Ni kweli Mbowe kachoka, lakini Lissu sio mtu sahihi wa kumwachia chama

Hata Samia mwanzo tulizani ni tofauti na mwendazake lkn alipoanza kutoa makucha tukajua rangi zake, same na Lissu kabla ya kugeuka tulidhani ni mtu sahihi.
Mkuu kubali kuchutama, ushavuliwa nguo kisomi.

Micomment yako tena ya siku za baribuni ndiyo yaliyokuacha uchi.

Kwa points hizo diyo maana watu wanaona kama umehongwa na team Mbowe.

Kwani kuendelea kujitetea unataka ushindi na ukishinda utapata nini?
 
Ina maana wewe umehongwa na nani.
 
Asilimia kubwa ya Watanzania wako hivi yaani ni wanafiki.😆😆😆😆😆😂😂😂
 
Kwani Chama ni mali binafsi ya Mbowe kwamba ni chake na Lissu siyo mtu sahihi wa kumuachia? Kwamba chama kakishikilia Mbowe mpaka useme hawezi kumuachia Lissu?

Nyie wafuasi wa Mbowe tutawachapa sana humu jukwaani. Hatutakuwa tayari kumpamba Mbowe kwa njia yoyote ile fahamuni hilo. Mbaya zaidi hatutaipigia kura Chadema maana mkivimbiwa ruzuku mnajisahau sana mnajiona nyie ndiyo mwisho. Tupo huku tutakutana kwenye debe.
 
Mwisho wenu January.
 
Mwisho wenu January.
Mwisho wa Mbowe au unamaanisha nini? Sikia nikwambie fanyeni kama mnajikuna mummrudishe Mwamba kwenye kiti ndipo mtajua hamjui. Kama mnadhani tunatania basi endeleeni na kejeli. Kitakufa bila kelele.
 

Ila alikuwa mtu sahihi kuongoza Inchi
 
Wachaga/wamachame wamepagawa
Inonesha mna chuki sana na wenzetu wachaga, ila wa mbili ni wa mbili tu.
Hatred yenu haitakaa ibadili mambo.

Kikwete: "Kama watanzania wangekuwa wachapa kazi kama wachaga, Nchi ingekuwa mbali sana kimaendeleo"
 
Miamba inataka sanduku la kura.Ili wajipime nani mbabe wa mieleka ya Soumo.
Wapiga kura ni wajumbe tu.
Kura za wajumbe 1200 ndio utakuwa ufunuo wa Chadema 2025.
Kura sio electronic voting bali manual.
Ikiwapendeza wahesabiwe wapiga kura, wapange line tatu yaani Mbowe,Lissu na wasiokuwa na upande.
Atakaeshindwa akili mbele ya wajumbe kuwa ameshindwa kihalali.
Misimamo ya wajumbe nadhani inajulikana.
 
This sounds true. Nadhani itoshe kusema Mbowe ni tatizo.
 
Mbowe alikuwa na muda wa kutosha kuachia hicho kiti, lakini ameng'ang'ania hadi mabadiliko yamemkuta. Ni kweli Lisu anaweza asiwe kiongozi mzuri, lakini ndio mwenye uwezo wa kuhakikisha huyo king'ang'anizi wa madaraka. Hivyo hapa Lisu sio wa kulaumiwa, ila Mbowe ajilaumu mwenyewe.
 
SIASA ni kama PLACEBO,,, KIPO lakini HAKIPO , because SIASA ni MCHEZO wa MATAPELI.
 
Facts hujaziweka zaidi ya porojo
 
Ajilaumu nini wakati anaenda kushinda kwa kishindo, wa kujilaumu ni Lissu anayekwenda kukosa kila kitu.
 
Ajilaumu nini wakati anaenda kushinda kwa kishindo, wa kujilaumu ni Lissu anayekwenda kukosa kila kitu.
Mbowe kushinda kwa kishindo sio hoja maana ana hela za kuhonga wajumbe kadhaa, tatizo liko kwenye mvuto wake wa kisiasa kwa wafuasi wa cdm. Mbowe akishinda itakuwa kama Lipumba alivyoshinda CUF, kisha Maalim Seif mwenye ushawishi akasepa na wafuasi karibia wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…