Ni kosa gani ambalo utalijutia maisha yako yote?

Hahahaaaa duh kumbe hisia zangu za kweli. Nilijua ni iringa maana huko kwa mabumunda ni balaa. Mie pia niliishi iringa kanisa langu lilikuwa rc mshindo. Ni kuna mabumunda hatari bila kusahau gubiti za kutosha[emoji23] [emoji23] [emoji23]
hahhahah umesahau bagia za kunde na pilipili kibao, unatembea unatafuna, asikuombe mtu hapo
 
Kuna jamaa mmoja ni jirani yangu anafanya kazi katika kampuni ya mawasiliano, yeye na mke wake niliwaachia laptop yangu ikiwa imezimwa nikijua ni majirani wema kumbe wao wakaiwasha na kuanza kuangalia personal documents zangu, pictures pamoja na accounts zangu za facebook na jamiiforums........
 
No privancy tena, ungeomba uongozi wa JF ukubadilishie username tu
 
Imebid tu nilike kwa kumwambia mdingi akome
 
Siku nilipowashabikia Mh. Lowasa na Mh.Kikwete kwani ilinifanya nikosane na mpenzi wangu..
 
Kumlamba bawacha, sitasahau inawasha kama umekatiza kwenye pori la upupu
 
Una dalili zote kwamba utalambwa tu dagaa.
 
Najuta sana kukataa majibu ya mtihani wangu wa 4m4 mwaka 2010. Kuna jamaa alinipa majibu ya English nikakataa, nikasema huu mtihani nitaupiga vizuri matokeo yake nikapata pass. Kwa kweli huwa nahuzunika sana kukataa nafasi ile. Natamani siku zirudi nyuma nichukue majibu yale. Jamani kurudia mtihani sio mchezo, natafuta crdt moja lakin nimekata tamaa kabisa ya kuipata.
 
Bora wewe na kaka yangu ana M.A in the same field hana kazi mwaka wa nne huu.


Mkuu
Ndugu yako kasoma BPA na MPA?

Kama amesoma degree ya kwanza public administration (3.8+) na masters degree ya public administration (GPA 4.0+) ni PM namba yake.

Ila kama ana GPA za gentleman basi mpe pole na Mwenyezi Mungu amsaidie.
 
Du pole sana mkuu. Majuto ni mjukuu.

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Mkuu umeongea jambo la msingi sana. Kuna jamaa yangu mmoja alikuwa accountant ktk shirika moja kubwa sana hapa nchini. Hatimaye alifukuzwa kazi kwa sababu nyepesi tu lakini hakukata tamaa. Baada ya kufutwa kazi akaamua kusoma sheria. Mwaka jana alihitimu PhD ya sheria kutoka Tumaini University, ambako amekuwa akifundisha tangu alipohitimu Masters degree. Huyu jamaa pia ni wakili maarufu sana...anamiliki kampuni ya uwakili jijini Dar. Kuna siku nilimsikia anamshukuru sana mwajiri wake wa kwanza kwa kumfuta kazi kwa kuwa vijana wenzake wote aliowaacha pale wamekufa kwa UKIMWI kitambo sana. Huenda naye angekwisha kufa. Sometimes mambo kama haya hutokea kwa makusudi maalumu. Unaweza ukadhani Mungu hajakuona kumbe anakuepusha na matatizo. Mungu akikufungia dirisha, hukufungulia mlango wa mafanikio. Hakuna kukata tamaa.
 
Najuta kuamua kubaki kazini kwangu wakati nilifanya interview kwenye taasis nyingine ya fedha nikapata ila nikaona basic salary itapungua elf 50.sasa kwetu kila Mwaka salary inaongezeka 5 to 7 % wakati huko kumbe ni 15 to 20 %.sasa ni miaka4 .
mkuu asilimia 15-20 kila mwaka hakuna taasis yenye jeuri hiyo manake after 5 years mshahara una double what a big joke.
 
Inawezekana nae anajuta huko aliko msamehe ili milango ifunguke kwako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…