DOKEZO Ni kweli Hospitali ya Taifa Muhimbili kulala kwa siku ni gharama zake ni tsh 50,000?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Serikali inawekeza palipo na hisia za wananchi. Mfano hivi sasa ni mipira na kamari hivyo fedha zitaelekezwa mlikoekekeza mioyo yenu ili wao waendelee kula kuku kwa mrija bariidii.
 
nadhani lawama zake anazipeleka kwa serikali na sio uongozi wa Muhimbili. serikali ina mawanda mapana kufanya kitu kuboresha huduma na kufanya ama kuwa bure au affordable. pesa nyingi zimeelekezwa kwenye anasa bila kusahau na mirija ya upigaji uliokithiri
 
So what?
 
majibu kama haya yana justify utumbili wa jamhuri ya ukimani 🐵
tatizo watu wanakua wakali kama pilupili tukipaita ukimani
 
majibu kama haya yana justify utumbili wa jamhuri ya ukimani 🐵
tatizo watu wanakua wakali kama pilupili tukipaita ukimani
Bora mliopakimbia maana its hard to stand infront of people and introduce yourself as a United Republic of Mogadishu Citizen.
 
Gentleman,
zidisha juhudi katika kufanya kazi. Na ni vizur zaidi uwe na bima ya afya. itakusaiadia sana wewe na familia yako...

Sasa puuza mawaidha haya,
wewe ng'ang'ana kwa bidii kutafuta na kuipa kipaumbele simu ya bei ghali, huku ukipuuza jambo muhimu kama afya yako na familia yako, utakuja kuumbuka kwa kushindwa kununua Panadol huku unamiliki iPhone6?

Je, hilo sio tatizo la Afya ya akili hili kweli gentleman 🐒

kwamba gharama ya afya ni juu zaidi, kuliko smartphone unayoimiliki right?

kutafuta huruma eti gharama fulani za afya ni ghali ni nonsense na completely useless,🐒
 
Nina Bima ya kutibiwa Great Skill hospital ya Cape Town gharama za usafiri ni zao kwa tuliobeba box De beers Marine tulikua tunakatwa hela nyingi sana kwa ajili ya matibabu tu ndio ambayo kwa sasa imekua hazina kwetu mwanzo ilikua inabeba hadi wazazi sasa hivi ni mke na watoto wanne tu...
 
nimefurahi mno kuweka kipaumbele muhimu cha afya kwenye bima. Angalau una uhakika wa tiba.

Inashangaza jamii,
kwa kiasi kikubwa eti kipaumbele wameweka kwenye kushindana kumiliki simu smartphone toleo jipya ya maana , na kukesha clubs kula bata huku suala la afya likiwa sio kipaumbele kabisa.

subiri augue sasa, anavyolalamika gharama za matibabu.🤣

Tujali afya zetu ndrugo zangu.Afya ni uhai na sio smartphones🐒
 
Kwani Basket Fund inaenda wapi siku hizi?
Basket Fund Muhimbili Mkuu?
Hata Kwenye Hizo Hospitali za Wilaya na Mikoa basket fund hutolewa Pesa Kidogo sana na Bajeti ya Pesa Zake Shughuli zake Nyingi zimejikita kwenye Huduma Ya mama na Mtoto na RCH kwa ujumla Ila Zehemu zingine hakuna
 
Mzee Nilifika Kuangalia Siku moja Bima ya Texas Marekani Duh bima Ni mamilion ya Tsh kwa Mwaka..
Mtu analipa Takribani Milion 7 Kwa ajili ya Bima kwa Miezi 12 tu Kutibiwa..
Nilishangaa Sana...Kwetu mtu analipa 155,000/= kwa mwaka ola anatamani Apate huduma anayoilinganisha na Texas..

Tufike mahali sisi kama Sisi Tuisaidie Serkali Kwenye Viti ambayo tunapaswa sisi kuwa Kipaumbele..

Mtu unashindwa Kutoa Pesa ya Bima bado unapunguziwa halafu bado hutoi hiyo pesa halafu unalia Kutokutibiwa Vizuri
NI haki??
 
