Ni halali Wazanzibari kufanya kazi za Watanganyika?

Ni halali Wazanzibari kufanya kazi za Watanganyika?

Hivi ni halali kwa Wazanzibari kuajiriwa Tanganyika kama waalimu bila ya kuwa na vibali vya kufanya kazi?

Ni halali Wazanzibari kuajiriwa kama watendaji wa mitaa na Kata?

Ni halali kwa Mzanzibari kuteuliwa kuwa Mkuu wa mkoa au wilaya huku Tanganyika?

Ni sawa kwa Mzanzibari kupewa Leseni ya biashara Tanganyika bila kwanza kupewa kibali cha kufanya kazi?

Mzanzibari anaweza kuteuliwa kusimamia wizara zisizo za Muungano?

Ni halali kwa Mzanzibari kugombea nafasi za kisiasa Tanganyika?

Kodi anayotozwa Mzanzibari inatakiwa iende nchini kwao Zanzibar ama itumike Tanganyika?
Muungano sijawahi kuupenda.Ni kaujinga fulani hivi.Nyerere sijui alikuwa amewaza kitu gani!Ni unyonyaji tu.
 
Yaani hao top ni matatizo tupu.

Rais wa JMT ni Mzanzibar.

Makamu kwakweli hana influence yeyote ya kisiasa.

PM naye haeleweki.

Tanganyika imebakia Yatima inapigwa front and behind , right ,left and center hakuna wa kuitetea.

Ndio maana kila kitu ni ghali na hakuna anayejali.

Maisha mtaani ni magumu mara dufu. Hao ambao wana jiweza hawawakumbuki kabisa wasiojiweza.
Bado haujaligusa tatizo.Funguka!
 
Mkuu, si halali kwa mujibu wa Wazanzibar lakini ni halali kwa mujibu wa katiba ya mpito ya 1964.
Katiba ya 1964 ilisema mambo yote ya Tanganyika yatakuwa ya muungano
Wazanzibar wanasema mambo ya muungano yalikuwa machache ingawa yameongezwa

Kwa mujibu wa Wazanzibar sehemu zote ulizotaja hapo si za muungano. Hoja yao ni kwamba kwa katiba ya mpito Tanganyika ilivaa koti la Muungano. Kitu cha kushangaza waliojificha ndani ya koti la Muungano ni Wazanzbar ambao hunufaika na mambo yale yale wanayolalamika yameongezwa kama ulivyoyataja

Kuteuliwa, hakuna sheria inayomkataza Mzanzibar asiteuliwe kwasababu nafasi 'X' husema kwa 'Mtanzania'
Hapa Wazanzibar wanavua Uzanzibar wao wanavaa Utanzania. Kwa miaka ya nyuma nafasi fulani za Tanganyika waliteuliwa katika spirit ya muungano lakini hawakupewa uongozi kamili

Kugombea: Again Wazanzibar wanapotaka kugombea wanavua Uzanzibar wao wanavaa Utanzania kwahiyo katiba inaruhusu wateuliwe. Ni kama ilivyo ardhi , elimu ya juu n.k. au usimamizi wa Taasisi za Tanganyika

Kodi: Yes,kuna kodi za muungano zinazopelekwa Zanzibar nje ya ile 4.5% ya pato la Tanganyika.
Tanganyika na Taasisi zake zinatoa ajira nyingi kuliko SMZ, hivyo kupunguza mzigo wa ajira Zanzibar.

Mfano, Zanzibar wanapewa 21% ya ajira za muungano wakiwa watu milioni 1.2 tu.
Ikiwa ajira za muungano ni 100,000 tunaongelea 21,000 mara mbili ya ajira za SMZ takribani 10,000.

Jambo la kushangaza kodi wanazolipa zinapelekwa Zanzibar! Yaani wanapewa ajira za bure za Watanganyika halafu SMZ wanalipwa kwa kupewa ajira hizo na kupunguziwa unemployment!

G55 wakati wa Mwinyi waliona upendeleo na matatizo makubwa. Yamerudi sasa hivi kila kitu Zanzibar hata majaji wa mahakama kuu wanateuliwa kutoka Zanzibar , mawaziri, viongozi wa Taasisi n.k.

Warioba kasema ni mambo 7 tu, mengine kila mtu aangalie utaratibu wake. Watanganyika kutoa hisani
Kuoa na kuolewa inakuaje

Masuala ya Ardhi kununua na kuuza, je watu wa bara tunaruhusiwa kwenda kurundikana na kununua mashamba na Ardhi uko Zenjibar na kujenga majumba, maviwanda na mahotel makubwa?

Masuala ya Biashara kodi na makato, ukinunua kitu Zanzibar Kodi inakuaje na makato yanaenda wapi na ukinunua kitu bara Kodi inaenda wapi na makato yanakuaje

Masuala ya usafiri kuingia na kutoka je kuna live permit au unaingia km unaingia uwani na kutoka

Emu gusia na hapo inakuaje mkuu
 
Ebu kuwa na akili..acha kijifanya mjinga na mpumbafu.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app

Kwani kuuliza ndiyo ujinga? Halafu nashangaa nyie mliovamia Zanzibar na kupora mali za watu, kumwaga damu za watu, kutia watu vilema kila siku mnapiga kelele kuhusu Zanzibar. Kwani mlitumwa kuja huku? Nyerere aliwadanganya akifikiri Zanzibar itakuwa sawa na Hawaii kwa Marekani kumbe la. Kawabebesha mzigo. Ondokeni tu huku Zanzibar tumeshawachoka.
 
