Ni jambo gani watu wanalifanya sana lakini wewe huwezi?

Ni jambo gani watu wanalifanya sana lakini wewe huwezi?

Kukaa bar kunywa pombe huku unaangalia mipira na kukesha mpaka asubuhi. Siwezi hiki kitu japo pombe natumia lakini ikifka saa nne usiku nikiwa nje ya ghetto langu huwa nakuwa sina amani. Bora niagize vitu vyangu nijifungie ndani niwe nashusha mdogo mdogo huku nafanya kazi zangu.
Tunafanana kwenye hili, Mimi saa nne ikinikuta nje nakosa amani, Sina utulivu wala Raha.

Au kwenda kunywa bia sehemu yenye makelele, watu wanaimba imba hovyo siwezi

Yaani, unaenda kwenye kula kilaji, sehemu Ina makelele mpk ukitaka kuongea na muhudumu utumie sauti kubwaaa while amekusogezea sikio maana hata yeye hasikii
 
Tuende sawa.
Kuna baadhi ya mambo ni ya kawaida na yanafanyika kila siku lakini wewe huwezi au hujui namna yakufanya...
Mfano mimi;
1. Zile ngazi mwendo(escalators)siwezi kuzitumia, na sizitumii hata iweje...Siwezi.

2. Kula wali /pilau na ndizi mbivu kwa wakati mmoja....Siwezi.

3. Kumsimamisha mwanamke barabarani/kuomba namba, nilishashindwa....

Tuendelee...
Kuongea na simu kwenye umati,au usafiri wa watu wengi,siwezi!
 
Hata Mimi siwezi ... Unawezaje kukaa kwa utulivu sehemu yenye makelele?

Hii duniani ni ya ajabu! Eti Kuna watu wanapenda kelele,
😃😃 mimi inategemea na Mood ya siku hiyo
 
Tunafanana kwenye hili, Mimi saa nne ikinikuta nje nakosa amani, Sina utulivu wala Raha.

Au kwenda kunywa bia sehemu yenye makelele, watu wanaimba imba hovyo siwezi

Yaani, unaenda kwenye kula kilaji, sehemu Ina makelele mpk ukitaka kuongea na muhudumu utumie sauti kubwaaa while amekusogezea sikio maana hata yeye hasikii
😃😃😃
 
This is best comment nadhani 😂

Kwa sababu jamaa amejibu kwa ukweli sio utani, japo it's seem so funny to me!

Inaonyesha ukisikia mtu anasema hivi unakerekwa sana 😂
😀😀atumbie huwa anaanzaje?
 
😃😃 mimi inategemea na Mood ya siku hiyo
Nishawahi kwenda club ... Nilishangaa sana
Naona watu wanafurahia kukaa kwenye makelele

Nilishangaa sanaaa, nilishangaa mnooo!

Napenda sana ukimya na utulivu
 
Back
Top Bottom