Ni rahisi kuongea hivyo kama unaishi maisha ya kulipiwa kila kitu na ofisi au kampuni.
Hapana Mkuu ni rahisi Kuongea Negativity kama Huishi maisha hayo..
Mimi ni mmoja wa watu tunaoona karaha kuhusu Hilo jambo tunatamani hata Angalau Mtu angelipa 100k kulipia Huduma hiyo ila tunaona Tuhurumie mwananchi asipate mateso lakini kwanini usikate bima Siku hizi 200k unapata bima ya Mwaka..
Unaweza ukatibiwa Muhimbili na kulazwa unavyotaka
 
Na Ndiyo maana Kunakuja Swala zima la Ofisi za Ustawi wa Jamii?
Kazi kubwa ya Ofisi za Ustawi wa jamii au Ofisa wa ustawi ni Kufanya makadirio ya Mtu asiyejiweza Kulipia matibabu na Kumpigia Hesabu au Kuweka Mkakati hasa Lini na Jinsi gani ataweza kulipa madeni yake..

Na kama Haiwezekani Ni jinsi gani anaweza kupata Msamaha..
Kuanzia mwezi wa Nne mwaka jana 2023 Mpaka mwaka huu naweza kusema Muhimbili Imesamehe Madeni au imetoa msamaha wa Madeni ya Dawa na Huduma Zaidi ya Tsh bilion 29...
Mbona Hiyo hamtaki Kuisema??
 
Hatimae Muhimbili inaenda kuwa hosptali yenye hadthi ya hosptali ya kitalii maana sio kwa bei hio.....
 
Kumbuka siyo kila kitu kina linganishwa. Yani Unalinganisha Texas Marekani na Tanzania? Dunia ya kwanza na Dunia ya 100 sijui?

Kipato chetu na chao havilingani, na hata standard za huduma wapatazo ni tofauti na tupatazo hapa kwetu. Na kama ilivyo kwa Tanzania hata marekani raia wengi hawana health insurance kwa sababu hawawezi kuzimudu. Wengi wenye Health Insurance huzipata kupitia kwa waajiri wao kama tu ilivyo hapa kwetu.

Gharama inatokana na package anayo weza kumudu, hata wao siyo suti kwamba one fit all. Ni wachache wanaweza kujinunulia Health Insurance huko Texas Marekani kama tu ilivyo hapa kwetu.

Kuhusu gharama, nadhani wao hupata value of their money, hapa kwetu hakuna kitu, kila kukicha NHIF wana hamisha magoli, utasikia utapata vipimo vya awali vya damu, vipimo zaidi utalipia, au utasikia huduma za tiba ya mionzi na uchunguzi wa mionzi utajilipia. Lakini utakuta wenzetu kule hizo huduma za uchunguzi wanapata zote kwenye basic package isipokuwa specialized procedures ndizo wanabidi wajipange.

Na hata hivyo wao sheria inawasaidia, mgonjwa hanyimwi huduma hata kama hawezi kumudu huduma atapata, deni litapelekwa kwa serikali.

Muhusika atakua na deni lakini halitomfanya ashindwe kuishi maisha yake, kwa maana nyingine siyo lazima alipe.

Hapa kwetu Insurance gharama iko juu sana ukilinganisha na vipato vya wananchi waliowengi. Sioni kama ni sawa kulinganisha gharama anazolipa mwananchi wa Texas marekani na hapa kwetu.
 
Maombi yanahitajika.
 
Karibu JAKAYA KIKWETE CARDIAC INSTITUTE tawi la Muhimbili.
Ukienda siku ya kwanza na matatizo yako ya moyo jitayarishe kwa haya.
Kumuona Daktari 35000 ( hii ni kila unapokwenda)
Vipimo vyote kabla ya kuanza matibabu Echo,X ray, Stress ,maabara kama huna bima tayarisha 700000- bado kuna dawa zinazo uzwa mara mbili ya bei za pharmacy za watu binafsi mjini..
Mwisho siku ya kwanza utaenda alfajiri saa 12 utatoka jioni saa 11.
 
Kipato cha USA ni sawa na huko Tanzania au unaongea tu Mkuu kwa nini unafananisha Nchi ambayo ishaendelea na wanaojitafuta kwenye Bajaji na Boda boda..Wabunge wao tu wanatakiwa wajue kusoma na kuandika ili Nchi iendelee..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…