Kwani kuuliza ndiyo ujinga? Halafu nashangaa nyie mliovamia Zanzibar na kupora mali za watu, kumwaga damu za watu, kutia watu vilema kila siku mnapiga kelele kuhusu Zanzibar. Kwani mlitumwa kuja huku? Nyerere aliwadanganya akifikiri Zanzibar itakuwa sawa na Hawaii kwa Marekani kumbe la. Kawabebesha mzigo. Ondokeni tu huku Zanzibar tumeshawachoka.

Kapimwe akili, hauko sawa hata kidogo!! Labda nikuhoji swali dogo: hivi Watanganyika wakihamua kuwatimua Waunguja wote na Wapemba wanao ishi bara na kumiliki mashamba,aridhi ,majengo na viwanda nk, niambie mtakuwa wageni wa nani??

FYI, you people needs us more than we do - don't you forget that, mnatutegemea kwa mambo mengi tu, msione mambo mengi tunamezea mkafikiri sisi ni KUBWA JINGA far from it, I trust this serves you right next time utafikiria mara mbili mbili kabla huja-comment chochote kuhusu masuala ya Muungano. CHEERS.
 
Mkuu Allen Kilewella , kwanza hiki ulichokileta ni ubaguzi wa kutaka kuwabagua Wazanzibari!. Mwalimu Nyerere alisema hii ni dhambi!. Kiukweli somo la uraia linahitajika sana Tanzania kwa watu kama wewe!. Tanzania ni nchi moja, ya JMT, yenye uraia mmoja tuu wa Tanzania, kila Mtanzania ana haki sawa na haki zote za raia wa Tanzania.

Ndani ya uraia wa Tanzania kuna uraia mmoja tuu wa Mtanzania.

Kwa vile Tanzania ni nchi moja ya JMT, ndani ya JMT kuna sehemu moja ya Zanzibar ina utawala wake wa ndani ambao Wazanzibari licha ya kwanza kuwa ni raia wa JMT wenye haki zote za uraia wa JMT, hawa wamepewa haki za ziada za ukaazi wa Zanzibar. Kitambulisho cha ukaazi wa Zanzibar sio kitambulisho cha uraia, hakuna uraia wa Zanzibar kuna uraia mmoja tuu wa JMT na ziada ya ukaazi wa Zanzibar.

Hivyo Wanzanzibari wana haki zote za uraia wa Tanzania na ziada ya haki za ikaazi wa Zanzibar.

Lile jambo langu likitimia, nafungua darasa la bure la Haki, kuwaelimisha Watanzania haki zao mbalimbali zikiwemo haki za uraia.
P
Brother bora ungekaa kimya maana hata ulichokiandika hakieleweki.
 
Ni halali Wazanzibari kuajiriwa kama watendaji wa mitaa na Kata?

Ni halali kwa Mzanzibari kuteuliwa kuwa Mkuu wa mkoa au wilaya huku Tanganyika?

Ni sawa kwa Mzanzibari kupewa Leseni ya biashara Tanganyika bila kwanza kupewa kibali cha kufanya kazi?

Mzanzibari anaweza kuteuliwa kusimamia wizara zisizo za Muungano?
Ndiyo maana hatuendelei

Yawezekana tunatengenezewa kero ili tuwafukuze watenegeneze sababu ya kujitoa kwenye union
 
Tanzania ni matokeo ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kama Zanzibar ipo ni kwa nini Tanganyika isiwepo.

Kwa nini kuwepo kwa Tanzania kuipoteze Tanganyika lakini Zanzibar iendelee kuwepo?
Swali la ku muuliza nyerere Na wazee wa zamani hili walio fanya hili kwa hapa sidhani kama utapata jibu sahihi[emoji28][emoji28]
 
Upumbavu wa viongozi kuikumbatia zanzibar imesababisha maumivu Tanganyika.Tozo zinazobuniwa kila siku zinatokana na matumizi makubwa kama haya ya kuibeba Zanzibar.IPO siku haka kamuungano kakipuuzi tutakavunjilia mbali pale wazalendo tutakaposhika madaraka.Haiwezekani Zanzibar chao ni cha kwao lakini cha Tanganyika ni cha wote
Wa Tanganyika ni wapumbavu, vunjeni muungano.
 
Inshort hakuna kitu kinachoitwa Tanganyika kwa Sasa... Kuna serikali ya Zanzibar na ya muungano wa Tanzania... Hakuna serikali ya Tanganyika wala Ardhi ya Tanganyika ipo Ardhi ya Tanzania ambayo imetokana na muunganiko wa Tz na ZN... Angekuepo mwalimu nyerer na wazee wengine wangetueleza wao waliona tanganyika tutapata manufaa gani hasa kwa kuungana na Zanzibar na pili kuiloweka Tanganyika kabisa isiwepo
 
Back
Top Bottom