Ni kheri ufiwe na mzazi kuliko kufiwa na mume/mke

Mkuu mkuu usikufuru kama hauoni umuhimu wa mzazi potezea na sio kuanza kumuombea kifo kisa mtu uliyekutana nae ukubwani. Mzazi ana umuhimu wake na mke,mume ana umuhimu wake pia. Jambo usilolijua au kulifahamu asilimia kubwa ya wanawake wapo tayari kumpoteza Mume na sio mtoto au mzazi wazazi wake.

Pole kwa msiba
[emoji419][emoji419][emoji419]
 
2019 nilifiwa na mke wangu hakika maumivu yake ni mazito, nyumba naiona chungu, ndani hakulaliki, naisikia harufu ya mke wangu mpaka sasa nikiingia ndani nasikia sauti yake.

Mke amefariki amekuachia watoto wadogo 3!

Kwa ambao hamjapitia hii changamoto ombeni sana Mungu awaepushe nayo.

Huu ni mwaka wa 4 lakini bado sijaweza kupata ahueni, nimeenda kwa psychologist lakini wapi.
Akili zikikurudia utaomba mods wafute huu Uzi.

Nakupa ushauri wa bure wasiliana na moderator waombe waedit hiyo heading ni ujinga umeandika.

Tuliofiwa na Mzazi tunajuwa maumivu yake ni ya kudumu, unaweza kufiwa na mke ukapata mwanamke mwingine na huenda akawa bora kuliko uliyempoteza lakini mzazi akiondoka ni forever na maisha yanabadirika rasmi tangu siku hiyo.
 
Yani MAISHA YANABADILIKA ASILIMIA 100.
 
Pole sana ,nami nimepitia hicho kikombe cha kupoteza mke wangu kipenzi.
Ameniachia mtoto mmoja wa mwaka mmoja, hakika ni maumivu yasiyo na mipaka
 
Mwanamke ye anataman afe mumewe lakin sio mtoto au wazazi wake

We wa kiume unasema bora wafe wazazi kuliko mke!

WAzazi ndio kimbilio letu tukiona mambo hayaendi kuna wakat mwingine huyo mwanamke unaetaka asife anaweza kukuvuluga utataman mzazi wako awepo ili umwambiee unayopitia

Pole sana mkuu
 
Tumetofautiana sasa, ndiyo maana wengine hutoa mpaka machozi wengine wakavu ukimpa hata gongo anakunywa bila shida yeyote

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app

Upo sahihi lakini tusifikie kiwango cha kuona uhai wa mtu fulani ulikuwa wa thamani, halafu uhai wa mtu mwingine si wa thamani kama mleta mada...

Mke au mume hufa, na hata kwenye kiapo cha wanandoa wa kikristo kuna maneno kama "hadi kifo kitapo tutenganisha"
 
Mwanamke ye anataman afe mumewe lakin sio mtoto au wazazi wake

We wa kiume unasema bora wafe wazazi kuliko mke!

WAzazi ndio kimbilio letu tukiona mambo hayaendi kuna wakat mwingine huyo mwanamke unaetaka asife anaweza kukuvuluga utataman mzazi wako awepo ili umwambiee unayopitia

Pole sana mkuu
Vipi wale wazazi wanaotoaga watoto wao kafala unasemaje hapo

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Upo sahihi lakini tusifikie kiwango cha kuona uhai wa mtu fulani ulikuwa wa thamani, halafu uhai wa mtu mwingine si wa thamani kama mleta mada...

Mke au mume hufa, na hata kwenye kiapo cha wanandoa wa kikristo kuna maneno kama "hadi kifo kitapo tutenganisha"
Hapo aliteleza tu naona na maumivu tu hayo, anatakiwa kufarijiwa tu lakini sio kumpa za uso kiasi hicho

Back
Top Bottom