Ni kosa kubwa sana kwa askari kunyang'anywa silaha yake

Ni kosa kubwa sana kwa askari kunyang'anywa silaha yake

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Nilipitia mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kwa mwaka mmoja miaka hiyo. Baada ya kumaliza ukuruta (pass out) tulipatiwa uwezo wa kulinda vituo mbalimbali kwa kutumia silaha za moto. Onyo kali tulilopewa ni kuhusu ubaya wa askari kunyang'anywa au kupoteza silaha yake, kofia, buti au chochote kinachomfanya aweze kutimiza majukumu yake ya uaskari.

Tufanye nini ili wananchi tuambiwe ni kwanini askari wetu walipokonywa silaha zao na Hamza?

Kwanini Hamza asingeachwa ili ahojiwe zaidi yeye mwenyewe?

Hakuna aliyestahili kujiuzulu kwa tukio lote lile?
 
Jaribio lolote kuichukua silaha ya askari akiwa anatekeleza majukumu yake ni kucheza na kifo.jambo lolote litakalotokea kama madhara ya jaribio hilo ni juu yako, hamza kwa kujua hilo aliua askari kwanza kwa kutumia bunduki yake pistol. ieleweke kwamba pistol sio upinde au manati ni bunduki pia,tena hatari zaidi kwa polisi maana haionekani kirahisi na ni rahisi kubebeka.

raia wengi wana ufahamu wa hatari iliyopo kwenye silaha hii aina ya bunduki,ni kichaa au mgonjwa wa akili ndiye anaweza leta mzaha ama umwamba mbele yake.

umeshaambiwa hamza ni gaidi,kama ambavyo wale wa kibiti,mkuranga,stakishari nk,bado unataka kujua sababu ya yeye kuwapora silaha!!!alikuwa na kazi nazo za kuua polisi wengi zaidi kama alivyokuwa akipiga kelele kuwaita.
 
Kuna baadhi ya askari ni wazembe kinyama. Kwanza kitambi kubwa kama gunia la mbaazi.
uzembe ni swala jumla jumla,sio kila mwenye kitambi ni mzembe.wengine wana miili ya chakula tu kama samo hang.
 
Nilipitia mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kwa mwaka mmoja miaka hiyo. Baada ya kumaliza ukuruta (pass out) tulipatiwa uwezo wa kulinda vituo mbalimbali kwa kutumia silaha za moto...
Fanya shughuli zako tu mambo ya Hamza achana nayo wala hutapata majibu sahihi.
Tunaweza jadili mambo mengine ya nchi
 
Hamza kawapokonya vizuri tu!
Hamza alifanya ambush... Kwenye ambush hata awe komando ananyanganywa silaha vizuri tu maana kwenye silaha wa kwanza kubonyeza trigger ya silaha yake ndio mshindi.

Bunduki sio Kama jiwe kile ni chuma kikipita kwenye nyama ushaisha mapema tu.

Kwa hiyo kwenye ambush kijeshi mkitegwa hata platoon nzima inaweza kumalizwa na maadui wawili tu.

Tulishapigwa ambush kalemie Congo kwenye oparesheni ya kijeshi. Usiombee.
 
Hamza alifanya ambush... Kwenye ambush hata awe komando ananyanganywa silaha vizuri tu maana kwenye silaha wa kwanza kubonyeza trigger ya silaha yake ndio mshind...
All in all Hayati Hamza amewapokonya askari silaha vizuri tu.
 
Nilipitia mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kwa mwaka mmoja miaka hiyo. Baada ya kumaliza ukuruta (pass out) tulipatiwa uwezo wa kulinda vituo mbalimbali kwa kutumia silaha za moto. Onyo kali tulilopewa ni kuhusu ubaya wa askari kunyang'anywa au kupoteza silaha yake, kofia, buti au chochote kinachomfanya aweze kutimiza majukumu yake ya uaskari...
Mkishakula mihogo ya kukaanga mkishiba basi mnaandika chochote. Unajua ambush wewe?
 
Nilipitia mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria kwa mwaka mmoja miaka hiyo. Baada ya kumaliza ukuruta (pass out) tulipatiwa uwezo wa kulinda vituo mbalimbali kwa kutumia silaha za moto. Onyo kali tulilopewa ni kuhusu ubaya wa askari kunyang'anywa au kupoteza silaha yake, kofia, buti au chochote kinachomfanya aweze kutimiza majukumu yake ya uaskari.

Tufanye nini ili wananchi tuambiwe ni kwanini askari wetu walipokonywa silaha zao na Hamza?
Kwanini Hamza asingeachwa ili ahojiwe zaidi yeye mwenyewe?

Hakuna aliyestahili kujiuzulu kwa tukio lote lile?
Uzembe...uzembe..uzembe..kuanzia mauaji, matangazo yake, rulling ya jeshi nknk All inclusive was too unprofessional! And neglence at high level!!!

Sent from my Infinix X692 using JamiiForums mobile app
 
Kwa hali ya kawaida askari mwenye bunduki anatakiwa akae mita kadhaa na mtu kwa hali ya kawaida angalau mita moja, ili kitendo chochote kitakacholeta mashaka ukigundue mapema na ua act without hesistation , Ila ktk ambush .uchomoki labda target ikukose
 
haya mtaalam twambie inatakiwa iwe angalau mita ngapi??ambapo pistol haifikishi risasi??
 
Uzembe...uzembe..uzembe..kuanzia mauaji, matangazo yake, rulling ya jeshi nknk All inclusive was too unprofessional! And neglence at high level!!!

Sent from my Infinix X692 using JamiiForums mobile app
wewe ni mkubwa kuliko mawazo haya mkuu.

haipendezi wakati wote watu wakakwambia fani yako ni ulozi.wakati unafanyia hobi tu.
 
Back
Top Bottom