uamsho walisalitiwa na Wazanzibar wenzao waliokuwa madarakani
 
Tumewahi kuwa naye.
Salim Ahmed Salim amewahi kuwa waziri mkuu
 

wewe utakuwa mzanzibar , nyie ndio wabaguzi mkiambiwa ukweli mnaleta eti suala la mshikamano.
Ubaguzi wenu zidi ya wabara lazima uanikwe na upingwe kwa nguvu zote ikibidi hata kwa kuvunja huu Muungano wewe na wenzako wote akina bakharesa, samia suluhu hasan na wapemba waliojazana kkoo mrudi kwenu mkija bara muombe visa.
Hii biashara ya chetu chetu, chenu chetu ni upuudhi uliopitiliza
 
Huyu jamani ni mpemba itakuwa ni mmoja wapo wa wanufaika wa huu upuuzi anaelewa kila kitu anajifanya kujitoa ufahamu
 
Swali la ku muuliza nyerere Na wazee wa zamani hili walio fanya hili kwa hapa sidhani kama utapata jibu sahihi[emoji28][emoji28]
Sio sahihi kusubiri wazazi waliokwenda mbele ya haki warudi kukurekebishia nyumba waliyokuachia eti kwa sababu hawakuijenga vizuri !! Fanyieni ukarabati hiyo nyumba mlioachiwa vinginevyo itakuja kuwaangukia siku moja !!
 
Kwa lugha rahisi Wazanzibar wanalaani kuongezwa kwa mambo ya muungano kama elimu ya juu, lakini hao hao wapo bodi ya mkiopo ya elimu ya juu na wanapewa bure (hawakopi) kutoka HESLB
Mkuu kuna mambo ama huyajui au jazba imepanda mno. Wazanzibari, kama Watanzania wengine, wanapata mikopo kutoka HESLB na wanalipa. Lakini haya mambo ya kuambiwa nawe ongeza yako.
 
Kuna mambo yanafanyika yanatia shaka mantiki yake.

Hakuna sababu za kujenga ikulu hizo kuongeza mzigo kwa mlipa kodi.

Majuzi Rais anasema Zanzibar iwe special zone ya police kwasababu ya nature yake.
Hivi Zanzibar inapakana na nchi ngapi?Tanganyika inapakana na nchi 8 inahitaji resources zaidi .
Kwanini special zone Zanzibar na siyo Mtwara ?

Haya yanatokea kwasababu hakuna mtu anayesimamia masilahi ya Tanganyika.

Watanganyika wanabeba muungano 100%. Kwenye vikao vya kero wanwakilishwa na nani?r

Ipo siku tutamuuliza Philip na hili linaweza hitimisha ndoto yake. Ataulizwa alisimamiaje Tanganyika?

G55 waliona mambo kama haya! siku hizi kule mjengo wamelala wakiamka wanaimba na kusifu
 
Nguruvi3 maslahi ya Tanganyika si yanasimamiwa na Waziri Mkuu, mbona Kassim Majaaliwa yupo kimya?
 
Mungelijua yalio kwenye mioyo ya wazanzibari, basi nadhani watanganyika msingekuwa mkija na thread kama hizi. Ukweli ukienda Zanzibar kila corner ya km kama 25 basi unapita kwenye checkpoint ya vyombo vya usalama vya Tanganyika (sawa na wapalestina).

Sasa ifike wakati tuheshimiane bana, mkiona kama mshachoka vunjeni. Huku hatuwezi kupigana na Tanganyika kwa hiyo tunawasubiri nyie huko ndio mlioshika mpini wa vyombo vya dola.

Kama mlivyokuja kupindua mkatuu na babu yenu Nyerere basi na sasa vunjeni tuu. Msianze kutuchosha na mathread ya sio na kichwa wala miguu.
 
Ulinzi ni jambo la Muungano. Kaa kimya.

Huku bara hakuna anayehoji makamanda na maaskari toka Zanzibar walioko Tanganyika. Tunachohoji ni kwa nini Mambo na kazi za Watanganyika zifanywe na wanzibari?
 
Nguruvi3 maslahi ya Tanganyika si yanasimamiwa na Waziri Mkuu, mbona Kassim Majaaliwa yupo kimya?
Waziri mkuu si anawekwa na Rais, anaweza kuondolewa wakati wowote. Hana kauli yoyote ile
Tanganyika ingalikuwa na kiongozi anayewajibika kwake, haya yasingetokea
Tanganyika hiyo hiyo ndiyo imebeba gharama za muungano 100%!
 
Kama ni hivyo kwann mtanzania bara haruhusiwi nunua ardhi Zanzibari kama kweli sisi wote ni uraua mmoja ambao ni JMT????
 
Nguruvi3 wakati mwingine nikiwaza nguvu ya waziri mkuu huwa najiuliza nguvu yake bungeni. Ukiangalia hakuna wakati Bunge la Tanzania linajadili mambo mahsusi ya Tanganyika. Kila wakati wakati tunajadili mambo ya Nanjilinji Kilwa, na mbunge wa kiembesamaki naye anachangia. Ila wao kwenye baraza la wawakilishi hakuna Mtanganyika anayejadili mambo yao.
 
Kama ni hivyo kwann mtanzania bara haruhusiwi nunua ardhi Zanzibari kama kweli sisi wote ni uraua mmoja ambao ni JMT????
Tatizo linaanza pale mnapojiita watanzania bara badala ya watanganyika.
 
Ulinzi ni jambo la Muungano. Kaa kimya.

Huku bara hakuna anayehoji makamanda na maaskari toka Zanzibar walioko Tanganyika. Tunachohoji ni kwa nini Mambo na kazi za Watanganyika zifanywe na wanzibari?
Nenda Jozani pale utakutana na kina Sara na Josephu wanafanya kazi kwenye taasisi ya utalii. Mambo ya muungano hayajulikani tena, but I hope Jozani sio taasisi ya muungano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…