Ni halali Wazanzibari kufanya kazi za Watanganyika?

Ni halali Wazanzibari kufanya kazi za Watanganyika?

Hao watanganyika ndio watu gani unatuletea mambo ya historia za mwaka 1964 kurudi nyuma mimi najijua ni Mtanzania na ninachojua Mzanzibari naye ni Mtanzania sasa kwanini ajira za Tanzania Bara asiombe acheni mambo yenu ya kibaguzi Watanzania hatuna hayo mambo ya kubaguana kwa kabila au ukanda ukiwa Dar panda boti nenda Zanzibar enjoy we uliopo Zanzibar njoo Dar es salaam au popote ndani ya Tanzania bara unapojisikia kwenda upo nyumbani hakuna atayekuuliza kwanini umeenda uko.
 
Ni suala la muda tu mchanganyiko wa watu Zanzibar utabadilika vya kutosha kuwapa "watanganyika" sauti na nguvu kubwa katika uendeshaji wa SMZ. Hili linafanyika kwa umakini sana.
 
Damu ya wazee wetu ilimwagika walipambana kupata Tanganyika...mwisho wasiku hakuna Tena taifa walilolipigania kisa watu wawili walikaa sirini wanafanya muungano usio na mawaza anuwahi!!
Unafutaje historia yenye heshma ya taifa la Tanganyika?? Muungano sawa lkn unafutaje jitihada za wazee kutafuta Tanganyika?? AIBU
 
Kitambulisho cha Uzanzibar wenyewe wanapeana kwa kuangalia nywele, seuse chogo wa Tanganyika!

Ni hivi Wazanzibar walinde ajira zao ni haki yao, lakini wasiingilie za Tanganyika.
Walinde pia ndizi zisiingie , wafukuze Wamasai kwa vipigo. NI haki yao

Ni wakati Watanganyika walinde ajira zao. Ni fedheha kuzunguka na bahasha la khaki tena akisailiwa na Mzanzibar kwa kazi za Tanganyika wakati kijana huyo hana nafasi Zanzibar
 
Hao watanganyika ndio watu gani unatuletea mambo ya historia za mwaka 1964 kurudi nyuma mimi najijua ni Mtanzania na ninachojua Mzanzibari naye ni Mtanzania
Wewe umekuwaje mtanzania bila kwanza ya Tanganyika na Zanzibar kuungana??

Sasa eti Kuna Mzanzibari na Mtanzania. Kwa Nini Mzanzibari kabakia wakati mtanganyika ionekane ni jambo la kabla ya Muungano??

Jee hadhi ya Mtanganyika na Mzanzibari zinafanana?

Mbona baada ya Muungano uzanzibari umebakia??

Kilichouua utanganyika ni nini?
sasa kwanini ajira za Tanzania Bara asiombe acheni mambo yenu ya kibaguzi Watanzania hatuna hayo mambo ya kubaguana kwa kabila au ukanda ukiwa Dar panda boti nenda Zanzibar enjoy we uliopo Zanzibar njoo Dar es salaam au popote ndani ya Tanzania bara unapojisikia kwenda upo nyumbani hakuna atayekuuliza kwanini umeenda uko.
Kumbe Tanganyika kwako wewe ni Dar es salaam!!
 
Kwasababu serikali ya Tanganyika ilivalishwa koti la Serikali ya muungano na Mwl Nyerere toka mwaka 1964 (hivyo serikali ya Tanganyika ilipotezwa kijanjaa) na huenda Karume aliridhia asichokifahamu vyema.
Jee wazanzibari hawamo kwenye serikali ya Muungano??

Wakati wa kujadili mambo ya Tanganyika kwenye Bunge la Muungano, wazanzibari hutoka nje au na wao hushiriki kujadili mambo ya Tanganyika "yasiyowahusu"?
 
Ufafanuzi wa Mwalimu ni kwamba kila mzanzibari ni mtanzania lakini si kila mtanzania ni mzanzibari. Kwa bahati bado hatujawa tayari kuhoji maoni yake haya.
Kuhusu kitambulisho cha mzanzibari vigezo muhimu ni uwe CCM au uthibitishe wewe si mpemba.
 
Ni suala la muda tu mchanganyiko wa watu Zanzibar utabadilika vya kutosha kuwapa "watanganyika" sauti na nguvu kubwa katika uendeshaji wa SMZ. Hili linafanyika kwa umakini sana.
Mzanzibari hata mfanye vipi anajulikana na kila mtu ana kwao Kama ulivyo na kwenu Mkuranga hizo mbinu tulizishtukia zamani
 
Hao watanganyika ndio watu gani unatuletea mambo ya historia za mwaka 1964 kurudi nyuma mimi najijua ni Mtanzania na ninachojua Mzanzibari naye ni Mtanzania sasa kwanini ajira za Tanzania Bara asiombe acheni mambo yenu ya kibaguzi Watanzania hatuna hayo mambo ya kubaguana kwa kabila au ukanda ukiwa Dar panda boti nenda Zanzibar enjoy we uliopo Zanzibar njoo Dar es salaam au popote ndani ya Tanzania bara unapojisikia kwenda upo nyumbani hakuna atayekuuliza kwanini umeenda uko.

Watanganyika ni watu wabaya sana , wametuvamia na kutuulia ndugu na wazee wetu, wametutia umasikini na hawakubali tuendelee. Mafuta tuliyoyagunduwa hawataki tuyachimbe tupate unafuu wa maisha ,kwa choyo na roho zao mbaya wanaendelea kuja kuweka vibaraka vyao kila uchaguzi ili tubakie maskini.
 
Waasisi walikuwa wanatamka tanzania bara na tanzania visiwani ila kadiri miaka inavyoenda zanzibar inajitenga kwa kasi sana ila muda si mrefu Tanganiyika inarudi
 
Waasisi walikuwa wanatamka tanzania bara na tanzania visiwani ila kadiri miaka inavyoenda zanzibar inajitenga kwa kasi sana ila muda si mrefu Tanganiyika inarudi
Bora irudi!!

Maana Tanganyika inadhalilishwa sana!!
 
Back
Top Bottom