DOKEZO Ni kweli Hospitali ya Taifa Muhimbili kulala kwa siku ni gharama zake ni tsh 50,000?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Haijalishi, je umma wa Watanzania unamudu hizo gharama? Tukizungumzia umma ni lazma ufuatilia the lowest income earners of the country. Mtu analipwa laki na nusu kwa mwezi. Je, akiumwa anatibiwaje hapo?

Huyo mbunge rafikio anaweza kwenda kulala hata wodi ya million kwa siku maana bunge linamlipia. Wewe unaweza lipa hio elfu 50 maana unaweza kuwa unatengeneza 6 times the sum of money kwa siku.

Je, yule mtanzania muuza maji ya kandoro atawezaje kumudu kumlipia mzazi wake alielazwa elfu 50 kila siku?
 
Mama katoa million 700 kwa kushabikia mpira, angekuwa mshabiki wa matibabu weñgi wangepona.
Vipaumbele hatuna hii nchi, katika sector ambayo haitakiwi ubabaishaji ni sector ya afya. Mtaji wa kwanza wa nchi inayojitambua ni raia wenye afya njema ili wazalishe mali kwa wingi na walipe kodi. Sio siasa chafu na wizi wa kura kama ambavyo jamuhuri ya Mogadishu inavyofanya. Wanatumia nguvu wasalie madarakani ili waendelee kulidhoofisha taifa kwa rushwa,ufisadi na kujilimbikizia mali. Very sad thing.
 
Chadema wakiwahimiza muitoe madaraka hii takataka ya fisiemu mnawaona kama wajinga, sasa hayo ndio matokeo yake.
 
Kaka unaogopa nini kusema Jamhuri ya Tanzania ?
Hatuwezi pata mabadiliko kama hata jina la nchi hii nzuri inayoharibiwa na masisiemu mnaogopa kulitaja.
 
HIZO NI GHARAMA ZA ICU
 

Nakubalina na Wewe kabisa 100%
Kama tukibadilisha Sera na Wizara ya afya ipokee Ruzuku na Hospitali Zisijiendeshe zipokee Pesa Moja kwa Moja kama vipokeavyo Vyuo na Mashule Tunaweza Kumudu Gharama
Umetufumbua macho wengi kuwa serikali haitoi ruzuku kwenye mahospitali hivyo zinajiendesha zenyewe kupitia michango.
KIUFUPI SERIKALI IMETUTUPA WENYE KIPATO CHA CHINI.
 
Sijaelewa kinachofanya hiyo hospital gharama zake kuwa juu kuzidi Johannesburg Hospital wakati ni Hospital ya Serikali achilia mbali gharama za vipimo utasikia laki mbili na nusu kipimo kimoja mara hiki na hiki laki sita hapo ni siku moja matibabu ya wiki hapo inakua balaa..
 
Mkuu watu wanapozungumza gharama za Hospital wanazungumzia kwa ujumla kuwa hiki Watanzania wengi wataweza kumudu sio kwamba ukiwa na Bima wewe basi hata ndugu wengine kutoka Kongwa huko na pia wana uwezo wa kuwa na bima ondoa ubinafsi harafu uelewe mtoa hoja anamaanisha nini..
 
Watanzania wengi wamedumaa sana na ubinafsi ndio upo vichwani vyao yeye akiwa na Bima na kipasso wakati ndugu zake hawana hizo Bima anajibu anavyotaka tu hapa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…