Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

nafikiri ulikua sahihi mwanzo kwakua nia nikukimbia nyumba zakupanga ukiwa kwako unaweza jiendeleza taratibu kulingana na mahitaji.
Wakati unakimbia kodi mara nyingi huwazi dada wa kazi atalala wapi lakini huyu ni sehemu ya familia.
 
kujenga mjengo mkubwa wenye complication kibao za rooms ambao haukuwa na ulazima sana hadi majirani mtaani na wapita njia walijua lodge, pia kuamini dawa ya mbao niliyopakiwa pale niliponunua mbao nikapaua hivyo hivyo. Next time mafumdi mjipange, ela mtakula ila kwa jasho na mtafanya kazi huku mnanielekeza hatua kwa hatua na mimi nitakuwa nachangia.!
Mninga mchwa hawawezi kula
 
Mimi nilinunua eneo dogo kwa milioni 4 ni 20*20 tukakubaliana na mwenyeeneo niongee 4m zingine aniongezee 20*20, nikaenda kukopa bank kurudi nakuta amepauza, ikabidi ile hela nianze ujenzi nyumba ilichukuwa miaka 4 kufikia hatua ya kuhamia nikiwa namaliza vitu vichache vilivyobaini.

Chumba changu cha master nilikijenga sehemu mbaya hakina upepo, vyumba 2 sio masters na ni vidogo ukipata ugeni ni shughuli.

Parking ni ndogo.
Hela ingeruhusu ungeenda vertical, chini jiko, dining sebule, choo cha wageni na master bedroom. Juu vyumba vya watoto na family bathroom.
 
. Najutia kwenda kujenga nyumba maeneo ya karibu na bagamoyo kwa kudanganywa na awamu ya nne kuwa bandari itajengwa soon,bwana weee!! Tunajuta mpaka leo na washkaji zangu,nyumba ambazo zingekuwa maeneo ya karibu na tegeta tungekula kodi hadi laki tano kwa mwezi,

Sasaivi tunaambulia kodi ya laki na nusu eti nyumba nzima
 
Mambo yatabadilika tu, kuanzia Vikawe mpaka Bunju jiandaeni. McJobs alirudi kurndeleza bandari kodi ırağıma 2M kama Sinza
 
Labda mti wa mlingoti,maana ni mgumu balaa,ile miti ya nguzo za umeme,

mchwa nuksi kabisa,sijui wanafaida gani hadi Mungu aliwaumba mchwa na kunguru
Miti ya mlingoti si ndiyo inatla sufi. Miti ya Nguni za umeme ni mitiki
 
Hela ingeruhusu ungeenda vertical, chini jiko, dining sebule, choo cha wageni na master bedroom. Juu vyumba vya watoto na family bathroom.
Sure nilikuwa muoga sana, Mungu ameijalia naanza mwakani sehemu nyingine
 
Wawekee watoto en-suite na uanze kuwapa jukumu la uşağı wa chumba na choo chake.
 
Niljenga nyumba kubwa kuzidi mahitaji wa familia yangu na uwezo wangu. Sebule kukwaa, jiko kubwaaa, dinning kubwaaa, stoo kubwaa na coridor kubwa mbele na na jikoni. mwaka wa 10 sasa nyumba haina finishing ya maana.

Mbaya zaidi nikaweka chumba kimoja tu kuwa self wakati vingine vyote vinne vya kulala vikitegemea bafu moja na choo kimoja. Ni makosa ambayo sitakaa niyafanye tena nikifanikiwa kukamata fyedhaa.
Asubuhi watu wanasubiriana kutumia choo
 
Back
Top Bottom