Ni kosa kubwa sana kwa askari kunyang'anywa silaha yake

Wanapenda sana kula viporo makambini et wanaita vijogoo au ugali pande unaliwa saa mbili asubihi
Kuna mmoja alikuwa anakula ugali Hadi 3 asubuhi tena ule Inga WA watu WA musoma halafu wanaanza patrol. Huyu akikutana na Hamza atampa bunduki Kwa hiari.
 
Umejuaje?
 
Mkuu kitambi ni dalili ya uzembe. Uzembe wa kufikiri, kwanini ule chakula kupita kiasi kinachohitajika na mwili wako?
Mkuu una umri gani?
Nimeuliza hivyo kutokana na dhana zetu kufanana, lakini baadaye mwenzako nilikuja kubadilika kwa kuujua undani wa kisababishi cha unene hata kama hauupendi.
 
Mkuu una umri gani?
Nimeuliza hivyo kutokana na dhana zetu kufanana, lakini baadaye mwenzako nilikuja kubadilika kwa kuujua undani wa kisababishi cha unene hata kama hauupendi.
Mkuu nipo kwenye late twenties. Hebu nieleweshe mkuu elimu ni muhimu na haina mwisho.
 

Hata mbowe wanamuita gaidi. Ficha Ujinga wako
 

Baki hivo hivo.
 
Swala la kutumia SILAHA NI SWALA LA "TIMING" Tusiwe wepesi kulaumu eti askari wazembe. Ukishafanyiwa TIMING hata ungekuwa na kombora halitakuwa na faida kwako!
Mnaporwa hivihivi
 
Kila mtu aliyepata mafunzo ya kijeshi anafahamu kuwa silaha moja lazima ilindwe na siliha nyingine, silogan hii inatimia kwa kujipotion TU. Kwenye lindo mtakaa vipi ili silaha ya kwanza ilindwe na silaha ya pili. Polisi wetu walipokonywa silaha zote mbili na mtu mmoja TU tena raia.
 
Askari wetu ukiwatuma waende kusimamia usalama kwenye viwanja vya mpira wanashindwa kumuona aliyerusha chupa ya mkojo uwanjani, maana na wao wanaangalia mpira kama wengine tu.

Wale askari wa uingereza wanageukia mashabiki kuona usalama ukoje askari wetu wao wanageukia uwanjani ili wacheki mechi vizuri
 
Kuna aina 8 za kunyang'anya silaha za moto na 21za mchanganyiko sasa wewe unasema aina ipi?
Ninasema aina ile ya askari 2 wenye silaha wakapokonywa silaha na mtu mmoja tu kwa wakati mmoja bila ridhaa yao wakiwa na akili zao timamu sehemu yao ya kazi.

Nini maana ya kupiga doria?
 
umeshawahi kutana na hao wanajeshi wakilinda mipaka!!!

wanabeba silaha ngapi shingoni,kama kweli wapo???
Kule Ethiopia na Rwanda katika kila lindo kuna askari ambao lindo lao liko juu kabisa (dungu) kiasi cha kumuona kila mtu anaekuja na kutoka eneo la lindo . Hapa kwetu unaweza kumpora polisi chochote kama ukitaka.
 
Wale askari wa uingereza wanageukia mashabiki kuona usalama ukoje askari wetu wao wanageukia uwanjani ili wacheki mechi vizuri
anaweza kupokonywa kirungu wakati wowote kutoka nyuma.
 
Umeambiwa aliwapiga risasi akawauwa kwanza ndio akazichukua .hamza hakuenda moja kwa moja kuwanyang'anya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kosa kubwa kwa askari kunyang'anywa silaha na mtu mwingine ambaye hana silaha. Sidhani kama ni kosa kwa askari kunyang'anywa silaha na mtu ambaye naye pia ana silaha, kwa sababu katika mazingira ya namna hiyo wawiili hawa wanakuwa katika mazingira ambayo ni ya kivita. Vita havina macho
 
Hakuna mtu ambae hana silala. kucha, meno, jiwe, wembe, kisu, panga, fimbo, jembe, upupu vyote ni silaha. Kunyang'anywa ni kunyang'anywa tu itategemea aliyenyang'anywa alikuwa na weledi wa kazi yake kiasi gani, alikuwa na utimamu wa afya na akili kiasi gani, alikuwa na silaha kubwa kuliko ya adui kiasi gani na waliomyanganya walikuwa wangapi.

Ndiyo maana kaka ukubwa wa mafunzo na silaha zinatofautiana. Mtu mmojs mwenye bunduki ya pistol, SAR au G3 kunyang'anya watu 2 wenye bunduki aina ya SMG au AK47 au LMG lazima kuna factors ambazo hazikuzingatiwa.
 
Nilimaanisha silaha nyingine ya ziada nje ya viungo kamilifu vya mwili wa mwanadamu. Silaha iliyotengenezwa kwa makusudi ya kutumika kama nyenzo
 
Ndiyo maana kaka ukubwa wa mafunzo na silaha zinatofautiana. Mtu mmojs mwenye bunduki ya pistol, SAR au G3 kunyang'anya watu 2 wenye bunduki aina ya SMG au AK47 au LMG lazima kuna factors ambazo hazikuzingatiwa.
LMG na hizo zingine ulizozitaja, huwa zinapiga target iliyo karibu na mwenye silaha? Mtu yuko karibu na wewe mnaongea wawili, LMG inakusaidiaje katika mazingira ya aina hiyo, just in case akiamua kukugeuka ghafla? Ulipita JKT wapi wewe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…