Mkuu
Allen Kilewella , kwanza hiki ulichokileta ni ubaguzi wa kutaka kuwabagua Wazanzibari!. Mwalimu Nyerere alisema hii ni dhambi!. Kiukweli somo la uraia linahitajika sana Tanzania kwa watu kama wewe!. Tanzania ni nchi moja, ya JMT, yenye uraia mmoja tuu wa Tanzania, kila Mtanzania ana haki sawa na haki zote za raia wa Tanzania.
Ndani ya uraia wa Tanzania kuna uraia mmoja tuu wa Mtanzania.
Kwa vile Tanzania ni nchi moja ya JMT, ndani ya JMT kuna sehemu moja ya Zanzibar ina utawala wake wa ndani ambao Wazanzibari licha ya kwanza kuwa ni raia wa JMT wenye haki zote za uraia wa JMT, hawa wamepewa haki za ziada za ukaazi wa Zanzibar. Kitambulisho cha ukaazi wa Zanzibar sio kitambulisho cha uraia, hakuna uraia wa Zanzibar kuna uraia mmoja tuu wa JMT na ziada ya ukaazi wa Zanzibar.
Hivyo Wanzanzibari wana haki zote za uraia wa Tanzania na ziada ya haki za ikaazi wa Zanzibar.
Lile jambo langu likitimia, nafungua darasa la bure la Haki, kuwaelimisha Watanzania haki zao mbalimbali zikiwemo haki za uraia.
P